Mke wangu kawa chanzo cha kuvunjika kwa ndoa ya jirani yangu

Dada napingana na wewe, mke wake ndiye aliyefanya connection za kuwakutanisha Malaya, naye si msafi, Kama anafanya nyumba ya mumewe kuwa danguro Kuna mke hapo? Huenda hata mke wake anaingiza wanaume kwa upuuzi huu
Huenda mchaga huwa anaitumia nyumba ya @Deepond kupasha kiporo.
 
Niliruhusu vip wkt matukio yote yanatokea nilikua Sijui,
Mkuu, mi sio mtu wa kushinda nyumbani

Nikiondoka asbh, kurudi ni saa 5 au 6 usiku
Asante mkuu, narudia tena, ULIRUHUSU!! Pale pale ulipobaini jambo hilo ulipaswa kuchukua hata kali mno!! Ulipaswa kulitazama kama kwamba kumbe kuna mchezo, wanatunziana siri. Halafu ungetishia kuvunja ndoa yako kwani huwezi kuishi na mwanamke mwenye tabia za kihuni. Mke wa ndoa ni DHAMBI KUBWA kushiriki ujinga huo. Ndipo nikasema hukulikemea vya kutosha mkuu wangu.
 
Niliruhusu vip wkt matukio yote yanatokea nilikua Sijui,
Mkuu, mi sio mtu wa kushinda nyumbani

Nikiondoka asbh, kurudi ni saa 5 au 6 usiku
Yumkini ungepay attention kwa familia yako ungegundua mapema na kuestablish misimamo kama mwanaume ndani ya nyumba. You have paid more attention nje do you see whats happening.

Familia inaanza kucrumble down slowly. Shetani ukimpa nafasi hafanyagi ajizi. With all due respect mkuu..si kwamba nakufundisha chochote. Its just a reminder. Familia inajengwa si bora liende. Sitaki hata kuwaza kuwa yumkin na mkeo anaweza akawa anago... Nje naogopa. Lakini if you were keen ungetambua. Kama unahisi unaipenda familia yako...tengeneza. na kama unaona ni porojo basi fresh. Ubaya ukishaingia...hauondoki mpaka umalize kazi uliokuja kuifanya. Beware.
 
Tusivunje ndoa mbili, hebu tuokoe moja, yeye aendelee kumdukua mkewe atamshika tu
Kama ana weledi kidogo tu, habari za mkewe kwa asilimia 60 zaweza kuwa kwenye simu ya huyo mke wa Mwalimu. Wanawake wana mbinu za hovyo sana. Kama anavyotumiwa mkewe kusuka mchongo ndivyo ilivyo kwa mkewe pia. Hiyo ndio mbinu wanayotumiakuwasiliana na Bwana zao, hawezi kugundua labda afanye fumanizi.
 
Shukran mkuu Juandeglo,
Nmekupata vema kabisa mkuu,
Nakuahidi ntalifanyia kazi kuanzia sasa[emoji120]
 
Makelio ndio vifaa gani mama D
 
Fanya kumsaidia jamaa aliyenda south kupambana alafu akarudi kuendeleza alipoishia uyo teacher hampendi uyo mke wake usimlaumu mkeo kajitahidi kwa upande wake hana kosa jamaa yupo tayari kumuoa uyo binti mwambieni binti arudi kwa mzazi mwenzake teacher atamuua binti wa watu atamchukia mtoto

Tulishakubaliani hatuoi single maza hadi aoneshe kabuli la baba ona sasa yamemkuta teacher [emoji16]

Uyo teacher atafute chimbo lingine mtoto ni vizuri akaish na wazazi wake usimchukie mkeo
 
Afu mke wa mtu kaja na mizigo kwako unamwacha tu mpaka analala? Unajua hiyo ni picha mbaya sana kwa mume na jamii? Nani atakuamini tena? Kwani huyo binti hana wazazi ama ndugu? Je, mamlaka za kiserikali hazipo hata aje kukusukumia wewe mzigo wa lawama?

Hapo mkuu ulipaswa SIKU HIYO HIYO kumpa likizo mkeo arudi kwao kwanza. Hiyo ingesaidia mambo matatu:
1. Kumtia hofu kuhusu usalama wake(mwanamke haolewi kwa sababu kampenda mume, anaolewa kupata security.

2. Kuwaamsha wazazi wake wamweke chini tena, wewe huna uwezo kumbadili mke, atakuletea kiburi na dharau tu kama alivyofanya.

3. Kusafisha hewa mtaani, kwani watu wote akiwemo Mwalimu wangebaini kwamba hukujua jambo hilo na pia umechukizwa sana. Hili lingekujengea heshima kubwa.

Kwa sasa watu wanaamini huo ulikuwa mchongo wenu wewe na mchaga, mkeo na Mrs Mwalimu. Action vs words, huwezi kujieleza ukaeleweka mkuu. Hata mimi nisingekuelewa katu!!
 
Usemalo Ni kweli kabisa mkuu,
Sema binti alitakiwa kujua Yuko kwenye mahusiano mengine kabisa.

Tena mahusiano serious na official kabisa
Hakupaswa ku-entertain upuuzi wa namna hiyo kwa jamaa
Teacher alifanya maamuzi magumu sanaa, kuoa mke mtarajiwa wa jamaa aliyeko safarini

*Isijekuwa jamaa aliposafiri alikimbia jambo..... mama D akapambanaa, akapendeza, kisha mawifi wakawa wanamwambia baba D, fulani amependezaa, baba D genye mshindo zimempanda anataka ongeza cha pili halafu arejee tena south africa, anamwachia mama D alee mwenyewe
 
Humtakii mema Baba G πŸ˜…
 
Ila inaonekana mama G na huyo rafiki yake bado Wana usichana mwingi, mwanamke mtu mzima na akili zake hawezi kuentertain hizo drama.
 
Manamake mengi ni majinga na mapuuzi makubwa.

Mkuu nilikua najiuliza sana hivi unafanya biashara gani maana nilivo soma uzi ule wa kuhusu mchepuko wako jinsi unavyomjari nikaona una pesa sana wew nikaanza kufikiria unafanya mishe gani hapa ndio nimepata jibu
Mmmh mkuu now your at the top [emoji41]

Ngoja niendelee kupambana naamini na mimi hipo siku hizi laki laki zitakuja kua sio shida kwangu.


Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Usifadhaike sana kwani nawewe usijisahaulishe mahazabe yako na makando kando kibaoπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Mkuu hawa viumbe tuwachukuliage tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…