Mke wangu kanipa wakati mgumu

It's not winning battles that makes you happy, but it's how many times you turned away and chose to look into a better direction!
 
Mzee mwenzangu nakushauri achana na hayo mambo kuyafuatilia......

Mungu amekupa bonus ya kuishi miaka yote hiyo ya kwenye ndoa lakini naona unatafuta mwenyewe kiranga cha kutangulia.........

Nikuambie tu mzee mwenzangu amani ni bora kuliko vita.....kukaa kimya sio ujinga.......funika kombe mwanaharamu apite.....

Hicho unachokazania kukifanya ndio itakuwa mwanzo wa safari yako ya kutangulia mbele za haki......na utakufa mdomo wazi huku mwili umekakamaa.......utakufa huku unasimangwa sana......

Nakusihi sana acha mara moja...... uchunguzi utakaouanza utazalisha uchunguzi mwingine na mwingine.....na kibaya zaidi majibu yote ya humo hayata kufurahisha bali yatakusogeza kaburini zaidi.......

Dah!!
Nakuhurumia sana mzee mwenzangu maana unajitafutia mwenyewe janga.....

Naomba nikukumbushe kuwa wanawake hawakui bali ni miili tu inachoka na moyo hauzeeki........

Lakini pia nakukumbusha kuwa mwanadamu anapenda sana faragha na kawaida hakuna anayependa kuingiliwa faragha zake....iwe mke/mume au hata mwanao.....na siku akigundua kuwa unamchunguza basi jua umeondoa kiasi kikubwa cha upendo baina yenu.......

Usipende kukaa kaa na mkeo nyumbani muda wote........nenda hata kwenye vijiwe vya kahawa au hata kacheze bao muda mwingi.....mwache mkeo apumue.....

Karibu tupate gahawa Mzee mwenzangu.....
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] weee.!! Kumbe??
Pole bff wangu chana nao watajijuuuuu
Tangu mwanzo wa uzi huu nilitia shaka uhalali wa kisa chako. Lkn huu mwendelezo wa tamthiliya hii umehitimisha nadharia yangu, kwamba hiki ni kisa cha kutunga maana hakuna 'touch' za mtu mzima katika usilimuliaji wako. Kwa kifupi hii ni chai.
 
Ajsante sana KIKULACHO kwa maoni na ushauri wa hekima namna hii, niliamua kumchunguza baada ya kuona kuna mabadiliko ya tabia na dharau fulani hivi,

Unaweza kumuuliza kitu akakupita hivi hivi mpaka umfate alipo na kumuuliza tena,

Kwa miaka yote tuliyoishi sikuwahi kujipa pleassure ya kumfuatilia,

Kwa kuhusu suala la shughuli , tayali ninayo na kipato scha kuweka mafuta kwenye gari sio haba, namshukuru Mungu kwa hilo.
Ahsante sana kwa mchango wa busara,

Maadam nimeshailewa tabia yake hatanipa shida
 
Kuhusu kuacha uchunguzi upo sawa ndio maana niliacha kuendelea ili nisije nikakumbana na mengi zaidi mabaya yakaniumiza na nikabomoa mji. Kama ana akili ataacha
 
Isije ikawa ni sonona ya kukosa hela ndiyo unaanza kumsingizia mkeo. Maana kukosa kazi miska 2 kwa mwanamume siyo jambo dogo.
Pesa ya kunilinda ninayo, na shughuli yangu inaniingizia kipato si haba,

Hivi mtu huna kipato na umajili vijana 5, utasema huna kipato,
Nasimamia shughuli zangu toka saa nne asubuhi mpaka saa mbili usiku utasema sina shughuli kweli,

Naona nipo vizuri zaidi kuliko hata nilivyokuwa kazini,

Naamka saa saa 11 asubuhi mke akienda kwenye shughuli zake mimi natembea km 10 kwenda na kurudi,

Narudi nakunywa chai naenda kusimamia shughuli zangu , mchana narudi napikiwa na msichana , nalala kidogo saa 11 naenda kusimamia mambo yangu mpaka usiku,

Kwa hiyo nipo vizuri,

Namshukuru Mungu
 
Mzee mwenzangu hakuna jambo gumu kama kuishi na kiumbe mwenye utashi na nafsi huru............

Kwenye safari ya maisha ya wawili hasa wanaolala kitanda kimoja wakiwa watupu kuna mambo mengi sana..........na ili muendelee kuwa wamoja unalazimika kuyapuuza mengi kati ya hayo.......

Mambo ambayo yanatuwahisha kaburini Wanaume ni umwamba, ushujaa na kutokubali kushindwa.......

Mimi nimeamua kuuvaa upofu angali naona ili kuhifadhi chem chem ya furaha moyoni mwangu........

Yanini ujiwahishe kufa kwa vitu ambavyo unaweza vipuuzia na hali ya kuwa mwisho wa siku utakufa......??

Miaka uliyoishi kwenye ndoa inakutosha kabisa kupiga moyo konde na kuendelea na maisha yenye furaha na amani moyoni............


Uwe na wakati mwema Mzee mwenzangu........
 
Katikati ya mahojiano hayo na bado nikiwa na hasira, akatoa wazo la tumpigie simu bwana Musa,
Nikamwambia usiku wote huu yeye hana mke , na unataka kumuuliza nini, akajibu si ni haya unayoniuliza,

Nikashangaa, yaani yupo na mke wake halafu akujibu wewe? Inawezekana kweli,

Akashauri tumpigie simu kesho .mimi nikakaa kimya natafakari baadaye nikamwambia afute namba yake , akahangaika kila akifuta inatokea, anipa simu nikaifuta, lakini mimi ninayo,

Nikaendelea kumhoji, mara ya mwisho umeonana naye lini, akasema ni muda meingi sasa , mimi huwa nampigia simu tu ili aniunganishe na watu wake nikiwa na shida.

Nikamuuliza aniambie wajihi wa huyo mtu, maana mimi hata sura yake siikumbuki( kumbuka ni mtu ambaye sikuwa na mazoea naye kabisa na simkumbuki , hata jina sikuwahi kumjua),

Akaniambia hajamwona siku nyingi kwa hiyo hawezi kukumbuka lakini sio mrefu wala mfupi,
Anadhani sio mnene kama mnene,

Nikamuuliza ni Mkristo au Muislam, akasema hafahamu,
Nikamuuliza tena ni kabila gani , napo hajui, nakashangaa sana , hapo akazidisha hasira zangu, yaani unaweza kuwasiliana na mtu , miaka yote mpaka kuandikuana msg kama hizo humwelewi hata kabila lake,
Akanijibu kwa jinsi anavyomuona ni mtu wa (anataja maeneo fulani)

Namuuliza hapa Dar anaishi wapi , anasema hafahamu,

Hapa ndio nishikwa na ghadhabu zaidi kwa kutukana na yeye analia,
Namwambia kwa jinsi ya maelezo yako huyu anaonekana ni mdogo kweko , unawezaje kulala na kijana mdogo kama huyo,? Anaingilia kati kwa kukataa hajawahi kulala naye huku analia ,

Namuuliza, aliwahi kukutongoza , anakataa, kwa hiyo wewe ndio unamtongoza maana wewe ndio unamuulizia kila wakati!!

Napo anakataa,
Namuuliza , hiki kutupa jongoi na mti wake maana yake nini?

Itaendelea
 
Nashukuru sana
 
Ila we Faza una fiksi sana..
Hapa mkeo alisema huna kazi.
Mke—- yupo tu aliacha na kazi sasa hivi yupo tu nyumbani.,
 
Ila we Faza una fiksi sana..
Hapa mkeo alisema huna kazi.
Mke—- yupo tu aliacha na kazi sasa hivi yupo tu nyumbani.,
Si ndio maana yake, nipo nyumbani , siendi kazini kama zamani, maana yake nipo tu nyumbani , lakini si nafanya kazi kazi zangu,

Sijaajiliwa kama zamani,

Na inaweza kuwa ni namna ya ku m tahadhalisha,
Ni kweli nipo nyumbani muda wowote, sio kama zamani muda mwingi sipo ikiwa ni pamoja na kusafiri kikazi,

Labda niweke vizuri hili kuna kipingi miaka kama saba hivi iliyopita nilikuwa nje ya nchi kwa miaka miwili, lakini nilikuwa narudi kila baada ya mirzi sita
 
Mbona unayumba sana..mara Mali..mara watu watatuonaje..ila hapo kwenye hiyo namba saba naona umemaliza kila kitu.
 
Tangu mwanzo wa uzi huu nilitia shaka uhalali wa kisa chako. Lkn huu mwendelezo wa tamthiliya hii umehitimisha nadharia yangu, kwamba hiki ni kisa cha kutunga maana hakuna 'touch' za mtu mzima katika usilimuliaji wako. Kwa kifupi hii ni chai.
Inawezekana ikawa huyu mtoa mada anacheza na akili zetu........😂😂😂😂
 
Inasemakana huyu ndugu anacheza na akili zetu......wataalamu wa kusoma kati kati ya mstari wameshamjua tayari......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…