Mke wangu vitendo ulivyomfanyia Mama yangu sitosahau kamwe

Mke wangu vitendo ulivyomfanyia Mama yangu sitosahau kamwe

Wakuu wa ndoa mmekuja.kimkakati eeh?, any way mbona umeshangaa sana mkeo kumjali mama yako ina maana sio jambo la kawaida huko kwenye ndoa?.

Ila Bro mbadilishie mama yetu maisha hapo kijijini, sio fahari kumuacha mama anateseka kijijini kaka.
Mambo mema yapo tena mengi tu, watu hawataki kuyaongelea...ila yapo na watu wanayaishi.
 
Nakiri kusema Kwa furaha hio ya mama utabarikiwa maradufu
Nilipoona tittle ya thread nikajua ni mambo ya kutisha atakua amefanya kumbe jambo la heri
Ameeni ameeni Mtumishi
 
Hongera Mwanetu.
Toa tips wanao wapone mana daily wanavamia michongoma.
Huku nje vilio vingiii
 
Ilikuwa ni mwishoni mwa Mwaka jana 2022.

Basi kutokana na kazi nyingi za kijamii huku ikizingatiwa kuwa Taifa tulikuwa bize ktk kujenga nchi, huku wengine tukihitajika zaidi katika maswala ya kitaifa ikiwemo swala la maridhiano, katiba Mpya, mfumuko wa bei ya bidhaa, kuifungua nchi na harakati za hapa na pale.

Basi nikamuomba msamaha Mama yangu mzazi kuwa kutokana na muda kubana basi nilipaswa niende mimi kumtembelea kijijini huko mkoani. Na kwakua nina muda mrefu sijaenda nikasema basi nimtumie nauli aweze kuja kwangu Mjini tuonane na kupiga stori za hapa na pale.

Basi mipango ikaanza kuwekwa sawa nikamjulisha Mke wangu kuwa Mama yangu mzazi atakuja muda ukifika kadiri atakavyoona yeye ataniambia tarehe na siku.

Mke wangu huyu akaniambia basi Nashukuru kwa taarifa hiyo na nipe kazi hiyo ni wajibu wangu niachie mimi nilishughulikie.

Nikasema sawa Mke wangu. Nilimwamini atalisimamia vema. Huwa haniangushi ktk mambo mengi makubwa na mazito.

Mambo ya ajabu aliyotenda dhidi ya Mama yangu yalikuwa ni haya.

1. Alisimamia safari yake kutoka kijijini hadi kufika mjini nilipo, safari ya takribani masaa 36. Huku mimi nikiwa bize aliweza kuwasiliana naye muda wote kuhakikisha anafika salama. Hapo alimtumia pesa zaidi kama pocket money na dharura mbali mbali asipate taabu njiani.

2. Mama yangu alionekana ni mtu wa furaha muda woote akiwa kwangu. Niliporudi usiku alipenda sana lazima tuonane na kusalimiana.

3. Mama yangu alinambia tangu amefika kwangu ameanza kunenepa na kusahau shida na tabu za tangu awali tukiwa kijijini akihangaika kutulea kwa shida


4. Mama yangu alinambia hajawahi kutembea sehemu yoyote na kupewa heshima kama aliyopewa akiwa nyumbani kwangu.

6. Mama yangu alinambia tangu yeye anakuwa na hadi sasa amekuwa mzee hajawahi kulalia mashuka meupe pee, mashuka safi ya kung'ara ambayo hubadilishwa kila siku na kuwekwa mengine.
Anaongeza kwa kusema alikuwa akitandikiwa Net ya Mbu safi kuhakikisha analala usingizi Fofofo. Usingizi usio na mawaaa!.

5. Mama yangu alinambia Mke wangu alikuwa akimpikia siku zote alizokuwepo nyumbani miezi mitatu asubuhi, Supu, chapati, juice, au maandazi na vingine mbali mbali.

7. Mama yangu alinambia Mke wangu akiwa anapika chakula akiwa bado anachemsha mboga let say Kuku au nyama au Samaki basi alikuwa anampakulia kidogo kwenye kibakuli aonje huku msosi wa nguvu ukiwa unaandaliwa.

Mama yangu alinisimulia haya tukiwa tumekaa kwenye kochi huku akicheka machozi ya furaha yakimtiririka, tukigongeshana mikono ya furahaa " Mwanagu rastaman mke wako amenirudisha utotoni" napakuliwa kibakuli cha supu nionje kabla hakijamaliziwa kupikwa, mbarikiwe sana na nyie watoto wenu wawafadhili kama mlivyonifanyia.

8. Jambo lingine Mama aliniambia alitendewa ni mavazi, baada ya kufika tu mjini alipumzika kama siku tatu akapelekwa shopping na kununuliwa mavazi mapya yote muhimu ya kike na ya Kama Mama.

9. Wakati tukiendelea mama alizidi kunifanulia kuwa ameweza kupata marafiki wapya mjini kwani hata inapotokea Harusi au Send off za Mashoga zake mke wangu basi Mke wangu alikuwa akimvalisha na kwenda naye kula bata huko za kike.

Mam yangu aliondoka kurudi nyumbani akiwa na zawadi kede kede na huku akijitazama miguu na mikono jinsi alivyo nawili na kuwa softi. Mama alinitania akisema mwanangu narudi nyumbani Baba yako ataniona Mpyaaa!! [emoji28][emoji28][emoji28]

Hivi ndivyo Mke wangu alivyoniwakilisha kuhakikisha Mama yangu anapata huduma Bora za kifamilia na kukirimiwa kama Mgeni Rasmi kipindi chote ambacho mimi nilikuwa bize na kazi zingine.

Sijutii kuwa katika Ndoa ya namna hii.

Ukiwa na Mke mwamini mpe nafasi ajitanue. Usimwingilie fanya yako afanye yake utafurahi mwenyewe.
Wanaume kweli tuna kazi, watoto mnawaalika mama zenu tu then sisi baba zenu mnatuacha vijijini...mnadhani sisi baba zenu hatupendi kunawili eeeh?

Nilijipinda kukusomesha, Kwa kujinyima sanaaa, ila wakati wa kula bata unamwita mama yako pekee, then mimi mumeniacha kijijini...[emoji34][emoji34][emoji34][emoji34]
 
Wanaume kweli tuna kazi, watoto mnawaalika mama zenu tu then sisi baba zenu mnatuacha vijijini...mnadhani sisi baba zenu hatupendi kunawili eeeh?

Nilijipinda kukusomesha, Kwa kujinyima sanaaa, ila wakati wa kula bata unamwita mama yako pekee, then mimi mumeniacha kijijini...[emoji34][emoji34][emoji34][emoji34]
Hehehe......najua umeandika utani. Lakini hii iwaendee wazee wa Kata ndoa ambao wao kazi yao ni Kuzaa watoto nje ya ndoa na kuwatekeleza. Harafu wakizeeka wanataka na wao waitwe mjini na Wanao.

Ukiwa mzazi hukumtunza mwanao kwa hali na mali usitegemee fadhila uzeeni
 
Hongera kwa kupata mke mwema.

Kabadilishe mazingira ya mama asije onea mjini vingine kama hivyo.

Asante kwa ku share.
Ni kweli mkuu ni hatua kwa hatua kwa kadiri Mungu atakavyotujalia
 
Wakuu wa ndoa mmekuja.kimkakati eeh?, any way mbona umeshangaa sana mkeo kumjali mama yako ina maana sio jambo la kawaida huko kwenye ndoa?.

Ila Bro mbadilishie mama yetu maisha hapo kijijini, sio fahari kumuacha mama anateseka kijijini kaka.
Tunaanza kidogo kidogo Kadiri ya uwezo. Insha Allah
 
😅😅
Nilimtumia mke wangu laki 2 wagawane laki laki na mama angu,wife akampa elfu 80 kakata 20 na wakati maza alikua anaenda hospital..ukibahatisha mke mwenye akiri kama wako ishi nae vizuri
👏👏👏ameen
 
Vizuri umejua wapi mkeo ana fit na umempa kazi ya kupaweka sawa...

Una babati mkuu japo mke wangu hana shida sana kwa wageni lakini Hawezi kufikia ukarimu wa mke wako..

Wenye bahati mtunze wake zenu vizuri maana hiyo ni tunu.
Na mimi najitahidi sana
 
Back
Top Bottom