Mke - Waziri Mkuu anahitajika kuisimamia serikali vema

Mke - Waziri Mkuu anahitajika kuisimamia serikali vema

Next King

Member
Joined
Dec 30, 2023
Posts
32
Reaction score
70
Wanawake wa JF,

Husika na mada tajwa hapo juu.

Waziri Mkuu anahitajika kwa minajili ya kuisimamia serikali ili kuleta amani, upendo, furaha na maendeleo ndani ya familia ambayo Mungu atatujalia kuanzisha pamoja.

Naomba ifahamike kuwa nchi yeyote Ile duniaini ili ifanikiwe inahitaji serikali imara inayosimamiwa kikamilifu na waziri Mkuu ambaye yupo imara.

Ukiwa kama mke wangu mtarajiwa na baadae mke wangu basi tambua wewe ndio msimamizi Mkuu wa idara zote za familia, na Mimi kama mume nitatekeleza yale yote yanayonihusu kama Mkuu wa nchi.

SIFA ZA WAZIRI MKUU (MKE )
  • Awe na hofu ya Mungu
  • Awe na hekima na kujitambua
  • Awe na utayari wa kuwa waziri Mkuu na kusimama kama mama na pia msimamizi wa mambo yote ya maendeleo ya familia
  • Umri miaka 28 hadi 35
  • Awe na elimu kuanzia kidato Cha nne na kuendelea
  • Awe tayari KUPIMA HIV

Sifa zangu
Elimu ya chuo
Muajiriwa - Nina kibarua public sector
Umri wangu ni 38
Nina hofu ya Mungu
Mpenda maendeleo na muwajibikaji
Nipo tayari kuwa na familia.

KARIBU MWENYE UHITAJI KAMA WANGU.
ASANTE 🙏🙏😘
 
Nilivyokuja mbio mbio nikajua braza kasimu anataka aniongeze mke wa pili😃😃..Anyways naona kigezo kimoja kinanikosesha mume
mimi ndo nikasema deal si ndo hili hapa nshatoboa wooooi
 
Umewasilisha vizuri, kila la heri. Hiyo age group iko poa, japo ungeanzia 28 hivi🤣, chap tafuta PM kabla hujafika 40 mkuu.
 
Raisi anatafuta waziri mkuu, baadae akitokea MAKAMU WA raisi(mchepuko) wa kumsaidia raisis usilalamike mzee. 😂
 
Naomba Nafasi ya bodyguard kwa Waziri mkuu,mheshimiwa Rais.

Ahsante.
 
PM anateuliwa kisha anathibitishwa, hakuna kutangazwa kwenye gazeti la serikali.
 
Back
Top Bottom