Mke wangu wa ndoa kapewa Mimba na mtu mwingine

Duh.....ndoa zina kazi sana!
 
Aisee pole sana kaka yangu, ila jiulize kama wewe je bado wampenda, na uko tayari kumsamehe na una uhakika gani kama hatorudia na ukizingatia bado waishi mbali na yeye?
 
Kapime DNA ya mtoto majibu nenda nayo kanisani kama ushahidi ili ndoa itenguliwe. Sio mwanamke huyo
 
Huyu mtoa mada kaniuzi hadi nataka kutapika hivi we kidume kweli?! Visa vyote upo tu!? Au ndio wale mnasomaa weee hamuonji kokote mkimaliza chuo baada ya kupata kazi mnaoa sasa unamuona mwanamke Kama maini yako yakotoka unakufa!! Ushauri wangu endelea nae na mtoto kambatize!!
 

ndugu yangu kimbia, ikiwezekana mpaka upoteze mguu hafai huyo!!!!!!!!!!!!!!! utajajuta.
 
kuoa ni kujiongezea matatizo. pole sana mkuu. mia

Mkuu sio kihivyo ... huyu Bwana ana behave very childish au Inocent? ... anafaa kuishi mbinguni na si hapa duniani ...seems to be very naive maybe?
 
Nafikiri hana watu wa kumshahuri vizuri, inavyoelekea huyo mkewe kakataliwa na jamaa aliyempa mimba sasa anajidai anarudisha majeshi. kama alishindwa kujizuia kwa mara ya kwanza ndiyo ataweza sasa ambapo huyu bwana bado yuko mbali nae? Trigger funguka macho yako kaka yangu hata biblia inaruhusu kumwacha mke mzinzi.
 

kaka fanyia kazi ushauri huu
 
Nathubutu kusema ulichagua kazi over ndoa yako. Ndoa sasa imekufa, eleza kama kazi nayo imekufa, wapi! Kazi iko palepale! Ulitakiwa kubalansi vitu hivi. Mlikuwa hamshauriani? Something was not right from the beggining! Kwa sala la ndoa kuvunjwa ili uoe tena linawezekana endapo ushahidi etc vitakuwepo. Nimeshuhudia ndoa mbili zimevunjwa tena mimba zimehusishwa. Mlolöngo ni mrefu pia. Uamuzi wako tu. Ila ukijaoa tena wajibika kiume, alaa!
 
Kama nafsi yako ilikutuma kumsamehe basi msamehe moja kwa moja. Nina jamaa yangu ilimtokea hiyo kitu alimsamehem mke wake mpaka leo wanaishi.
 
Jamaa lililotia mimba limesepa, demu akaona ajirudishe kwa bushoke wake, wewe bushoke hebu jitambue bana, piga chini dakika sifuri.
 
Anaomba ushauri kama anaweza kumuacha na kuoa mwingine kwa sababu alifunga ndoa ya kikristo
sasa kama alitakaushauri huo si aende kule alikofungia ndoa wamshauri?...kweli wanaume wengine mna roho ngumu...binafsi nikisikia ana cheat tu napiga chini sembuse kuzaa mtoto kabisa! halafu unakuja kutuomba ushauri nini cha kufanya.....mi nakushauri uendelee nae maana huna guts za kumuacha!
 
Duh Wewe kweli ni mshamba wa mapenzi....Kuna kuomba ushauri hapo? Upi tena?...Basi endelea naye kaka.
 
hivi ww unakaa mwaka mzima hujaonana na mke wako unategemea nin? Acha wakutombee ili ujue maana ya ndoa alah, kama n kaz ulishindwa kumhamishia huko uliko au na ww una mke huko?
 
Halafu ni mtoto wa kwanza. Aaah, mimi siwezi kabisa, yaani bora hata angekuwa wa pili au wa tatu, yaani tumbo la mkeo limefunguliwa na kunguru mwitu ilihali wewe ndiyo uliyeoa kwa harusi kanisani? Hata ingekuwaje siwezi kuishi naye.

Lakini wewe sikiliza moyo wako, kama uliweza kwenda kwake ukashuhudia hali aliyonayo na bado ukaendelea kupiga naye story, basi una moyo wa ajabu sijawahi kuona. Kuna akina siye hapa ungekuwa ndiyo mwisho wa mawasiliano.

Habari ya kufunga ndoa nyingine kwangu haina msingi sana, ndoa tunafunga ili kulifurahisha kanisa tu, biblia haijasema popote kwamba ufunge ndoa. Na zaidi ya yote, mbinguni hakuna kuoana, hata ungeoa wake kumi, siku ya hukumu hutaulizwa ni yupi alikuwa mke wako.

Piga chini, tafuta anayekufaa, endelea na maisha bila kujali kanisa linasema nini. Maisha ni yako binafsi, siyo ya kanisa wala ya wachungaji au majirani. Na siku ya hukumu hutasimama na yeyote kati ya hao. Wakati mwingine usiwasikilize sana wachungaji, jisomee biblia mwenyewe, halafu ujipe amani ya moyo, bila kujali wengine wanakutazamaje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…