Mke wangu kanificha mengi, naomba ushauri

Yupo hawakua na maelewano kama miaka mitano nyuma japo walikua wanaishi nyumba moja na hilo nililijua siku ya mazishi kwa wachimba kaburi
Sawa, hivyo kuna tatizo tu.

Mama awezaje nunua nyumba kimya kimya na vikao wanaweka humo ndani mwako.

Ni mkeo hamna namna yamalize kiume hivyo hivyo.
 
Sijui kwanini nimetamani kujua umri wa mama mkwe na mwanae...ili nijue mkeo nae kazaliwa nao au laa
Hilo la kuzaliwa nao ondoa shaka hana na watoto wetu hawana, dont be obsessed na ugonjwa hiyo sio issue, issue ni tabia zake za usiri kwa mume anae muwezesha kwa kila jambo liliopo ndani ya uwezo wake.
 
Sawa, hivyo kuna tatizo tu.

Mama awezaje nunua nyumba kimya kimya na vikao wanaweka humo ndani mwako.

Ni mkeo hamna namna yamalize kiume hivyo hivyo.
Ndo nimekuja humu kupata 'soft landing' nisije kutatua kumbe najiongezea matatizo mengi, kusema ukweli huyu mama tabia yake ya uongo inanikera kwelikweli
 
boss ugonjwa n siri ya mtu mwnyewe .tena kama AiDs ukifa na hiyo kitu n fedheaha huenda mkeo alihofia aibu ya mama yake kufa kwa gonjwa hilo ila cha kuzingatia wewe na mkeo kama mahusiano yenu yako vzr no need tumia hela wife aje mlee wa watt cjaona changamoto sema tyu usiri haufai katika maisha ya ndoa baina ya nyie wawili muweke chini umueleza ukweli umeshaujua mpe mifano ya hasara kuwa na siri ndani ya nymb hususani vinavyohusu familia
 
Kwa jinsi navyowapenda wanangu kwakwel huyu mwanamke angenipa tabu sana kifikra maana nisingemuan hata kwenye malez yao ataniharibia madogo kwa kuwarithisha upumbavu huo
 
Hakutaka ujue ugonjwa wa mama yake ndio maana alikuficha msiba.

Nadhani huo ugonjwa wa mama yake aliuchukulia vibaya akahisi nawe pia utamjudge mzazi wake.Muache aje muyazungumze punguza hasira.
Hapana maelewano na mwanamke muongo, Uongo huwa ni tabia sio bahati mbaya
 
Mkuu kama ni mimi siwezi kuendelea kukaa na mwanamke ambaye ni muongo wa kiwango hicho. Ikiwa hilo kakuficha just imagine mangapi anakuficha.
 
Ukiskia wanaume wana gubu basi haya ndio mazingira yenyewe yanayosababisha.
 
Sio kweli mie niko simple sana wala sinaga makuu ila nachukia uongo kwasababu nimelelewa kwenye misingi ya dini
Mkuu katika maisha ya ndoa ukiwa simple kwa kumaanisha mwenzio lazima awe huru kukwambia chochote kile.
Hiyo ya kulelewa kwenye misingi ya dini ni moja ya tatizo pia inawezekana unalitumia Kama fimbo kwake na yeye in response anaamua kutokwambia kila kitu kwa sababu anaona atakukwaza au utamdharau
Trust me hata huo msiba usingekuwa sharp ungekuta washazika, and she would have been very comfortable with it.
 

Mke anakuwa msiri na mwongo Kama:

1. Wewe si mweIewa.
2. BahiIi
3. UnafuatiIiya vitu boya kijinga!

Si sifa mtu kufa kwa ukimwi! Kama umemchoka we mwache mie nitaishi naye, share contact!

Wanawake wametutesa mno, huu udhaifu wa kawaida hivi unaahindwa vumiIia and you have two children!?

If people want they privacy you give them, Kama hakukutaka kwenye msiba (nahisi wanakujua u mshamba) kwa nini u force?
 
hii inaukweli ndani yake japo pumba
 
Hapana maelewano na mwanamke muongo, Uongo huwa ni tabia sio bahati mbaya
Uongo ni tabia lakini pia una sababu zake . Mara nyingi husababishwa na hofu.
Ukishajiweka katika mazingira ya kuogopwa na jamii lazima uzalishe watu waongo
 
Mkuu kama ni mimi siwezi kuendelea kukaa na mwanamke ambaye ni muongo wa kiwango hicho. Ikiwa hilo kakuficha just imagine mangapi anakuficha.
Tena sio hilo tu huyu mke wangu ni muongo kiwango cha sgr..

kuna siku nilisafiri kuenda mkoani kwenye kazi zangu, nilivo toka tu nayeye kaondoka kwenda kwa Kaka yeke hapa jijini, majirani ndo walinishitua kwamba sasa wiki mbili taa za nje haziwashwi shemeji inaonekana hayupo ila hajatuaga,...mmh

nikampigia simu mbona haupo nyumbani? Kanijibu eti kaondoka jana kwa Kaka ake eti kuna mgonjwa!!!

Nikawapigia jirani kwakikisha wakaniambia nilivyo ondoka kesho yake nae katoka karibu wiki mbili na nusu.......kweli huyu ndo mke wa kuishi nae nakujenga maisha ya badaye?
Nb
Ila sijawahi kupata vyashiria vyovyote kama huenda inachochora na wanaumme simu yake naikagua mwanzo mwisho hamna kitu hicho, ila uongo wake
 
Uwongo ni tabia mkuu, unakuemo ndani ya damu.
Mimi nimepitia sana kwenye mazingira hayo, Na jambo la mwanzo mwanamke hunishanda kwa tabia ya kuwa muongo. Tena huwa wanadanganya kwa mambo mengine hayana hata msingi kabisa.

Asilimia kubwa ya wanawake wa TZ ni waongo kiwango cha SGR. SIo poa kabisa hawa viumbe.
 
Uongo ni tabia lakini pia una sababu zake . Mara nyingi husababishwa na hofu.
Ukishajiweka katika mazingira ya kuogopwa na jamii lazima uzalishe watu waongo

MKuu wanawake waache tu, mimi nina kitabu kizima kinachonihusu mimi binafsi. Wanawake wa TZ uongo ndio sifa yao kuu vyengine vinafuata.
 
Tizama kama tofauti na hilo kuna mengine ambayo unaona hayako sawa katika ndoa yenu.. Kama yote yako vizuri basi tambua tu huu ugonjwa bado huwa kuna stigmatization kubwa sana katika jamii. Na wengi hatupendi kuweka wazi kwamba wapendwa wetu wamekumbana na hiyo changamoto. Pia kwa kulinda heshima ya mama yake aliona si vyema kuweka wazi kwako bila idhini ya mgonjwa mwenyewe. Ila shida niliyoiona ni kutokukupa taarifa za msiba mapema..
 
Wanawake wengine ni pasua kichwa...

Kuna mwana mkewe wa ndoa kabisa hakumwambia kuwa ana mtoto aliyezaa kabla ya ndoa.

Mtoto huyu alizaliwa miaka mitatu nyuma kabla ya kuona na huyu mjewe.

Na mume kagundua miaka sita mbele. Wakati mtoto wa mke ana miaka 9.

Alijuaje?
Aliona mawasiliano ya simu yasiyoeleweka. Akaamua kutap mawasiliano. Ndio kwa umafia mkubwa akakutana na hayo.


All in all....kama hakuna usaliti, na bado una amani kuishi naye katika maeneo mengine yote, mvumilie tu.
 
Tatizo la mkewangu ni kutokua muwazi angeniambia mama anaumwa umekija kuugulia hapa kwa mda, hata angesema ana kisukali au pressure nisingekazana kuthibitisha hilo, kinacho niuma ni kua na mgonjwa maututi kwa mwezi mitatu ndani mwangu bila kunishirikisha kwani haniamini kwanini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…