Una ushahidi wa hili?
Kwanini wawe wanawake wa JF na sio mahali pengine?
Ni kwanini umefikiria hili ni suala la wana wake na sio la kibinadamu?
Una matatizo wewe
KUtokuwepo mahali ambapo Mungu amesema kuwa mwanamke ni mtu haina maana kuwa mwanamke sio mtu
Usichanganye hayo mambo mawili
Lakini hiyo haimaanishi kuwa hakuna mahali ambapo Mungu amesema mwanamke ni mtu
Mwanzo 1:27 inasema
27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
Hapo Mungu anasema kuwa wote aliwaumba kwa mfano wake,kama mwanamke aliumbwa kwa mfano wa Mungu na mwanaume nae hivyo hivyo watakuwaje na tofauti za hovyo unazotaka kuzileta?
Pia tazama mstari huu
Mwanzo 2:18
18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana
Mungu anasema hapo kuwa anamfanyizia Adam msaidizi wa kufanana nae
Unajua maana ya kufanana wewe?
Anaetafuta sifa ni nani sasa?
KUFANANA NA SIO KUWA wewe ndo ukae kimya cc
Eiyer