Mke wangu karudi kwenye dini yake

Mke wangu karudi kwenye dini yake

Habari wakuu

Naomben mnishauri

Mim nilioa miaka 18 iliyopita mpaka niko na mke wangu tuna watoto kadhaa na mali kadhaa.

Sasa huyu mke wangu alikuwa mkiristo mimi muislam KWENYE kufunga ndoa ni yeye alibadil dini na tukafunga ndoa ya kiislam.

Tumeishi vizuri miaka yoote hiyo kwa aman na upendo.

Sasa hivi karibuni nimegundua mke wangu amerudi kwenye dini yake na nimemuuliza amekubali na amesema uislam umemshinda kama NAMPENDA niishi nae hivi hivi tu na ukiristo wake.

Sasa jamani niko njia panda sjui nifanyeje maana naona kama watoto wangu watahangaika mara leo mskitini kesho kanisani.

Hebu nisaidieni
Kauli yangu haitokaa ibadilike kamwe ni kwamba usije oa au kuolewa na mtu ambaye amakubali kubadili dini kwa ajili ya ndoa . Abadili dini kwa sababu ameifuatilia ,kuisoma na kuifahamu kiundani hadi kujua ukweli upo wapi .

Watu wengi ambao nimeona wake zao wamerudi kwenye dini zao za awali hali ya kuwa waliingia kwenye uislamu kwa ajili ya ndoa ni wale wenye sifa hizi hapa chini.

1. Mume si mtu wa ibada na hiii inampelekea mke kuishi bila kufanya ibada na kuona ni jamba la kawaida.

2. Mume haujasoma dini na haujafanya jitihada za kujifunza elimu ya dini basi hata mke wako naye hatofanya juhudi zozote.

3. Mke alibadili dini kwa sababu ya kuolewa sasa meshapata alichokuwa anakitaka na ameamua kurudi kwenye dini yake (hii inaendana moja kwa moja na #1 na #2 japo juu).

4. Mume unajiita muislamu lakini maisha unayoishi si ya kiislamu yani muislamu jina tu.

Yapo meengi ila kwa uchache makubwa ni hayo hapo sasa mkuu jichunguze katika hizo sifa ujue wapi ulikosea .
 
Mi ntabadili dini kuwa muislamu ili nioe binti za kiislamu then narudi katk dini yangu maana jina langu ktk nida bado ni la kikiristo
Kwa binti timamu na anayeijua dini basi hutoweza kumuoa kwa sababu ya kubadili kwako dini , na hata kama itatokea basi muda ule umebadili dini ndoa inavunjika automaticaly hivyo mawanamke anaweza kuondoka zake.

Kingine ni kwamba kama mtu unajiita muislamu halafu huswali swala za faradhi za kila siku basi wewe moja kwa moja umetoka kwenye uislamu.
 
Dini sio jambo la muhimu sana infact hakuna miungu wawili,
Kama anatambua uwepo wa Mungu na anakuheshimu hilo ndio jambo muhimu,
Mtu alieshi dini yake kwa zaidi ya miaka 20 kumtoa hapo sio jambo dogo na kama ulioa ama yupo anaetarajia kuoa imani tofaut aweke kichwani kuwa kumbadili mtu imani ya miaka zaidi ya 20 sio jambo dogo na akubaliane na lolote
 
Hitaji la moyo wa mtu ni kiza kinenee
Endapo hamkwaruzani kwa hilo, na yuko na furaha na wampenda endeleaa nawe kuwa na amani na furaha si ajabu ukaungana nae mara moja moja kumsifu Mungu
 
Kosa ushalifanya Muft wangu,, alafu ukute we mwenyewe Jidah unaenda Eid hadi Eid, ijumaa hadi ijumaa,, Ishi naye tu mlee watoto kwani watoto wakiwa imani nyingine unapungukiwa nn😂, Mungu wetu sote, jivuruge sasa kwa kuongeza mke
 
Shida ilianzia pale mmoja alipokubali kubadili dini lwaajili tu ya ndoa! Huu ujinga hautakiwi

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeongea point sana. Kuna jamaa yangu alioa mke akabaki kuwa mkirsto 20 years ya ndoa mambo tanaenda poa tu. Siku alipotaka kuongeza mke, ndoa ikavunjika. Yeye kashikilia uislamu, mke kashikiria ukristo
 
Akirudi maana yake hakuna ndoa imeshavunjika mnaishi sogea tukae kuanzia sasa hivi

Ulivombadilisha ulimfundisha uislam?

Wewe unaswali swala tano?

Ulimfundisha kuswali na afuate mafundisho yake?
Upo vizur Aaliyyah Ipo ndoa yamtu wangu wakaribu imevunjika hivi karibuni..alipoenda kwa viongozi wa dini alipewa jibu hilo kuwa hiyo ndoa ilishavunjika tangu siku huyo mwanamke aliporudi kwene dini yake kwaiyo walikuwa wanaishi kama wazinzi tu.
 
Habari wakuu,

Naombeni mnishauri.

Mimi nilioa miaka 18 iliyopita mpaka niko na mke wangu tuna watoto kadhaa na mali kadhaa. Sasa huyu mke wangu alikuwa mkiristo mimi muislam kwenye kufunga ndoa ni yeye alibadil dini na tukafunga ndoa ya kiislam.

Tumeishi vizuri miaka yote hiyo kwa amani na upendo.

Sasa hivi karibuni nimegundua mke wangu amerudi kwenye dini yake na nimemuuliza amekubali na amesema uislam umemshinda kama nampenda niishi nae hivi hivi tu na ukiristo wake.

Sasa jamani niko njia panda sjui nifanyeje maana naona kama watoto wangu watahangaika mara leo mskitini kesho kanisani.

Hebu nisaidieni.
Mkeo hakufuata dini kwako alifuata mapenzi ya mwili. Usimlaumu kwa sasa mapenzi hamna kaenda kwa Mwamposa hageuki tena, wewe hakikisha hapeleki hela zote huko.
 
Umeongea point sana. Kuna jamaa yangu alioa mke akabaki kuwa mkirsto 20 years ya ndoa mambo tanaenda poa tu. Siku alipotaka kuongeza mke, ndoa ikavunjika. Yeye kashikilia uislamu, mke kashikiria ukristo
Sasa hapo angeahirisha kuoa tuu maana lengo lilikuwa awe na wake wawili. Angemwomba mkewe yaishe waendelee na maisha.
 
Upo vizur Aaliyyah Ipo ndoa yamtu wangu wakaribu imevunjika hivi karibuni..alipoenda kwa viongozi wa dini alipewa jibu hilo kuwa hiyo ndoa ilishavunjika tangu siku huyo mwanamke aliporudi kwene dini yake kwaiyo walikuwa wanaishi kama wazinzi tu.
Huo ndo ukweli japo mchungu
 
Onana na kiongozi wako wa msikiti, umpe hicho kisa akikwambia ndoa ipo kisheria basi ruhuaa kuendelea nae(utamuacha tu kwa maamuzi yako) ila watoto wape elimu nzuri ya dini uhakikishe wameijua na usiwalazimishe upande wa kuwepo, kikubwa wape elimu.
Ima sheikh akisema ndoa hamna hapo, basi huna budi kuachia goma.

Je ulivyombadili dini ulimpa elimu ya dini, ulikuwa kiongozi mzuri kwake, ama ndio ile muislam jina, ukiwa muislam lazima uoneshe athari za uislam wako, marafiki, majirani n.k wote wapate athari kwamba huyu kweli ni muislam

Pole kwa yote mkuu.
 
Kubadili dini kisa ndoa ni uongo, ni kheri muoane kila mtu abaki na dini yake.
Mkiwa ndani ya ndoa huenda mmoja anaona dini ya mwenzie ni njema akajoin the chain.

Hii imewahi kutokea kwa muislam alieoa mkristo, ndoa imeenda almost 10yrs baba mtu akabadili dini na kua mkristo, wakati huo watoto wote tayari walaishafata dini ya mama.
Na sasa familia yote ni wagalatia.
 
Onana na kiongozi wako wa msikiti, umpe hicho kisa akikwambia ndoa ipo kisheria basi ruhuaa kuendelea nae(utamuacha tu kwa maamuzi yako) ila watoto wape elimu nzuri ya dini uhakikishe wameijua na usiwalazimishe upande wa kuwepo, kikubwa wape elimu.
Ima sheikh akisema ndoa hamna hapo, basi huna budi kuachia goma.

Je ulivyombadili dini ulimpa elimu ya dini, ulikuwa kiongozi mzuri kwake, ama ndio ile muislam jina, ukiwa muislam lazima uoneshe athari za uislam wako, marafiki, majirani n.k wote wapate athari kwamba huyu kweli ni muislam

Pole kwa yote mkuu.
Hamna ndoa kaka ishavunjika hata aende akaulize Makkah 😄
Hiki kisa Kuna mmama alinisimulia Dec nae alirudi kwenye ukristo na wamezaa na mumewe watoto 4 sababu alisema hamfundishi dini mwanaume haend msikiti kabisa nae haend hata atembee kichwa wazi mume Hana mpango tu Yan muislam jina tu dad wa watu karudi anasali na hawana ndoa wanafanya mpango wafunge ya serikali au waachane tu
 
Back
Top Bottom