Mke wangu kawa chanzo cha kuvunjika kwa ndoa ya jirani yangu

Mke wako jembe sana. Umewekeza mno kwa michepuka ukasahau kujenga nidhamu ndani ya ndoa yako. Mwanakulitaka mwanakulipata,mwanakulitafuta mwanakulipewa. Mwanakulitikita mwanakulitokota. Hamia kwa mama J
Nihamie kwa mamaJ?
Wallahi Wee unitakii mema[emoji848]
 
Kuonana na ticha nilishawaza Sana baada ya kikao na mwenyekiti,
Nikaweka ratiba kua nikishatoka kazin ndo ntaenda kwake.

Sasa nilivyofika nikakuta kamtimua mkewe kwa mkofi na mabegi kamtupia, Kuna mtu akanishaur nitulie kwanza hasira zake zipungue ndo nikaonane nae.
 

Nimepata hasira kukuzidi wewe, huyo mke wako Ana makosa 3,,

1. Sio mshauri mzuri kwa rafiki yake.
2. Hana adabu na anakudharau.
3. Kamkosea sana teacher!

Nasikiaga tu kuhusu single mothers, kwa hii simulizi, kweli sikio la kufa halisikii dawa.

Kwako Sasa mdau, the assumptions is this, mke wako a naona ni sawa kabisa mtu kuwasiliana na x wake na kuonana naye, mke wako is a time bomb. Weka msimamo mkali akishindwa fukuza.
 
Sahii kabisa,
Nikirudi nikamkuta nafukuza wote
 
Usije kuthubutu single mother ni hatari sana ...unamuweka ndani siku mbili unampiga nguo za maana anaridhika anapata shavu ,jmaa yake anaanza kumtamani Tena kwa kigezo cha mtoto lazima tu atamla Tena.
Kuna ukweli Hapa[emoji848]
 
Sinaga ushoga usiohisiana na kutafutiana michongo ya pesa.nucta
SIPATAGI MATATIZO YOYOTE POPOTE NINAPOISHI.
Yaani sina common interest na mtu ya kutafuta pesa hatuwez kuwa mashoga?
Tutazungumza nini zaidi ya mbinu za kijinga jinga.
Huo ushoga wa mkeo na huyo dada hauna common interest
Wote vichwa vyao maji
Kwanini aingize mgeni nyumbani kwako bila kukupa taarifa?
 
Upo sawa kabisa mkuu...ila visa kama hivi ndio vinazidi kufanya watu waogope kuoa single mamaz !
1. Nimekuwa nikiwatetea sana dada zetu
waliozalishwa kabla ya ndoa na kutelekezwa lakini wao wanajiharibia na kuwaharibia wenzao sana kwa matukio ya kijinga kama haya.

2. Huyu dada kaheshimishwa sana na ticha lkn amesahau taabu zote na jinsi alivyofutwa machozi na ticha...bure kabisa

3. Kuna watu huwa wanasema tusiwaamini wanawake..huwa nakata lkn kiukweli wanawake ni dhaifu mnoo.

4. DeepPond ulicheza vyema nafasi yako tangu awali kwa kukemea uovu huo.

Nakusihi urudishe moyo nyuma uinusuru hii ndoa...huyo mchaga anachotaka ni mtoto tu mdivyo walivyo.

Hivyo muite ticha wakalisheni wake zetu.

Onyesha kuchukizwa zaidi na kitendo cha mkeo ili u win moyo wa ticha.

Mwisho kabisa mshauri ampe huyo binti mjinga nafasi ya mwisho kwa sharti kuwa mwanae apelekwe kwa wazazi.
 
Hapana, unapokaa kimya ndo unazidi kumuumiza anakuwazia mengi sana na shemeji pia. Nenda na mwenyekiti kamwombe msamaha, sisi wanaume tukiombwa msamaha na wanaume wenzetu huwa tunaamini jamaa kajishusha Sana, lazima asuuzike moyo.

Ila bro, shemeji kazingua Sana, nakuhakikishia kwa uzoefu wangu wa Mambo ya ndoa, ticha atalipa Jambo. Tumia akili kubwa Sana. Wife mrudishe kwao kwanza hata kwa mtego ili ujisafishe, ujinga wake aubebe mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…