Mke wangu kanificha mengi, naomba ushauri

Aisee!
 

Hili swali kaa ujiulize kwa nini ufichwe? Lazima kuna sababu na hiyo sababj mkeo anaijua. Ameshakusoma anakujua vizuri. Ndio maana kaamua ku mute. Inawezekana kuna neno moja tu ulimtaka kuhusu familia yake likamuumiza basi ni hilo ndio limenfanya awe msiri, kwa mwanamke hata kama utatoa mamilioni hata kama utamlisha mpk avimbiwe lakini kauli moja tu itamfanya asahau mema yote.
Kama unatoa hela na hata huchukui muda hata siku moja kumsindikiza kuona mama hospital tayari anajua huyu hmm.
Uko na binti atakua utaona atakavyokuwa anajali sana familia yake.
Kuishi na mwanamke inahitaji akili nyingi kutuelewa.
 
Ni mke wa ndoa kamili mkuu
Kama ni mke wa ndoa. Baci nakusihi usiendelee kumlaumu mke wako. Kwa mila na tamaduni za mswahili hilo tatizo ulitakiwa kuchirikichwa na wakwezako . Mke wako amedhibitiwa na ndugu zake au mama ake amewalazimisha watoto wafanye siri
 
Mkuu unmuuliza wa kazi gani na mtumie nauli aende mpe pole mambo yaendelee mkuu
 
Mke anaona aibu kwa yaliyomsibu mama yao.
 
Pole, mwambie kabla hujamtumia nauli aseme ukweli wote asikufiche na umwambie umejua mengi kupitia majirani zao

Akishaweka ukweli wote

Mwambie nakupa rikizo ya kujifunza kuwa muwazi.
Sidhani kama utaitaji ushauri mwingine tofauti na huu sidhani kwakweli
 
Mkuu hili jambo hata mimi liliwahi kunikuta lkn ni tofauti kidogo na la kwako....zaidi ni uwongo kwa mkewangu nilivumilia kwa muda mrefu na mwisho hivi karibuni niliitisha kikao cha dharula na washenga pamoja na baadhi ya ndugu zake na ktk hicho kikao msimamo wangu ulikuwa ni kuhitisha mahusiano yetu ndani ya ndoa kwakuwa sikuona haja tena ya kuendelea kuwa na huyu mwanamke hali ya kuwa ni muongo muongo sana na nikaeleza mambo yote niliyokuwa nikiyajua

Basi ndipo nikapata wasaa mzuri wa kuujua ukweli baada ya rafiki yake wa karibu kutuelezea baadhi ya mambo aliyokuwa anayajua na mengine aliyokuwa hayajui kikao kiliendeshwa kwa muda mrefu na mwisho wa siku yeye mwenyewe alikili makosa na alijutia sana na kuomba msamaha sana,nilikuja kuukibali msamaha wake baada ya wamama watuwazima kunipigia magoti tena mpk machozi kuumuombea msamaha ndipo nikakubali sasa hivi heshima ipo mpk inamwagika[emoji38]
 
Covax Kwa umri wake Mkeo kubadilika si rahisi labda AOKOKE..

Ushauri Wangu Kwako ni huu muite yeye na Nduguze wote walokuwa wakifanyia vikao hapo Kwako na umuulize mbele yao Kwanini alifanya alivyofanya ili kuweka defensive mechanism kwa Siku zijazo!

Hofu yangu kama ameweza kukuficha kifo cha Mamake mzazi je, unadhani atakuwa na hofu gani nyingine hapa duniani?

TAFAKARI NA CHUKUA HATUA !!
 
Kimsingi alikudharau na kukuona boya (samahani kwa kutumia neno hili) akadhani huwezi kujua Nini kinaendelea...
 
Kuna wanawake vichwa maji kweli, kuna vitu vya kuficha ila sio kwa situation yenu hii, anyways huwa siikubali dini ya kiislam ila pona ya mwanaume Ni kuoa/kuzaa na mke zaidi ya mmoja mmoja akikosa akili na kukufariji mwingine atakuwa na akili na utapata faraja ya maisha,,

Mkeo ni mjinga tu, anajichetua kukuficha lakini mama yake alimfikishia hapo kwako na huduma inakutegemea wewe, kufikia kuugua bado anaficha Hadi msiba,, akili za wanawke wengine bhana dah sijui mnawaokoteaga wapi
 
Hadi leo hajaona kama kuna kosa kafanya, anaomba kwa haki zote nimtumie nauli tena ya ndege eti kwasababu anasafiri na mwanangu mdogo wa mwaka moja na nusu.
 
Mkuu hilo sio kosa msamehe na mtumie nauli sio ya ndege bali ya basi
kuna wengine wanaleta magonjwa ndani km UKIMWI kwa kutembea na vidume huko nje, sasa huyo kamleta mama yake , na ni makosa ya mama alikoupata atajijua mwenyewe baada ya kupokea pensheni
 
Fanya hivi hukuoa mama mkwe tuma nauli arudi watoto wamuone mama yao
 
Huyo ni mkeo hamna namna zambi tunayochukia wanaume ni ya usaliti hayo mengine mnakaa na kuambiana ukweli kwamba hujapenda na siku zote ajifunze kuwa muwazi.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Hakutaka ujue ugonjwa wa mama yake ndio maana alikuficha msiba.

Nadhani huo ugonjwa wa mama yake aliuchukulia vibaya akahisi nawe pia utamjudge mzazi wake.Muache aje muyazungumze punguza hasira.
Ushauri bora kabisa huu, mleta uzi chukua huu ushauri.
 
well said....busara itumike japo kuna kosa la kusudia,na kosa la kimantiki,na kosa la bahati mbaya....yote yanawezwa fanya na binadamu walio tumamu
 
Yaani wife wako kakaa msibani mpaka siku 40 zimeisha?
Hana kazi!?
Hana biashara za kusaidia kusukuma maisha?
Hajali familia yake!?

By the way, msamehe tu mkuu.
Kuna wakati akili huwa inachanganyikiwa.
Na Mambo yanakuwa magumu.
Kuuguliwa sio mchezo hasa pale unapojua mgonjwa Ana ugonjwa mgumu usiokuwa na matumaini ya kupona.
Alichokosea ni kutosema tu mwanzoni kuwa mama anaumwa amekuja kujiuguza!!
Lakini hata Kama walikuwa wanajadili Mambo yao wewe yasingekuhusu mpaka yawe yanaingilia na familia yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…