Mke wangu hashiki mimba, naomba msaada wa mawazo

Mke wangu hashiki mimba, naomba msaada wa mawazo

Toka nimeoa nina miezi sita. Huwa tunahesabu siku ya 11 hadi 14 lakini hatujabahatika. Nini inaweza kuwa sababu ya hili? Tiba yake ikoje?

Msaada wa mawazo kwenu wataalamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Miezi sita bado ni mapema sana. Jipeni muda, fanyeni njia zilizo sahihi na mkiona mpaka miezi 8 bado hamuoni majibu ni vyema mkamuona Gynecologist ambapo atawafanyia vipimo nyote wawili na kuangalia tatizo lilipo kisha kuwapa tiba/ushauri wa kitaalamu.
 
Asante kwa ushauri Mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muulize Mara ya mwisho kuchoma sindano ya uzazi ilikuwa ni lini ili ajue muda bado wa sindano kuisha mwilini.Atapata tu
Unaona sasa!. . Masindano yenu yale, yameingia mwilini yameharibu mfumo mzimaa!!

Dawa hapo ni kuyaondoa hayo masindano mwilinii kwa kuDETOX mwilii
 
Toka nimeoa nina miezi sita. Huwa tunahesabu siku ya 11 hadi 14 lakini hatujabahatika. Nini inaweza kuwa sababu ya hili? Tiba yake ikoje?

Msaada wa mawazo kwenu wataalamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe una historia ya kumpa mimba mtu?

Usije ukawa Jux umeleta mada

Kati ya miezi 6 hadi 12 muoneni daktari au mtaalam wa uzazi awafanyie uchunguzi?
 
Me nina watoto wawili kwa wanawake wengine

Sent using Jamii Forums mobile app
Basi mwanamke wako anashida, ila huwa zinatibika kama sio critical.

Mwanaume huweza kutia mimba kila siku.

Ila wanandoa au watulioko kwenye mahusiano ambao wanafanya mapenzi mara 1 kila wiki wanatakiwa watunge mimba kati ya 6 hadi 12 nje hapo, wamuone daktari.
 
Asante kwq ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Stage 1,
Mnapaswa kujua mzunguko wake, usikariri siku ya 11 sijui 14 wakati mkeo mzunguko wake ni mrefu au mfupi, download app inaitwa FLO ipo playstore itawasaidia kutrack period, fertility days na ovulation day na zaidi itamsaidia kujua mzunguko wake ili muanzie hapo....

Stage 2,
Je, anapata siku zake kila mwezi bila kupitisha?
Je, anapata maumivu makali akiingia kwenye siku zake?
Je, damu inakua nyingi sana na kutoa mabonge kama maini?
Huenda ikawa chango na dawa ya chango tafuta wasukuma wanazo sana maana hospital hawana dawa yake zaidi watamwambia azae litapona... angalizo asitumie dawa chungu zinaweza kuzua tatizo jengine kubwa....

Stage 3,
Akapime kama kizazi kipo vizuri, Mayai kama yanapevuka na hormones kama zime balance...

Good Luck.
 
Toka nimeoa nina miezi sita. Huwa tunahesabu siku ya 11 hadi 14 lakini hatujabahatika. Nini inaweza kuwa sababu ya hili? Tiba yake ikoje?

Msaada wa mawazo kwenu wataalamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Miez 6 n michache kuanza kupata uoga. Miaka 2 ikipita ndo wasiwasi wahitajika.

Ila nakushauri nendeni hospital mukapime wote wewe mbegu zako kama nyepesi au huna uwezo wakubebesha na mkeo km anauwezo au lah, vp anapata ute cku za hatari? Vip a aujua mzunguko wake vizuri na ajue mzunguko wake ni wa siku ngapi kama 21/25/28/30/35?

Akishajua hivyo mutashauriwa cku za kukutana au mutapewa dawa na milo ya kula kama lishe.

Pia nataka kujua upo mkoa gani?
Ukipima mukakuta kila kitu sawa kuna dawa za mitishamba ni mzizi umesagwa unakunywa wewe na mkeo asubuh na jion ndan ya mda wa wiki 1 kuelekea kwa cku za hatari.

Ni bure tu nitatoa kama msaada ila kama utani offa si mbaya😊.
 
Toka nimeoa nina miezi sita. Huwa tunahesabu siku ya 11 hadi 14 lakini hatujabahatika. Nini inaweza kuwa sababu ya hili? Tiba yake ikoje?

Msaada wa mawazo kwenu wataalamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na
Me nina watoto wawili kwa wanawake wengine

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuwa na watoto wawil kwa mwanamke mwingine haikufanyi kuwa uko safi. Tatizo linatokea mda wowote na cku zinavyokwenda. Kumbuka kuna ugumba wa hatua ya pili. Yan unakuwa na watoto tayar ila utakavyoitaj zaidi na zaidi unashindwa kupatakutokana na mbegu kuwa nyepesi mno matatizo ya afya au ugumba wa ukubwani. Wanaume wengi wakishakuwa na watoto mwenzao akakosa mtoto wanazani wapo safi na kuwaza shida ni ya mwanamke. Kumbe shida inaweza kuwa ya kwenu wote au ya kwake. Vipimo ndo vitaongea na siyo dhana za kuwa na watoto tayar nje.
 
Huyo alishatoa mimba sana enzi za ujana wake?piga chini
 
Japo miezi sita ni michache ya wewe kuanza kupiga makelele, kunao tulipiga miaka miwili kabla kumpata mtoto wa kwanza.
Hata hivyo kama una haraka ya kupata mtoto, nendeni mkapimwe nyote na mfuate ushauri mtakaoupata wa kitaalam, ukimpa presha usije kulaumu kitakachotokea.
Pia jiandae kisaikolojia kwamba mtoto ni baraka ila sio lazima, maana ikija kutokea huna uwezo wa kumpachika mwanamke mimba au yeye hana uwezo wa kushika mimba, mumejiandaaje kwa matokeo ya kihivyo.
 
Toka nimeoa nina miezi sita. Huwa tunahesabu siku ya 11 hadi 14 lakini hatujabahatika. Nini inaweza kuwa sababu ya hili? Tiba yake ikoje?

Msaada wa mawazo kwenu wataalamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama hakuna dakatari wa kuwasaidia, badilsihen diet yenu muwe mnakula majimbi sana. Hamtakawia kutengeneza mapacha
 
Back
Top Bottom