Watu humu ndan mshavurugwa au ni ujinga umewajaa. Kweli mtu kauliza kitu ambacho hakijui mtu anasema ni utoto mara cjui nini. Wewe mtu mzima kwa nini usimshauri kiutu uzima kuliko kumjibu kifala hivyo. Na kila sku ntasema sio kila uzi uujibu kwa matope yako pita kushoto na hautapungukia chochote. Hata kama mtu ni mdogo ana haki ya kuuliza jambo ili wewe mtu mzima umjibu na sio kumkebehi na vimatusi vy kijinga. Bora huyo alosema mimba tayari atleast inaleta jibu au alosema apge mswaki atleast nayo ina afya kidogo na sio huna akili, unafaa ufe, cju maada ya kitoto na wewe mwenyewe pamoja na swali la kitoto umekosa jibu na badala yake ni upuuzi unamwandikia. Hata bora mtu amjibu kuwa aongee na mke wake amwambie tatizo ni nini? Short simple and clear. Nyie watu nyie hizo akili mnazotumia kujibu mtu visivyo jaribu kubadilika. Hakuna point unapata unapomjibu mtu. Mtu mzima na nusu anajibu kitoto zaidi ya utoto wenyewe na hakuna faida mnapata. Pita kule kama uzi unakuboa punguza ujuaji mwingne wa kujizalisha mwenyew