Mke wangu kanificha mengi, naomba ushauri

mchane ukweli halafu mwambie alichofanya ni ujinga na uzembe hayo mambo aliyoficha yapo toka zamani alivyokufikilia sivyo kwahiyo mwambie umemsamehe na umsamehe kweli mapungufu kama haya ndio huwa ya kujengea ndoa na sio kubomolea ndoa

Simama kama mwanaume mpe mwelekeo asilete mbwembwe na ujuaji halafu na umkanye haswa zen maisha yaendelee.
 
Suala la ushirikiano sio kweli nampa ushirikiano nimesomesha mdogo wake nimemfungulia biashara japo alishindwa kuindesha ikafungwa Baba ake akiniomba msaada na mtumia japo yeye alinikataza kwa sababu ya migogoro ya familia na mama, mimi nimtu peace sana katika ushirikiano wa maendeleo nda udhaifu wangu huo.
 
Boss,

Kwanza kabisa hakikisha unamtumia nauli anakuja home.

Akifika home wewe mkaushie usimsemeshe kitu chochote kile zaidi ya kumpa hela ya matumizi tu, najua atataka suluhu tu, sasa wewe mwambie akueleze kuanzia mwanzo hadi mwisho hapo unampima atakudanganya au LA

Kisha mrudishe kwao mwezi 1 akajifunze
 
Ilikuwa ni mwaka gani hilo tukio. Ukimwi sio ugonjwa kwa maana kamili ya kitabibu ila ni upungufu wa kinga mwilini. Mama mkwe alijisahau nini kuchukua tahadhari asife kwa fedheha maana naona kifo huwezi kukikwepa ila unaweza jieupusha na kufa kifo cha aibu kama icho. Maana MARADHI aliyokufa nao mama ni ule ukimwi wa miaka ya 80 sasa ivi ukishajitambua umeathirika ukafata masharti huwezi kufa kifo kama icho cha fedheha madonda kudhohofu naona hilo ndo walikuwa wanalificha. Samehe ishi na mkeo. Alichokuwa kuwa anafanya wyf wako na ndugu ni kuficha aibu ya mama yao
 
Mtumie nauli arudi mkae kitako muyamalize kama wana_ndoa, Mweleze kwa kina kuwa hukupendezwa na tabia yake ya kukuficha mambo kama hayo

Mwisho kabisa,... Legeza moyo msamehe mkeo, yeye pia ni mwanadamu kukosea kupo.
 
Reactions: HLM
Ulitaka kulenga nini hapa mkuu.?
Manake umeniacha na mimi njia panda.
 
Mkuu ni sawa hilo unalo sema, kilicho sababisha ungonjwa umdhohofishe haraka nikuuficha sanaa, mimi sikatae kuficha aibu ya mama yao, lakini mimi nilikua sehemu ya familia yao, pili kama wasingetaka mimi nijue wasinge mleta kwangu, kwasababu alikua na watoto wengine wakubwa kuzidi mke wangu, kwanini mimi nitoe hera ya usafiri ya chakula Malazi arafu nifichwe?
 
Hilo nikweli kabisa ni msiri sana na hofia huku mbeleni itakuaje?, nikiacha hili lipitehivi hivi, sasa hivi ananihitaji kwasababu ya msada wangu kwake, je kesho nikiwa sina uwezo huo wakumsaidia kweli atanivumilia?
Sidhani Kama ina tatizo saana, mtu kuwa msiri kwa mambo ya nyumbani kwao, na Mara nyingi hi husababishwa na upande wa pili, maana kwa kawaida binadamu tuna tabia ya kufunguka kwa watu ambao tumesoma attitude zao na kijihakikishia usalama.
Sasa kwa mfano Kama mtu amekusoma kukuona una dharau, majivuno, nk, anafunguka vipi kwako mambo mazito ya nyumbani kwao..
Hata hivo pamoja na kukuficha mwisho wa siku umefahamu Kila kitu, hi Ina muanika yeye kwamba hata Kama amekuficha, Kuna mambo hayafichiki na ukiyaficha mwisho wake Ni kuumbuka tu kama mtu anayejaribu kuficha Moto.
Hivyo ushauri, cha kwanza jitathmini hasa approach zako unazotoa dhidi yake au familia yake uone Kama Zina ukakasi wowote katika hisia za binadamu na uziboreshe,
Pili. Kama alivyosema mchangiaji mmoja, muweke wazi kwamba umejua Kila kitu ili ajue kwamba Ni ujinga tu kuficha mambo ambayo yanaweza kujitokeza yenyewe,
Tatu, mueleze faida za uwazi na hasara za usiri..
 
Ni mkeo na mna watoto wawili. Muulize sababu ya kukuficha kuugua kwa mkweo na pia kuficha kuhusu kifo chake, labda anaweza kuwa na maelezo ya kukuridhisha vinginevyo ni wa kuwa naye makini sana huyo kwani ana tabia ya uongo ya kuficha mambo yenye umuhimu mkubwa. Pia anatakiwa kujutia alichokifanya hivyo akuombe samahani.
 
Mkuu hiyo ni changamoto ndogo sana!imagine siku ukijua hao unaowaita wanao sio wanao wa damu si utajiua sasa!tuishi nao kwa akili mke sio kiumbe wa kushirikiana siri zako maana hizo ndio zitageuka kuwa silaha siku za baadae
 
Mi ningeomba kukuuliza swali. Je huu ni mke wako wa ndoa? Au ni mwanamke uliemzalisha kisha mmeamua kuenshi pamoja
 
Mambo mengine kuyawka rohoni utakuja it's kabla ya siku zako
Msamehe tu be a man!
 
Ahsante kwa ushauri mzuri, mimi sikutaka kujua ya kwao na sijawahi kumuuliza, ila suala la mama kuumwa paka kufa bila kuniambia ili niuma sana, kwasabb yule mama alikua nguzo kubwa kwenye familia yangu na yakwao huenda kunamambo ningemuuliza kabla ya kukata roho.
 
Samehe saba mara sabini alificha aibu ya mama yake na familia yake! Mimi nadhani alikuheshimu! Potezea mzee baba! Kwenye ndoa mambo
Mengi yanatokea hilo
Mbona dogo! Mie mke wangu kununua nyumba bila Mie kujua na tuna nyumba tatu! Na nimesamehe aliniambia kitendo kimeshatokea! Kuuliza why akasema “surprise”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…