Mke wangu hatimizi majukumu yake ya nyumbani ipasavyo

Mke wangu hatimizi majukumu yake ya nyumbani ipasavyo

Ndug mleta mada ni kupe pole.
Mara nyingi changamoto za kwenye ndoa huwa hazikosekaniki, kama mwanaume unabidi uzikabili kwa sababu mwanaume ndie apaswae kuwajibika kuisimamisha ndoa na familia yake.
Mtu ambae mmekutana ukubwani maranyingi madhaifu huwa hayakosekaniki ndio maana kukawepo na kipengele cha kuvumiliana na kuchukuliana kwa upole na jitihada za kubalance hizo changamoto ziendane.
Nadhani ndio maana kuna neno kuoana, maana yake wewe unabeba yake na yeye anabeba yako.

Lakin pia jitihada za kuelimishana yale yalipungua sana yakae sawa na yale yaliozidi sana yawe sawa pia.

Kwa changamoto ulizozibaini kwa mwenzi wako unaweza kuzi badilisha kidogo kodogo mpaka pale yeye atakapoona kumbe nimepungua nijisahihishe ili kuendana na mwenzangu.
Hii unaweza kulifanya bila ya kutumia nguvu na bila ya shari pande zote.

Mwanadu akili yake imeindwa katika hali ya kujifunza daima, iwapo tu atapatikana mkufunzi mzuri.

Kwa hivyo kuwa mwalimu bora kwa mkeo, kule kuyabaini mapungufu yake ndio mwanzo wakujua namna ya kumbadilisha awe namna unavyotaka.

Unaweza kuanza kufanya wewe kile ambacho angepaswa afanye yeye, hali ukimueleleza kwamba hivi ndivyo ikupasavyo kufanya, nenda namna hio hatua kwa hatua, kwa upole na inyenyekevu , naamini kabisa atabadilika tu, lau asipobadika isikate tamaa bali iwe kama changoto ikupasayo kuenda nayo mpaka makusudio ya Mungu.

Nakutakieni yote mema.
 
Na ya kufuta vumbi tv ipo pia?vipi ya kitandani? na kupanga siting room pia,na kutandika bedroom? ushauri huu wa under age.

Ni hiv,angalia trend,je hii ni tabia yake toka unamuoa? au ameanza karibuni?kama ni tabia yake toka zamani kabla ya kupata watoto hao wawili basi hiyo haiwezi badilika. Ila kama ni tabia mpya itabadilika ukizungumza naye kwa respect.usimfanye yeye kushinda home ndiyo hana cha kufanya.anza kutambua mchango wake kwenye familia kwa kukufulia nguo hata hizo chache,kulea watoto wenu,kukupikia,hata kama mchana hakuletei chakula
Umenena vyema kama mtu ambaye upo matured. Sisi tuliooa tunajua. Wanawake wana changamoto zao nyingi, asiye na hili ana lile. Cha msingi tafuta mazuri yake na uyafurahie. Mapungufu tupa kule. Zaidi sana vumilia yanayovumilika, yapo mengine hayavumiliki
 
Kiongozi pole Sana! Kuna kitu kimoja sisi wanaume huwa tunaambiwa/kufundishwa au ni mapokeo kutoka kwa wazee wetu kuhusu maisha ya ndoa au jinsi ya kuishi na mwanamke kwenye ndoa. Tumeshazoea au zoezwa kuwa kazi zote za ndani ni za mwanamke! Mfano tunategemea mwanamke akufulie nguo, apasi nguo nk. Sawa lkn ushawahi fanya hizi kazi ukiwa gheto? Wakati wa u bachelor? Ni time consuming halafu haviishi unazunguka tu hapo hapo mwisho wa siku unajikuta umechoooka!
Naa

Asante na mimi umenifundisha kitu.
 
Mkeo atakua anazidiwa na majukumu ya nymbn...mm ni mfanyakazi na nna dd wa kaz lkn kaz za nymbn ni shughuli haswa kufua! Ila kwa upande wa mume huwa namhandle ipasavyo...ila pia kauvivu katakua kanamsumbua.
Watt wako wana umri gani?
 
Na ya kufuta vumbi tv ipo pia?vipi ya kitandani? na kupanga siting room pia,na kutandika bedroom? ushauri huu wa under age.

Ni hiv,angalia trend,je hii ni tabia yake toka unamuoa? au ameanza karibuni?kama ni tabia yake toka zamani kabla ya kupata watoto hao wawili basi hiyo haiwezi badilika. Ila kama ni tabia mpya itabadilika ukizungumza naye kwa respect.usimfanye yeye kushinda home ndiyo hana cha kufanya.anza
Asante mkuu. Nimekuelewa sana
 
Back
Top Bottom