Mke wangu habebeki...

Standard gani asiyoweza kuihudumia mwenyewe_standard unaiishi kwa kuomba omba na kusaidiwa na wengine,..a good standard to live ni ile unayoweza kui_finance kulingana na cash flow yako mwenyewe.
 

...hhaahha ha... ni ukweli usiopingika bana! ...



kweli tupu!...kuna baadhi ya wake wanaishi vile walivyozoeshwa...kama ulishamzoesha high life,
kumshusha ni shughuli!
 

JS Jama umeolewa nakupa pole, na mumeo nampa pole pia mana huna heshima kwa mumeo.

''Utasemaje upate mume kama huyu....''Ina maana mume uliyenae hakufai kwa kuwa tu hana fedha?!Halafu pesa si mwisho wa matatizo.
 
mnachokisema ni kweli ila wazazi wangu wanamtetea sana..hata sijui hawewapa nini?
Hiyo ni sababu ya ziada kuona kuwa huyo ni nyoka, anatafuna na kupuliza. Anajaribu kuwarubuni wazazi wako aonekane mwema, lakini kwa wewe anafanya anayoyafanya.
 
ungekuwa hapa karibu nikekupa hug moja la nguvu yaani kuna watu hapa bongo wanaishi maisha ya kusikitisha kuna mdada nipo nae ofsini mtoto wake wa primary kwa mwezi analipiwa 60% ya mshahara wake bado nyumba bado gari yaani anaishi kwa kuungaunga vibaya,hana saving yeyote. watu wanaitaji somo la financial management jamani
 

...

kweli tupu!...kuna baadhi ya wake wanaishi vile walivyozoeshwa...kama ulishamzoesha high life,
kumshusha ni shughuli!

Na kuna baadhi wanaume wanaotaka wake zao waishi high life ila hawataki kufacilitate kufikia hiyo high life.
 
Reactions: Mbu
Hivi bado hujampiga chini tu!!!
 
Yeah_man!...umeongea kitu hapo mkuu,...nakumbuka maisha flani nimewahi kuyaishi nikiwa kwa bro kitambo kidogo ni mazuri lakn hayafai kabisa kuizoesha familia,....hapa tunahitaji kujua huyu jamaa aliichaachaje familia yake hapa bongo_asije kuwa yeye ndiye cause ya usumbufu wa mkewe.
 
Nawashukuru wandugu kwa mchango wenu wamawazo mazuri nitafanya maamuzi then jumapili nitawapa feedback..
 

...hhaahha....fa unaua!....
ukishazoea kipato cha kuajiriwa, ni shughuli kujiajiri!
tena kwenye system zenyewe hizo za kujuana bongo ndio kabisaaa!

anyway, ...kama asemavyo jamii01, anasoma kwanza,
labda tungemshauri amuanzishie mkewe mradi ausimamie
badala ya kumtumia pesa.
 
Hivi na huyo mtoto una uhakika ni wa kwako!!!
 
unaweza kukuta kawaacha appartment za masaki dollar 1500 kwa mwezi jamani
 
mnachokisema ni kweli ila wazazi wangu wanamtetea sana..hata sijui hawewapa nini?

Maamuzi ya maisha yako mikononi mwako na si wazazi!mwagia mbali kabla hajakumaliza!heri nusu shari kuliko shari kamili
 
Pole sana kwa kweli. Huyo ni kati ya wanawake wapumbavu wanaobomoa nyumba zao kwa mikono yao wenyewe.
 
Reactions: Mbu
Nimekupata FA na kama umeacha mke bongo yep nakubaliana na wewe ni vyema ukajiwekea malengo na limit kwani mimi ni mmoja ya wasioamini kwamba relationship ya mbali inawork! Lakini nikimuangalia huyu jamaa nadhani amejieleza kwamba yuko huko kimasomo hivyo vijidola anavipata kwa kupigika na boksi tu, labda atujulishe nini malengo yake? atarudi baada ya masomo au ndio imetoka? maana hapa kuna mengi sana yamejificha kwenye hii stori ila mimi kama hawakuachana muda mrefu basi nashawishika kwamba mdada ameingiwa na mentality ya kwamba hazbendi wake yuko majuu hivyo na yeye anastahiki kuishi maisha ya juu.
 
Jamani huyu mke nyumba ya kwangu mwenyewe hakuna anacholipia zaidi maji na umeme nazo ninalipa mie kutoka kwenye biashara zangu ada ya mtoto nalipa mwenyewe moja kwa moja kutoka kwa bro wangu ndiye niliyemkabidhi swala la shule hakuna kitu kingine.
 
Pole sana lakini chakufanya kama bado unampenda na unataka kua nae mueleze kua unataka abadilike,haijalishi kama anapendwa na wazazi au anapenda na mawifi siku pesa ziikisha hatokua na wewe huyo, kama ulikua unapeleka 1000usd sasa peleka 500 nyengine weka mtoto usimpeleke muachie sababu yeye ni mama akisema pesa haitoshi mwambie ajipange itoshe au akueleze matumizi yake yakoje,manake utakuja kujuta baadae,pole sana hawa wanawake wengine wanatutukanisha sana kwa ujinga wao basi hapo hana chamana anunue bazee cm mpya achukue pesa amchangie shoga anaharusi ya mdogo wake ,aende Twanga akatajwe jina ndio ajione na yeye mjini yupo puka chaka....
 
Yeah_suali la msingi sana hili,..maake kuna makabila mengine hawaridhiki mkuu...wengi tu wahanga wa hili
Kama kuna ukweli wa hilo katika red ni sehemu ndogo sana. Nisingependa tuwahukumu watu wote wa kabila moja kuwa wana tabia moja. Kama ni tatizo la kutotosheka inaweza kuwa ni ulimbukeni wa huyo dada, kutokuwa na fikira za mipango ya baadaye na kukosa huruma. Bila ya kutumia jazba, tuangalie bajeti yake ya mwezi inaendaje - matumizi ya kila siku na ya mwezi au miezi kadhaa mara moja kama vile nguo na elimu ya mtoto.
Vyovyote iwavyo, mtu anapaswa kuishi "kwa kujikuna ajipatapo", tunapoanza kujilinganisha na walio juu yetu ndio mara nyingi tunaharibikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…