Mke wangu kanificha mengi, naomba ushauri

La kua na mtoto kabla ya ndoa na kutomsema, angalau kdgo angalau, nasisi wanaumme tunaficha watoto wetu wa nje ya ndoa, ila kuficha msiba wa mama mzazi kwa mme wako inauma sana
 
Hivi wewe huyo mama hukuona kama anaumwaa...?? Miezi mitatu unaishi naee ulitaka mkeo aanze kukwambia nini akati ameshachanganyikiwa mtoto wa watu mama yake anaumwa na anajua ana hali mbaya.

Sema unataka kumtafutia sababu tu mzee ila huyu mwanamke hana kosa kabisa. Labda kuchelewa kukupa taarifa kuhusiana na kifo cha mama yake hapo kidogo alikosea.

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
Paka sasa hivi hajamueleza chochote wala kukiri kosa....huyu sio mke wakujenga nae maisha
 
Mkuu hata usihofu huyu mke wako ni wale wanawake baadhi ambao hawana elimu ya VVU thus hata yeye alikuwa anamnyanyapaa mama ake na ndo maana hajakwambia ,msamehe kisha mwelimishe songa mbele ila chukua tahafhari.
 
fact
 
Umtumie nauli kwani hafanyi kazi?
 
We jamaa unaonekana ni sample flani za watu ambao wanapenda kutukuzwa n kunyenyekewa sana,kwa kutoa vijihela vyako ulitaka ww ndo uwe mfalme sasa wa kuambiwa kila kitu cha familia nyingine?acha utoto ngoma sio kitu cha mchezo we bora ushajua chanzo cha kifo piga kimy maisha yaendelee,afu unaonekan huna utu kabisa maana unasema unaona kinyaa kulala na mtu muongo je ungeambiwa mama mkwe anangoma na yupo kwako si ungemyanyapaa sana? Jiangalie tabia zako kwanza kabl y kumjudg mke
 
Mke wangu asiniambie mama yake kafa halafu niende? Kufanya nini?

Halafu ninune nisimtumie nauli? Nigundue nini?

Mimi namtumia na bila kinyongo kwani mama yangu yule mpaka iniume?
 
Mkuu mchukue wife muende kituo cha afya mkaangalie status zenu, utakuwa umefichwa mengi
 
msamehe tu ila muonye asirudie kukuficha ficha chochote kile kinachokuhusu directly ama indirectly
 
Fukuza huyo duuuuh huyo hakupendi anakutumia tu
 
Kwahili hana sifa za kuwa Mke...
Japo wengi humu wanashauri umrudishe kisa tu watoto lakini binafsi naona Mkeo hana sifa za Mke.

Yaonekana majirani Wana mengi Sana wayajuayo kwa Mkeo na wameshachoka na tabia zake hadi wameanza "kufunguka".....iko Siku utakachosikia kinaweza kukuua kwa presha. Be careful !

Waweza kagua simu Siku zote na kamwe usione chochote cha kukutia hofu kumbuka wako wazinzi wabobevu hawakamatiki kamwe toka ujanani hadi uzeeni.
 
Nimekuelewa saba ambapo hukuuliza "nani kafariki" ili huyo mtu asijue kuna siri kati yako na mkeo..akili ya fasta hivi wengine hatuna.
 
Uchambuzi mzuri sana mkuu, unajua watu wengi humu wanaona uongo sio issue, nijambo la kawaida wakati uongo huzaa madhambi yote kwenye mahusiano.
 
Mwanamke muongo hanogi hata kwa mbali aisee.Yaani mimi kunidanganya ni tiketi ya kuachana kabisa
Ukipuuza uongo huu kuna kubwa zaidi atakudanganya utalia maisha yako yote.
Zungumza nae kwa uwaz kabisa ujue why alificha taarifa za msingi kama hizo then akili kumkichwa
 
Nitumie namba yake ya simu nimwulize halafu ntakwambia ukweli wote
 
Mtumie nauli mkeo aje nyumbani,akifika nyumbani kaa naye chini zungumza naye kwa upole akueleze nini sababu ya kukuficha habari ambazo tayari unazijua,kisha mpe pole na umsihi ajaribu kuwa muwazi,
Kumbuka mkeo amepoteza mama na wewe ndiyo faraja yake.
 
Kwa sisi ambao tushadanganywa mauongo makubwa makubwa sioni kama mkeo anatatizo hapo. Mtumie nauli arudi bana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…