Mke wangu ni mchawi ama mama ndio mchawi?

Mke wangu ni mchawi ama mama ndio mchawi?

Mkuu hao wote ni wachawi na wameshajuana. Wanachofanya ni kujihami kwako. Omba sana Mungu kwa imani yako.
 
Pole aisee kiatu chako hakivaliki,, kila la heri ktk kutatua hili
 
Habari wana JF

Mimi ndugu yenu nina makubwa ambayo yamenifika na sijui nitayatatua vipi?

Nina mke wangu nilimuoa mwaka 2015, baada ya kuishi nae miaka kama 7 sasa kuna siku juzi nipo kazini nikapokea simu kutoka kwa mdada wa kazi pale nyumbani akinitaka nirudi haraka nyumbani, bila kusita nikafanya hivyo baada ya kama lisaa nikawa nishafika nyumbani, nikamkuta mke wangu kakaa chini sebuleni kama analia afu mdada wa kazi kasimama. Nikamuuliza mdada kuna nini hapa akaniambia naona kama dada kapandisha mashetani!! Ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona mtu au mke wangu kapandisha mashetani, yakawa yanalia kwa sauti kubwa mnoo huku anajipiga piga chini.

Baada ya dakika 4 za kulia yakanitaka tuanze mazungumzo ila kwa sharti yule mdada wa kazi ama mie nimshike sikio mke wangu "kiti" kwa lugha yao. Kupitia mdomo wa mke wangu yale majini/mashetani yakasema kuwa yamekuwa yakipambana na MCHAWI kwa takribani mwaka sasa ila leo yameona vita inataka kuwashinda hivyo kiti "mke" anaweza akazidiwa na kupoteza maisha.

Nikawauliza huyo mchawi wamemuona wapi au anatokea wapi? Yule jini akaniambia je unatuamini? Au hautuamini? Kulingana na shauku ya kutaka kujua hilo tatizo linalotaka kuchukua maisha ya mke wangu ikanibidi niombe kutajiwa kwa kujibu "ndio nawaamini" Basi yule jini aliyepo kwa mkewe wangu akaniambia bila hata kupepesa macho kuwa "Mchawi ni bi fulani" ambaye ni mama yangu mzazi kabisaaa. Nilishtuka sana kiasi kwamba nilitamani hata kuchapa fimbo wote waliokuwepo palee ila nikajikaza na kuacha lipite. Basi hiyo siku ikapita.

Baada ya siku kama 3 nikapokea simu kutoka nyumbani kwa wazazi wangu, nikaenda bila kusita kufika tu baada ya mama kuniona akaangua kilio na kunikumbatia kwa huzuni. Ikabidi nimuulize mama kulikoni? Kuna tatizo? Au kuna msiba? Akasema hapana kuna jambo nimekuwa namuhadithia baba yako kila siku hivyo na wewe yakupasa kulijua leo. Nikamwambia sawa mama niambie...basi akaanza kusema "ujue mwanangu mie mama yako huwa nina karama kama sio bahati fulani kichwani mwangu toka nikiwa binti mdogo tu, nina uwezo wa kuona na kuzungumza na vitu/viumbe ambavyo wewe kwa jicho lako hilo la nyama huwezi kuona"....baada ya maelezo mengi tu ya historia na nguvu zake hizo ndipo mama bila kusita akasema "Mwanangu mkeo ni MCHAWI" kama utakubali sema nikupe dawa ambayo itakusaidia kumuona bila yeye kujua ili ikusaidie kusadiki haya ninayo yasema na badae uchukue hatua...

Basi nikarudi nyumbani nikiwa na mawazo mengi nisijue nini kinaendelea hapa katikati. Nikafika nyumbani ile kuingia tu mke akaanza kupiga kelele kama jogoo huku akinifuata kwa hasira na kuniomba nimpe nilichopewa na huko nilipotoka. Nikashtuka mnoo!!

Ikabidi niitoe ile dawa na kumkabidhi mke wangu, baada ya dakika 3 akaniambia sasa achana na hii dawa ngoja nikupe ya kwangu ili ushuhudie mama yako anachotufanyia usiku.

Nikamwambia kwa sasa hapana ngoja nifikirie then nitakuambia unipe...

Ndugu zangu nipo hapa Sea clif napata upepo nikitafakari nini kinaendelea kwenye familia yangu haswaa kwa watu ninaowapenda mnoo. Je yupi ni yupi?

Nipeni ufumbuzi.
Mama yako anasema ana karama ya kuona matukio, Je kuna dawa ya kumuonyesha mtu maono yako? Hivyo Mama ni member, Pia Mke alipandisha mashetani, inaonekana naye kama sio member wa kudumu basi amepitapita huko wanakoongeza matatizo na hayo mauchafu aliyabeba pengine yamlinde. Sasa yawezekana mama alikuwa anjaribu kwa mkeo kumbe na mkeo nae kafungasha. Apo ita wote , Baba, Mama, Mkeo na Mkwe ikibidi. Na kama ukweni hawana itikadi za kishirikina watakusaidia sana kumaliza hiyo. Kabla ya kwenda church au wapi kwanza ita wote kila mmoja aeleze kwanini ana muhisi mwenzie, interrogation kwa wanawake is an esiest thing lazima watalipukiana na mmoja atasema ukweli tu. Pia wewe ni wakiume kama una uhakika na umejidhihirishia baba sio member, mvute chemba akupe dots za mama kisha kaa uka connect mwenyewe, Pia linganisha na za mkeo kwa miaka sita yote. Naimani utapata kitu.
 
Kama stori yako ni ya kweli, hapo wote wachawi hao...

Mama yako kakiri kuwa na 'karama ya kuona' watu wabaya, halafu kakupa nawe dawa ili uweze ona mauzazuza ya mkeo, kuwa na karama haina maana unakuwa na uwezo wa kutengeneza dawa...kama anatengeneza dawa huyo ni fundi tayari

Pia kwa mkeo ni wale wale tu, ana uchawi wa maruhani, na kitendo cha yeye kukupa dawa ina maana na yeye ni fundi...

Nina swali moja, kama mama yako ana karama ya kuona mauzauza, iweje hakuona kabla mwanamke uliyenaye hajawa mkeo?
Ibarikiwe mkuu hata mimi mkewangu ana tatizo la maluhani anapandisha mara kwa mara anapoona wachawi au kitu kibaya
 
Ibarikiwe mkuu hata mimi mkewangu ana tatizo la maluhani anapandisha mara kwa mara anapoona wachawi au kitu kibaya
Mkuu kma unataka msaada kuhusu tatizo lko nambie nikusaidie usione jambo dogo ilo
 
Very true.nilimsikia mama mmoja upendo Tv alisema kama kwenye familia kuna mama mchawi wale watoto wake wa kiume lazima ataoa mwenga mchawi ili kuendeleza uchawi wao..
Hao wote wanga. Walikuwa timu moja wamezidiana speed. Mamaako ndio alimshauri mkeo aolewe na wewe baada ya kukutana anga zao. Sasa wamezidiana speed,wamechenjiana
 
Wote wachawi

Wewe na hao wachawi wenzako.

Unasikilza maruhani
 
Ushauri

Ningekuwa Mimi ningefanya yafuatayo.
Kwa kuwa Dawa uliyopewa na Mama umuone mkeo tayari Ulishamkabidhi mkeo. Mwambie Mkeo Akupe hiyo Dawa kiboko ya kumuona Mama yako.. itumie Kama ukifanikiwa kumuona Mama yako mubashara Akiwanga mshukuru Mkeo then mwambie Utajua namna ya kushughulika na Mama yako.

Kisha Rudi kwa Mama Kama hakijatokea kitu Mwambie Mama ile Dawa ya mwanzo Mke wangu Aliigundua na kuninyang'anya mapema kabla sijaitumia. Hivyo Naomba hiyo Dawa Unifanyie huku huku nyumbani au twende sehemu Nyingine ili nimuone Mke wangu mubashara Lazima atakubari Atakufanyia Hiyo Dawa na utamuona Mke wako Akiwanga kama kweli ni mchawi katika trick hii Utaujua ukweli hivyo hata Ukiamua Kuchukua hatua utakuwa Unajua unachofanya. Kikubwa Tafuta ukweli bila kuwa na upande.
 
Back
Top Bottom