Mke wangu hatimizi majukumu yake ya nyumbani ipasavyo

Mnunulie mashine ya kufua, ni elfu 95 tu.
Na ya kufuta vumbi tv ipo pia?vipi ya kitandani? na kupanga siting room pia,na kutandika bedroom? ushauri huu wa under age.

Ni hiv,angalia trend,je hii ni tabia yake toka unamuoa? au ameanza karibuni?kama ni tabia yake toka zamani kabla ya kupata watoto hao wawili basi hiyo haiwezi badilika. Ila kama ni tabia mpya itabadilika ukizungumza naye kwa respect.usimfanye yeye kushinda home ndiyo hana cha kufanya.anza kutambua mchango wake kwenye familia kwa kukufulia nguo hata hizo chache,kulea watoto wenu,kukupikia,hata kama mchana hakuletei chakula huko ofisini kwenu,ila jioni unakutaga chakula ukirudi.hata tu kulinda nyumba yenu ni kazi kubwa.

Kifupi anza kutambua yale mazuri yake kwanza.ila kama unaishi na mke kama unaishi na mdada wa kazi,hata angekuwa mvumilivu vipi mwisho atachoka.

Labda nikwambie,kila ndoa unayoiona hapa duniani inachangamoto zake.Wako wanawake wanaofanya hayo uliyoyasema,ila pia ni wachepukaji,walevi,wachawi.wanachukia ndugu wa mme, so huwezi kuwa na mke mwenye sifa zote,yaaani in short hayupo,simply kwa sababu hakuna mwanadamu mkamilifu.

Naona umesema umefikiria kuwa na mchepuko,hilo ni bomu lingine bro. unaliandaa likulipue ufe.usijaribu hata kidogo.Ni bora uendelee kumkumbusha huyo mkeo hivyo hivyo kuhusu hilo suala la unyumba.

Tafuta tabia nzuri alizonazo na umpongeze na vifurahie.Ongea naye kwa heshima kama mke
 
Wengi huwa wana fake tabia zao pale mwanzoni,unachokiona sasa ndio tabia yake halisi,pole sana ndugu,yeye hana cha kupoteza,kama ni ndoa kashafunga,sherehe ikafana,na mapicha yakapigwa,anaendelea tu kufurahia maisha,na usikute pia hata ni yeye ndio aliekuwa anakulazimisha mbona mnachelewa kufunga ndoa.....
 
Mkuu mwanzo mwanzo pia alikua na huto tuvipengele? Maan hvo viumbe vinajisahau sana ..jaribu kuwa kam unampiga madongo ukiona hashtuki kiivo ujue ndo alivo alivo tu,kutokan labda na malezi aliyopewa.(chukulia kam mapungufu tu)

Na kuhusu kitandan atakua kakuzoea ,yaan anajua unapoanzia na unapomalizia (yale maajabu yamepungua pengine) so apo jiongeze ongeze mwenyew

Utan :sometimes kuna umuhimu wa kua na matawi pemben ili kufidia fidia magep yanayoachwa waz...
 
Amebadilika au yupo hivyo tangu mwanzo?
Kama amebadilika inawezekana mwili umechoka maana kukaa nyumbani na watoto wawili na huna msaidizi kama unatumia tu mikono unachoka sana. Mwambie yanayokukera na wewe msaidie hata vikazi kidogo.

Mwenyewe sina msaidizi hapa nashukuru day care na mzungu tu.
 
Hizi tabia za uvivu kama huyu mkeo nazionaga sana kwa wanawake Wanene.

Pia nakushauri mtafutie shughuli ya kufanya maana kukaa tu Nyumbani nako kunachosha. Mfungulie Genge, au Duka, Au Mtafutie kazi yoyote anayoimudu ili awe anajishugulisha hivyo hataboreka na kazi za Nyumbani. Utaona baadhi ya Kero nyingine zinapungua.

Kwenye Ndoa, kero kubwa zisizovumilika ni uchepukaji, hizi tabia kama za Mkeo zinavumilika zinaweza kuisha hata akipata Housegirl.

Kuhusu kunyimwa kugegeda napo ni jambo la kawaida kwenye Ndoa (wewe jaribu kula chakula cha aina moja mwezi mzima utaona kinavyochosha). Hicho kidude kinahitaji stim na hamasa kwanza.
 

1. Kuna watu ambao ni wavivu by nature. Yaani hata ufanye nini yeye ni mvivu tu na hawezi kubadilika.

2. Kuna watu ambao ni wachafu by nature/hawapo organized. Wewe huo unaoona kama uchafu au vitu unaona havijakaa vizuri yeye anaona mbona kila kitu kipo sawa?

3. Mtu anapokaa mazingira hayohayo miaka nenda rudi (mfano mama wa nyumbani) kuna vitu anavizoea anaona kawaida tu, japo wewe ukitoka ukirudi utaona tofauti.

4. Wanawake wengi wakishaolewa ni kama wanakua wamemaliza matamanio yao kimaisha. Yaani hana tena haja ya kuhangaika anaona ameshamaliza kila kitu.

Cha kufanya:

Kwa hapo mlipofika nadhani niungane na wanaoshauri uweke mfanyakazi wa ndani ambae wewe ndio uwe unamuelekeza cha kufanya. Kama ni usafi muelekeze wapi pa kusafisha, nguo zifuliwe lini, vitu vipangweje nk. Mfano akiwa anafua kidogokidogo kila siku baada ya mda mfupi utakuta hakuna nguo zimerundikana. Ikiwezekana muondoe huyo mwanamke hapo ndani ama kwa kumfungulia kabiashara au uende nae huko ofisini kwako yani asikae tu nyumbani.

Hilo la uvivu kitandani ndugu yangu bana we tafuta ka mchepuko tu usitake kujiumiza maisha ni hayahaya. Wamechepuka kina mfalme Daudi, Sulemani, kina Bill Clinton, Bill gates nk we ni nani? Tena unaweza kushangaa akijua una mchepuko ndio akazinduka usingizini ukajikuta umeua ndege mmoja kwa mawe mawili..!😉
 
Kama vile umokopy na kupaste kutoka kwangu, mimi kutokana na hayo uliyoyataja imebidi nianzishe mchakato wa kumfuatilia labda ana mchepuko. Kwakweli ndoa ni ngumu sana na wanawake ni rahisi sana kubadilika.
 
Ushauri wangu nikiwa kama mwanandoa ninayefurahia maisha: Hakuna kitu kizuri kama mawasiliano, hebu haya uliyotuambia hapa kamuambie yeye pia, ni suala la communication tu mkuu, usikae unajiumiza kumbe hujacommunicate naye ju ya yale unayopenda yawe, mbona rahisi sana kaka. Communication is key!!!
 
Kama vile umokopy na kupaste kutoka kwangu, mimi kutokana na hayo uliyoyataja imebidi nianzishe mchakato wa kumfuatilia labda ana mchepuko. Kwakweli ndoa ni ngumu sana na wanawake ni rahisi sana kubadilika.
Usimhisi vibaya, ni kawaida kuwa mchovu hasa kama ni mama wa kukaa tu home, mtafutie ishu awe busy nayo na pia ongea naye afanye yale unayohisi hayafanyi vyema, just communicate mkuu!!!
 
unyanyasaji tunaoupitia,Wanaumetutaingia mbinguni tukiwa hoi tumechoka na kuchakaa kabisa tukihema na ulimi nje kama jibwa la polisi naona malaika getini akitukokota kutushika mkono tukiwa na magoti yanayogongana
 
So far sijaona tatizo hapo naongea as a married man kwa muda wa kutosha tu kwenye ndoa!

Kuna issues ukizifuatilia sana zitakupa stress utashindwa kuielelea familia yako! Endelea na ratiba zako za kuwajengea future wanao. Hao ndio damu yako huyu mmekutana tu ukubwani.

Kukaa na watoto wawili kisha akupikie akuletee chakula mchana kazini hii ni BIG NO! Wewe kama uko serious basi Fanya mpango urudi home kula, that's simple! Ila dah kwa mwanaume halisi kurudi home kufuata msosi au kuletewa msosi kazini aagh hai-click kwangu.

Tatu, tendo la ndoa ni wewe na mpenzi wako, hapa atakayekushauri anakudanganya! Kila familia na kila MTU ana style yake na mwenza wake! Watoto wawili bila msaada na kazi za nyumbani na usiku unataka chakula on time na mkilala unataka AKUANZE huu ni UBISHOO na kujifanya wewe ni wa maana zaidi kuliko yeye!

NNE, unataka ukirudi aanze "kukutetemekea" jiulize, wewe Mara ngapi umerudi hata na chupi tu ya buku tatu pale mwenge ukampelekea? Au hata tango tu? Ukifika home anza kutengeneza furaha wewe mwenyewe. Sasa hutaki kutengeneza hio furaha na unataka wewe ndio utengenezewe furaha? Acha hizi

Sometimes tengeneza simple jokes, cheza na watoto, mtanie kidogo mkeo, piga nae story za kawaida, msifie kwa kazi za kutwa nzima hata kama you don't mean it.....inasaidia.

Mwisho, furaha yako au future ya wanao na ndoa yako iko mikononi mwako wewe mwenyewe!

Huyo Binti wa watu unamuoneleea tu, anza kubadilika wewe mwenyewe, kama hujatoka weeks msaidie kufua huku mnapiga story, msaidie kukàa na watoto wakati anafanya usafi. Sio ufanye home kwako kuwa gereza. Ni hayo tu
 
Mimi ni mke na mama wa watoto watatu. Nina miaka 11 katika ndoa na naomba nikushauri yafuatayo:
1. Mawasiliano kati yako wewe na yeye. Hizo kero za uchafu huenda katika mazingira aliyolelewa yeye wala hazimpi kero. Wewe ukiwa mume una nafasi ya kuzungumza nae na kumueleza unavyojisikia ukikuta manguo yamerundikana,vumbi kwenye fenicha nk. Unaweza kupanga nae ratiba ya kufua kila wiki labda Jumamosi. Tafuta namna ya kupush kwamba kila hiyo siku ikifika nguo zifuliwe.
2. Mambo ya kitandani pia ongea nae kiunaga ubaga vile unafeel. Na mweleze kushindwa kuonesha ushirikiano kunavyoenda kuathiri familia yenu. Mwelezee vishawishi unavyokabiliana navyo na jinsi unavyojiepusha kwasababu unampenda. Hivyo unahitaji abadilike
3. Someni Waefeso 5:33 na mlitafakari

All the best kaka!
 
Mkuu hebu orodhesha na mazuri aliyo nayo ili tubalance equation..
 
anakula bata sana, ataishi maisha marefu kuliko wewe, utakufa utamwacha, mwenzio anapumzisha akili na mwili havichoki wala kuzeeka na wewe unajichakaza. pole.

kosa kubwa ulilolifanya ni kumfanya awe mama wa nyumbani, tafuta hata mradi wowote asimamie, hajazaliwa kwa ajili ya ngono na kuzaa watoto kama ng'ombe, anatakiwa kufanya kazi ili hata leo ukidondoka asikimbilie kutafuta wanaume wengine wa kumlea kwa pupa, atakuja kupata limtu litaharibu hadi watoto wako, umeshindwa hata kumfungulia genge? mradi wowote hata wa kufuga kuku? mimi mke wangu ukimwambia awe mama wa nyumbani nahisi ndio utakuwa mwisho wa ndoa, manake anajishughulisha na huwa anapenda aweke kitu mezani. funguka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…