Mke wangu kaamka alfajiri anaona anatoka maji maji ya njano tatizo ni nini?

Mke wangu kaamka alfajiri anaona anatoka maji maji ya njano tatizo ni nini?

🏥 Haende hospital akapime 🌡️🤒 ila kuna uwezekamo ni candida kwa kuwa gonorrhea au STI/STDs kwa wanawake huwa haionekani haraka tulitarajia wewe huoneshe dalili kabla yake.
🤒🚑 Ikiwa anahisi homa ni seriously haraka hospital.

🍞🍭🍻 Mwambie asitishe matumizi ya sukari kabisa ( soda, energy drinks, keki, pipi biscuits) kwanzia sasa, ulaji wa vyakula vyenye ngano ( mikate, mandazi, pombe n.k) na amira mara moja kwa kuwa huchangia uzaliswaji wa fungus kwa wingi. Msishiriki tendo bila kinga mpaka mtibiwe.

🥦🍉🥗 Ale vyakula vyenye virutubisho vyakutosha kama mbogamboga na matunda kwakuwa huboresha kinga ya mwili, pia muulize juu ya afya yake ya tumbo kama anashida eneo hilo kama tumbo kuja gesi, kuuma, kinyesi cha makamasi n.k
🤮 Kwa kuwa kama ni candida maeneo hayo ya tumbo pia huweza kuambatana. Ikiwa ndivyo nashauri pia atibu eneo hilo kwanza either dawa za mitishamba au hospitali choice is yours.

Nb: Ni vizuri pia hata wewe pia akaacha hivyo vyakula kwa kwa kuwa manii huweza kubebe pia hizo asidi.
🙏🙏📋
Dokta unatibu STI's na matunda??.
 
Candida inatoa weupe mzito kama maziwa ya mgando. Lakini gonorrhea inatoa uchafu wa njano au mweupe but maji maji mepesi sana. Wakati wa sex anapata maumivu sana. Dalili huwa zipo but huchelewa ukilinganisha na mwanaume. Mwanaume anapata dalili within 24 to 48 hrs. Wakati mwanamke anaweza chukua hata wiki 2 kupata dalili.
Mim mbona siumwi chochote nahapo kama siku tatu nyuma tulishiriki tendo
 
Okay.
Mara ya mwisho wewe kumkula ilikua lini?
Kama ulimkula ndani ya siku tano zilizopita hiyo sio gonorrhea. Labda Kama ulimkula kwa kondom.
Gonorrhea haliongopi kwa mwanamme ndani ya siku tatu habari utakua nayo.
Ila hii ya mke kulala na chupi wakati hayuko period sijaipenda.
Mara ya mwisho tumeshiriki siku tatu nyuma kabla hajaipata Hali hiyo
 

Mtumie hii link mkeo whatsapp
 
Dokta unatibu STI's na matunda??.
Kama hicho ndicho ulichoelewa? Kazi ipo.

Ikiwa umeenda hospital baada ya vipimo na kupewa dawa na dokta hasa lazima atagusa ulaji kwa kuwa dawa pekee hazina uwezo wakutibu bila mlo kamili. Hivyo dawa ya kwanza ni chakula na lifestyle hata kwa mgonjwa/muadhirika wa HIV.

Ingawa sicho nilicho maanisha kwenye statement yangu ya awali. 🙏
 
Wakuu habar mke wangu usiku wasaa kumi kaamka imemtokea Hali yakutoka maji maji ya njano hivi ukeni bila kujua anaona nguo ya ndani imelowa tu,hii itakua anashida Gani hasa

Dawa ya Uchafu Ukeni

Kwa kawaida mwanamke hutokwa na majimaji mepesi (vaginal fluids) yenye rangi nyeupe au ya njano.

Inapotokea anatokwa na majimaji yenye ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yanatoa harufu kali na muwasho, hiyo huwa ni ishara ya ugonjwa uitwao wa kutokwa uchafu ukeni ujulikanao kwa kitaalamu kama Vaginosis.

Mwanamke mwenye tatizo hili hujisikia vibaya na anaweza akaacha kushiriki tendo la ndoa ama kwa kuhofia maumivu au kwa kuona aibu kwani mwanaume ni vigumu kuvumilia harufu hiyo au hata kuuona tu huo ute ute kwani humjengea hisia kwamba mwenza wake atakuwa na magonjwa ya zinaa au si mwaminifu kwa ujumla.

Kinachosababisha kutokwa na uchafu ukeni:

Kuwa na wapenzi wengi
Baadhi ya dawa za uzazi wa mpango
Kusafisha uke kwa kutumia dawa zenye kemikali
Uchafu
Uvutaji sigara
Pombe
Maambukizi ya Bakteria au bakteria wabaya wanapozidi ukeni

Dalili

Kutokwa na uchafu usio wa kawaida
Kutokwa na uchafu wenye harufu kali kama shombo ya samaki au kitu kilichooza
Kuwashwa sehemu za siri na ndani ya uke
Uke unaweza kubadilika na kuwa na rangi nyekundu
Maumivu sehemu za siri wakati wa kukojoa
Maumivu makali chini ya kitovu
Kutokwa uchafu uliochanganyika na damu

Matibabu

Mara uonapo dalili hizo unashauriwa kwenda kumuona daktari haraka iwezekanavyo kwa vipimo zaidi na dawa zaweza kuwa ni za kunywa au za kupaka.
Mkuu nitafute kwa wakati wako ilinipate kumtibia mke wako apate kupona amradhi yake.

1758957774396.png
 
Back
Top Bottom