Shida inaanza hapa, kwanza haujasema umemkosea kitu gani hadi akafikia hayo maamuzi.
Pili na muhimu zaidi, inaonekana haujajutia kosa ulilofanya, hadi sasa naona kinachokuumiza zaidi ni kuachwa na yeye kuwa na mwanaume mwingine, najua itakuuma lakini usipokua makini ataliwa na unaweza usijue.
Ikiwa unaenda kwake kumbembeleza kama ulivyokuja hapa, itakua unaendelea kumtia hasira tu. Haunyeshi kabisa kwamba ulichokifanya kimekuumiza, unajutia na unadhamiria kutorudia tena.
Pia kumbuka yule nae ni binadam, anahisia, anasikia uchungu na anakwazika kama watu wengine, mpe muda. Usimzonge sana, mwachie nafasi. Ilimradi amekuruhusu kuwaona watoto, hapo ndio iwe mwanya wa wewe kuonyesha ulivyobadilika. Acha aone kwa vitendo sio maneno.
Ni hayo tu mkuu, pole sana.