magnus msambila
Member
- May 7, 2017
- 31
- 12
Mwambie hapo nyumbani watu hawatakiwi kukaa zaidi ya siku kadha ulizia shughuli zake zitachukua muda gani. Amefikia kuondoka na familia yako kwenye bichi, chunga atachukua mkeo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapo ndo shida sasa. Hata maelezo yake yanaonyesha ni boya, mwanaume mwenzio anatembea ni kichupi mbele ya mkeo kisha unanyamaza kimya unakuja kulia huku JF.Ukiwa boya nani atajali kuwa wewe ndo mwenye nyumba. Hata mkeo atakupuuza tu na atatoka na hilo jitu.
Mwanaume mashine.Waheshimiwa nina mgeni ambae sasa anaelekea kumaliza wiki akiwa hapa kwangu, ni binamu yangu huwa anaishi mkoani amekuja kwa shughuli zake binafsi, ataondoka atapokamilisha yaliyomleta.
Nimewaandikia kwa sababu, huyu jamaa amenishangaza sana, imagine weekend hii iliyokwisha anashinda na boxer kutwa nzima tena kifua wazi, au kwasababu amevimba kifua anataka tumwone au?
Mke wangu na house girl wanafua nguo Jumamosi asubuhi eti anaenda pale awasaidie kufua, natoka ndani namuuliza wife mbona mgeni anafua nguo, najibiwa kuwa eti ameomba mwenyewe, hii ni sawa kweli?
Yote tisa, kumi ni Jana, inafikia hatua linamkuta wife jikoni anasonga ugali linaomba limsaidie kusonga ugali, mgeni gani wa namna hii?
Wadau nitumie njia gani kulitimua hili jitu hapo nyumbani? Kabla halijaleta madhara maana mdogo wa mke wangu naona kama yuko nalo karibu sana, pia wife kaniuliza kama mimi pia naweza kufanya mazoezi nikawa kama hilo jitu badala ya kitambi, ingawa alinieleza kwa utani huku tukifurahi na kutaniana ila najiuliza kwanini aseme sasa wakati hili jitu lipo?
Linakaa hapo sebuleni kwenye video hadi usiku mwingi likiwa na mdogo wa mke wangu bila kujali maadili.
Jumapili nilienda kwenye Bonanza la timu yetu ya veterans narudi nimekuta nyumba nzima hawapo wameenda beach wote pamoja na huyu jamaa.
Hivi unaendaje ugenini halafu unaanza kuleta ujuaji wa namna hii?
Wadau msaada wa mawazo unatakiwa haraka.
Dada upoNgoja nicheke kwanza.
HahahaNgoja nicheke kwanza.