Jina la ubini wa baba ni Cheo cha heshima anachobeba mtoto kwa heshima ya baba!
Baba aliyepambana usiku na mchana kuhakikisha mtoto unaendelea kuwa hai, mwenye afya, mwenye kukua na kupata mahitaji yote ya kijamii
Kutelekeza mtoto ni kupoteza haki zako zote mbele ya mtoto
Mtoto aliyetelekezwa anaingizwa kwenye jamii mpya inayomtunza, na kumkuza
Niwakumbushe tu, watoto wengi wanazaliwa na wababa wa nje ya ndoa lakini wanatumia ubini wa baba mwenye ndoa,
Niwakumbushe tu watoto wengi walibadilishiwa ubini ili kurisiti mitihani ya darasa la Saba enzi zile
Niwakumbushe tu, wanawake hapo zamani ndani ya ajira zao ( mama yangu kwa mfano) walibadili ubini na kuchukuwa ubini wa mume
Masingle mother wawe na shukrani kwa waume wanaojitoa kulea watoto waliotelekezwa, wawaruhusu kujenga muunganiko na watoto Hawa kwa kutumia ubini wa baba