Ruyama
JF-Expert Member
- Sep 6, 2019
- 367
- 563
Aisee [emoji44]
Kwa uzoefu wangu,Mme na mke mkishaanza kupeleka mashitaka Mara kwa wazazi,kwa balozi sijui wazee Wa kanisa au sijui kwa jirani,hapo hakuna ndoa ni michosho tu,Mimi naamini kuwa ikiwa mke wangu nilimtafuta mwenyewe na tukaelewana sisi wawili hadi kufikia kuoana hivyo na mambo yetu yatamalizwa na sisi wawili,majirani ,padri,mchungaji na balozi kamwe hawezi kuwa suruhisho la ndoa
Hivyo kama mlitafutana ninyi wawili,mnawajibu Wa kuyamaliza ninyi wawili,uamzi ni wako kumeza au kutema,lakini pia bora pengo kuliko jino bovu.
Kuhusu swala la kukuroga hapo anakutisha tu,kumuua mtu au kumroga ni kazi ngumu sana kuna vitu vingi sana yapaswa vikamilishwe ili kutimiza lengo,na nakuambia hawezi kwani inavyoonekana wewe ni muoga Wa nguvu za Giza hivyo anatumia uoga wako kukuendesha,hakika nakuambia utapata tabu sana.
Mwisho ,Maisha ya duniani ni mafupi sana,Fanya uwezavyo uyaishi kwa furaha,kamwe usiruhusu mtu awaye kuvuruga na kuingilia amani ya Maisha yako na kukufanya uteseke ,fukuza oa mwanamke mwingine,akileta jeuri fukuza oa mwingine,hadi siku ya kifo chako,lengo ni kuhakikisha unaishi Maisha ya furaha,babu Yangu alioa Mara tano,mke Wa kwanza alifukuza hivyo hivyo Wa pili ,tatu,nne akaja kufa akiwa na mke Wa tano,lengo lake ilikuwa ni kutoruhusu huyu kiumbe mwanamke anampa tabu maishani mwake.
Ova.