Mke wangu ni mchawi ama mama ndio mchawi?

Mke wangu ni mchawi ama mama ndio mchawi?

Hao wana misunderstanding zao binafsi, wametumia neno uchawi kama njia ya ku articulate feelings zao.

Ningekuwa ni mimi, hapo uliposema unapata upepo ndio ningeitumia kuwa alika kila mmoja bila wao kujua kua watakutana halafu wanatoa dukuduku zao na ku press reset button kumaliza fitna zao

Hakuna uchawi
Sasa mkuu kama hakuna uchawi kwanini kila mmoja ajinadi kwa kusema atanipa dawa ili nimuone mwenzake
 
Hapo wote wachawi wameshindwana hivyo wamekimbilia kwako kuitafuta amani. Kwa nini nasema hivyo? Ni kwa sababu wote wametoa dawa ili ushuhudie, kwa kawaida aliye na uwezo wa kuona visivyoonekana kwa jicho la kawaida kwa madai kuwa anawatu kichwani huwa Hana dawa zaidi ya kutegemea wale Majini/Mashetani waliopo kichwani. Kuja kwako Mungu amekuchagua wewe ili uwasaidie tumia hekima jambo linaisha hilo kiongozi.
 
Hizi Mambo zinaweza zikakupotezea Hadi taste ya maisha!
Kwa experience yangu mm na hayo Mambo na kwa yaliyonikuta hapo inaelekea Mama ako sio mtu mzuri! Mkeo anajua hilo...atakachokifanya ni kumchukua mkeo na kufanya kila mbinu muachane! Pole ndio ukubwa
 
Habari wana JF

Mimi ndugu yenu nina makubwa ambayo yamenifika na sijui nitayatatua vipi?

Nina mke wangu nilimuoa mwaka 2015, baada ya kuishi nae miaka kama 7 sasa kuna siku juzi nipo kazini nikapokea simu kutoka kwa mdada wa kazi pale nyumbani akinitaka nirudi haraka nyumbani, bila kusita nikafanya hivyo baada ya kama lisaa nikawa nishafika nyumbani, nikamkuta mke wangu kakaa chini sebuleni kama analia afu mdada wa kazi kasimama. Nikamuuliza mdada kuna nini hapa akaniambia naona kama dada kapandisha mashetani!! Ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona mtu au mke wangu kapandisha mashetani, yakawa yanalia kwa sauti kubwa mnoo huku anajipiga piga chini.

Baada ya dakika 4 za kulia yakanitaka tuanze mazungumzo ila kwa sharti yule mdada wa kazi ama mie nimshike sikio mke wangu "kiti" kwa lugha yao. Kupitia mdomo wa mke wangu yale majini/mashetani yakasema kuwa yamekuwa yakipambana na MCHAWI kwa takribani mwaka sasa ila leo yameona vita inataka kuwashinda hivyo kiti "mke" anaweza akazidiwa na kupoteza maisha.

Nikawauliza huyo mchawi wamemuona wapi au anatokea wapi? Yule jini akaniambia je unatuamini? Au hautuamini? Kulingana na shauku ya kutaka kujua hilo tatizo linalotaka kuchukua maisha ya mke wangu ikanibidi niombe kutajiwa kwa kujibu "ndio nawaamini" Basi yule jini aliyepo kwa mkewe wangu akaniambia bila hata kupepesa macho kuwa "Mchawi ni bi fulani" ambaye ni mama yangu mzazi kabisaaa. Nilishtuka sana kiasi kwamba nilitamani hata kuchapa fimbo wote waliokuwepo palee ila nikajikaza na kuacha lipite. Basi hiyo siku ikapita.

Baada ya siku kama 3 nikapokea simu kutoka nyumbani kwa wazazi wangu, nikaenda bila kusita kufika tu baada ya mama kuniona akaangua kilio na kunikumbatia kwa huzuni. Ikabidi nimuulize mama kulikoni? Kuna tatizo? Au kuna msiba? Akasema hapana kuna jambo nimekuwa namuhadithia baba yako kila siku hivyo na wewe yakupasa kulijua leo. Nikamwambia sawa mama niambie...basi akaanza kusema "ujue mwanangu mie mama yako huwa nina karama kama sio bahati fulani kichwani mwangu toka nikiwa binti mdogo tu, nina uwezo wa kuona na kuzungumza na vitu/viumbe ambavyo wewe kwa jicho lako hilo la nyama huwezi kuona"....baada ya maelezo mengi tu ya historia na nguvu zake hizo ndipo mama bila kusita akasema "Mwanangu mkeo ni MCHAWI" kama utakubali sema nikupe dawa ambayo itakusaidia kumuona bila yeye kujua ili ikusaidie kusadiki haya ninayo yasema na badae uchukue hatua...

Basi nikarudi nyumbani nikiwa na mawazo mengi nisijue nini kinaendelea hapa katikati. Nikafika nyumbani ile kuingia tu mke akaanza kupiga kelele kama jogoo huku akinifuata kwa hasira na kuniomba nimpe nilichopewa na huko nilipotoka. Nikashtuka mnoo!!

Ikabidi niitoe ile dawa na kumkabidhi mke wangu, baada ya dakika 3 akaniambia sasa achana na hii dawa ngoja nikupe ya kwangu ili ushuhudie mama yako anachotufanyia usiku.

Nikamwambia kwa sasa hapana ngoja nifikirie then nitakuambia unipe...

Ndugu zangu nipo hapa Sea clif napata upepo nikitafakari nini kinaendelea kwenye familia yangu haswaa kwa watu ninaowapenda mnoo. Je yupi ni yupi?

Nipeni ufumbuzi.
Mkuu unayasikiliza na kuamini majini?
Shetani ni baba wa uongo cha kufanya hapo wachukue wote wapeleke kwenye maombi au mlete mchungaji aje afanye maombi hapo nyumbani kwako
 
Mama ako hana madhara kwako? Biblia iliposema "usimwache mwanamke mchawi aishi" haikudanganya. Subiri ifikre zamu ya mama yako kutoa sadaka kama hajawatoa nyie watoto wake au wajukuu zake. Au subiri hadi amrithishe mtoto wako mmoja mikoba, ndiyo utajua hana madhara.

Wachukue hao wote mkeo na mama yako, wapeleke kwenye maombi
Ndio mama hana madhara kwangu ila mke ananiambia kuwa anataka kuchukua uhai wake hivi karibuni!..
 
KAMA NI MUISLAM NJOO PM HARAKA NIKUPE MAELEKEZO YA KUFANYA BILA GHARAMA YOYOTE. HARAKA IWEZEKANAVYO.

INSHAA ALLAAH, BI IDHNI LLAAH ITAKUSAIDIA NA UTAFANIKIWA.

KAMA SI MUISLAAM, NACHELEA NAMNA YA KUKUSAIDIA...
 
Inaonekana mama yako alianzisha ligi, ndipo akakutana na mwamba;ila ndio ukubwa hutakiwi kukimbia ndoa, kusuluhisha wachukue wote wawili wapeleke kwenye maombi; atakayekataa ndio chanzo cha ugomvi.
 
UCHAWI UNADHURU HATA KAMA HUUAMINI...UTAKUDHURU TU ALLAAH AKIRUHUSU UKUDHURU...NA VILE VILE MWENYE UWEZO WA KUZUIA MADHARA YA UCHAWI NI ALLAAH...

CHUKUA KILA AINA YA TAHADHARI YA UHAKIKA NA SALAMA JUU YA MADHARA YA UCHAWI WA MAMA YAKO NA MKEO.
 
Pole sana kwakweli ni mtihani. Nimejikuta nacheka sana kama ni mazuri vile
 
Okey mkuu nimekuelewa,je hawa wanao nifuata inbox ni waganga au watu wa maombi?..ningependa zaidi wangejipambanua maana hata mie nina hofu nikienda kiuganga nitaweza kupotea zaidi

Hao wa inbox achana nao, achana na wafuatao:

  • Manabii wanaofuatwa na famous.
  • Kwenda kichwa kichwa kanisan

Cha kufanya:

Create muscle - Omba Mungu peke yako serious, hata Kama Hujui kuomba wewe funga na mwombe Mungu tu alone.

Nina uhakika atakuongoza Kwenda Kanisa Fulani ambalo litakuwa la Msaada kwako, sincerely: Kuna Makanisa Mazuri Sana Dar and are not famous!

Hapa pagumu, ukiyumba hapa unaharibu kila kitu, don't take this light, you real need God at a personal level kwanza, then maombi
 
Back
Top Bottom