- Thread starter
- #101
7yrsHongera...Ndoa ina muda gani mpaka sasa mkuu?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
7yrsHongera...Ndoa ina muda gani mpaka sasa mkuu?
Sasa nyie vijana endeleeni kukataa ndoa huku mkizaa nje na kutelekeza watoto harafu mkishazeeka mtegemee mtaletwa mjini.Vipi baba yako ?
Ulivyomwacha pekee yake kijijini na wewe utaachwa hivyohivyo
Na wanao
Muwe mnawachukua wazazi wote pamoja
Unyambizi sana hata usingeleta kisa hiki hapa
Kila mtu anafanya kwa uwezo na majaaliwa ya Mungu.Na uzee wote huo unamsafirisha saa 36? Kwanini haukumtumia ticket ya mwewe?
Hayana nafasiMbona habari ya kuchapiwa huleti?
😅😅😅😅Mimi nikajua jamaa anataka kuwapa promo wazee wa upinde wanaokataa ndoa.
Atakuja na yeye alibaki kutazama mifugo yake na mashambaMbona Dingi nae hakuja sasa?
Thanks. Bless to you too.Ni kama roho yangu imeingia kwa mkeo.
God bless her
Ni kweli Mtumishi haya yanatokea sana kwenye famili nyingi.Hongera kwa Mkeo lakini hongera zaidi ziende kwa Mama, hakika Mama yako ana Utu wa kupenda kukirimiwa na akakubali, kuna wamama wengine mtihani akiona maisha mazuri anaanza kuonesha wivu na choyo kwa mkeo yan ataona kama mkeo anafaidi maisha, ataanza kufanya visa, atakumbuka huko kijijini kuna binti wa shoga ake yupo tu atataka umuoe akiamini atafaidika zaidi yeye na shoga ake,
Atajisononesha, atakua mkali, hatothamini kila anachofanyiwa na mkeo, vurugu zitaanza, utaanza kumuona mkeo ndie mkorofi na kuhisi ana roho mbaya kwa mzazi wako, mkeo atachoka kuvumilia, ugomvi utazidi kua mkubwa hatimae mnaachana,
Utaletewa huyo mdada wa kijijini, baada ya kukaa kwa miezi mitatu watakuja kutembea mama ako na shoga ake ambaye wewe ni mkweo, mtu na mwanae wataanza kumnyanyasa mama ako, kwa aibu hatokwambia atavumilia, ataanza kukonda, utahisi mama anaumwa, mkeo atakwambia amemiss kwake, utamsafirisha yeye lakini shoga ake/mama mkwe wako atabaki, mkeo ataanza kukupanda kichwani, utakua unarudi usiku hawajapika lakini yeye na mama ake wamekula, ukihoji utaambulia maneno ya kashfa, utamkumbuka mke wako wa kwanza utaona kuna tofauti, utamtafuta atakujibu alishaolewa, utampigia simu mama yako na kulalamika, atakufungukia na kukuomba msamaha lilikua kosa lake, mkeo alimtendea mazuri lakini yeye hakuridhika, utakasirika, utamfukuza mkeo na mama yake kwako, utaishi maisha ya majuto, utaichukia ndoa na wanawake.
Sasa nyie vijana endeleeni kukataa ndoa huku mkizaa nje na kutelekeza watoto harafu mkishazeeka mtegemee mtaletwa mjini.
Lete kwanza wewe habari yako ya kuchapwa.Mbona habari ya kuchapiwa huleti?
Hongera sana chief kwa kupata 1 in million..maana wengine waliobaki huku kitaa wana roho ngumu na mbayaIlikuwa ni mwishoni mwa Mwaka jana 2022.
Basi kutokana na kazi nyingi za kijamii huku ikizingatiwa kuwa Taifa tulikuwa bize ktk kujenga nchi, huku wengine tukihitajika zaidi katika maswala ya kitaifa ikiwemo swala la maridhiano, katiba Mpya, mfumuko wa bei ya bidhaa, kuifungua nchi na harakati za hapa na pale.
Basi nikamuomba msamaha Mama yangu mzazi kuwa kutokana na muda kubana basi nilipaswa niende mimi kumtembelea kijijini huko mkoani. Na kwakua nina muda mrefu sijaenda nikasema basi nimtumie nauli aweze kuja kwangu Mjini tuonane na kupiga stori za hapa na pale.
Basi mipango ikaanza kuwekwa sawa nikamjulisha Mke wangu kuwa Mama yangu mzazi atakuja muda ukifika kadiri atakavyoona yeye ataniambia tarehe na siku.
Mke wangu huyu akaniambia basi Nashukuru kwa taarifa hiyo na nipe kazi hiyo ni wajibu wangu niachie mimi nilishughulikie.
Nikasema sawa Mke wangu. Nilimwamini atalisimamia vema. Huwa haniangushi katika mambo mengi makubwa na mazito.
Mambo ya ajabu aliyotenda dhidi ya Mama yangu yalikuwa ni haya.
1. Alisimamia safari yake kutoka kijijini hadi kufika mjini nilipo, safari ya takribani masaa 36. Huku mimi nikiwa bize aliweza kuwasiliana naye muda wote kuhakikisha anafika salama. Hapo alimtumia pesa zaidi kama pocket money na dharura mbali mbali asipate taabu njiani.
2. Mama yangu alionekana ni mtu wa furaha muda woote akiwa kwangu. Niliporudi usiku alipenda sana lazima tuonane na kusalimiana.
3. Mama yangu alinambia tangu amefika kwangu ameanza kunenepa na kusahau shida na tabu za tangu awali tukiwa kijijini akihangaika kutulea kwa shida
4. Mama yangu alinambia hajawahi kutembea sehemu yoyote na kupewa heshima kama aliyopewa akiwa nyumbani kwangu.
6. Mama yangu alinambia tangu yeye anakuwa na hadi sasa amekuwa mzee hajawahi kulalia mashuka meupe pee, mashuka safi ya kung'ara ambayo hubadilishwa kila siku na kuwekwa mengine.
Anaongeza kwa kusema alikuwa akitandikiwa Net ya Mbu safi kuhakikisha analala usingizi Fofofo. Usingizi usio na mawaaa!.
5. Mama yangu alinambia Mke wangu alikuwa akimpikia siku zote alizokuwepo nyumbani miezi mitatu asubuhi, Supu, chapati, juice, au maandazi na vingine mbali mbali.
7. Mama yangu alinambia Mke wangu akiwa anapika chakula akiwa bado anachemsha mboga let say Kuku au nyama au Samaki basi alikuwa anampakulia kidogo kwenye kibakuli aonje huku msosi wa nguvu ukiwa unaandaliwa.
Mama yangu alinisimulia haya tukiwa tumekaa kwenye kochi huku akicheka machozi ya furaha yakimtiririka, tukigongeshana mikono ya furahaa " Mwanagu rastaman mke wako amenirudisha utotoni" napakuliwa kibakuli cha supu nionje kabla hakijamaliziwa kupikwa, mbarikiwe sana na nyie watoto wenu wawafadhili kama mlivyonifanyia.
8. Jambo lingine Mama aliniambia alitendewa ni mavazi, baada ya kufika tu mjini alipumzika kama siku tatu akapelekwa shopping na kununuliwa mavazi mapya yote muhimu ya kike na ya Kama Mama.
9. Wakati tukiendelea mama alizidi kunifanulia kuwa ameweza kupata marafiki wapya mjini kwani hata inapotokea Harusi au Send off za Mashoga zake mke wangu basi Mke wangu alikuwa akimvalisha na kwenda naye kula bata huko za kike.
Mam yangu aliondoka kurudi nyumbani akiwa na zawadi kede kede na huku akijitazama miguu na mikono jinsi alivyo nawili na kuwa softi. Mama alinitania akisema mwanangu narudi nyumbani Baba yako ataniona Mpyaaa!! 😅😅😅
Hivi ndivyo Mke wangu alivyoniwakilisha kuhakikisha Mama yangu anapata huduma Bora za kifamilia na kukirimiwa kama Mgeni Rasmi kipindi chote ambacho mimi nilikuwa bize na kazi zingine.
Sijutii kuwa katika Ndoa ya namna hii.
Ukiwa na Mke mwamini mpe nafasi ajitanue. Usimwingilie fanya yako afanye yake utafurahi mwenyewe.
Asante sana aisee lakini mbona wapo wengi tu. Ni namna tu ya kujipanga sisi wanaume tunaweza kuamua wanawake zetu wa behave vipk na ikawa.Hongera sana chief kwa kupata 1 in million..maana wengine waliobaki huku kitaa wana roho ngumu na mbaya
😅😅😅😅kwani vina uhusiano?Siku mkeo huyo mwenye roho yake ajue unachepuka ndo mwisho wa ndoa.
😅😅😅Lete kwanza wewe habari yako ya kuchapwa.
😅😅😅wakataa ndoa mna msimamo mkali sana kama al-qaedaMpka uone ajabu mkeo kumfanyia mama yako utu ni kwamba kwa sasa ndoa zinatisha ,ndio maana umeona ajabu mama kufanyiwa wema na mkeo , kwa kizazi hiki cha sasa mke kumfanyia mama wa mume wema imekuwa ni muujigiza , kataa ndoa kwa sababu mke kumpenda mama yako ni kitu cha kubahatisha mno tena cha kushuhudia kwenye umati .