Mke wangu mchafu, nimeongea nimechoka


Ungetushirikisha wakati unamuoa. Mda huu tungekuwa na cha kuchsngja
 
Ajiri dada wa kazi,ili usikereke na uchafu wa mkeo
 
Mvumilie, kwa shida, raha na mapungufu.
 
Umepata usiefanana nae
 
Vp kwa bibi hali ikoje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ye mwenyewe msafi na anajali mwili wake afadhali, inawezekana mkeo kakulia mazingira ya hivyo nyumbani kwao unakuta kijana wa kazi ndo alikua kila kitu kwenye usafi wa nyumbani. Ko jaribu kumbadilisha taratibu, tabia nyingi za ukubwani zinachochewa na malezi ya utotoni.
 
Kuna naturally wako hvyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwambie ataft house girl wa kitanga tena mshika dini atamsaidia kuelewa mambo ya usafii. Wanapiga deki Hadi uvunguniii
 
Sawa,huo ni udhaifu wake.hakuna asiye na kasoro bro.Lichukue hili ni kasoro ya mkeo.Ila tabia hiyo isiende kwa watoto wenu hasa wa kike maana huko tuendako wanaume wavumilivu wanapungua kwa kasi sana.
 
Tatizo ni lako, sio la mke wako. Kama ujiwa mwenyewe unaweza kufagia ndani na nje, kutandika kitanda, kufua nguo, kuosha vyombo n.k. kwa nini uache kwa sababu mke wako yupo? Ukiona yanakushinda ajiri mtu wa kufanya kazi hizo siku zote. Inaelekea mke wako ameajiriwa lakini unataka afanye yote hayo, aende kibaruani na akirudi akupikie vile vile! Vyote hivi unaona ni wajibu wake kama mwanamke maana sijakusikia ukilalamika kuwa mtoto wako wa kiume nae hafanyi usafi! Inabidi ubadilike.

Amandla...
 
Non sense

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi pia napitia hali km yako mkewangu asubuh yeye anajua kutoka kitandani tu anashindwa kutandika hata kitanda, vyombo mlivyokulia vinaweza kukaa hata siku tatu nguo hafui...ninachokifanya mimi nikikuta hajatandika kitanda natandika, nguo nafua mpaka zake nafagia ila vyombo ndio inakua ngumu kuosha...km ukiacha mazingira hayo yakiwa machafu na ww basi ww pia mchafu we fanya usafi tu au tafuta msaidizi km unajiweza
 
Sisi tumefindishwa na maadili kuwa unapotaka kuoa unaangalia mambo mapana
Kwanza familia nzuri, msichana mzuri na mwenye hofu ya Mungu au tuseme mcha Mungu hapo lazima atakuwa msafi
Hapo wewe inaonekana hata kwao hupajui kabla ya kuoa

Utakuta ni familia iko hivyo na mama yake mchafu pia maana kama na mwanao kawa mchafu basi na yeye haikutoa mbali hii tabia

Pambana sana kumbadilisha au kataa kabisa kula chakula anachopika na hata yeye unamtenga kwa uchafu wake

Lazima mtoto unahakikisha asiwe kama mama yake na mwambie ukweli kuwa mama yako mchafu hilo sio aibu Sema kama wimbo kila saa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…