Mke - Waziri Mkuu anahitajika kuisimamia serikali vema

Mke - Waziri Mkuu anahitajika kuisimamia serikali vema

Wanawake wa JF,

Husika na mada tajwa hapo juu.

Waziri Mkuu anahitajika kwa minajili ya kuisimamia serikali ili kuleta amani, upendo, furaha na maendeleo ndani ya familia ambayo Mungu atatujalia kuanzisha pamoja.

Naomba ifahamike kuwa nchi yeyote Ile duniaini ili ifanikiwe inahitaji serikali imara inayosimamiwa kikamilifu na waziri Mkuu ambaye yupo imara.

Ukiwa kama mke wangu mtarajiwa na baadae mke wangu basi tambua wewe ndio msimamizi Mkuu wa idara zote za familia, na Mimi kama mume nitatekeleza yale yote yanayonihusu kama Mkuu wa nchi.

SIFA ZA WAZIRI MKUU (MKE )
  • Awe na hofu ya Mungu
  • Awe na hekima na kujitambua
  • Awe na utayari wa kuwa waziri Mkuu na kusimama kama mama na pia msimamizi wa mambo yote ya maendeleo ya familia
  • Umri miaka 28 hadi 35
  • Awe na elimu kuanzia kidato Cha nne na kuendelea
  • Awe tayari KUPIMA HIV

Sifa zangu
Elimu ya chuo
Muajiriwa - Nina kibarua public sector
Umri wangu ni 38
Nina hofu ya Mungu
Mpenda maendeleo na muwajibikaji
Nipo tayari kuwa na familia.

KARIBU MWENYE UHITAJI KAMA WANGU.
ASANTE 🙏🙏😘
Tatizo member mpya.
 
Mahii
Hiyo title nimeshtuka,, nikajiuliza ndo tunafunga mwaka na majukwaa ya siasa?

Rais atuwekee picha embu 😂 au achambur hicho kibarua cha public sekta. Wengine mahi tulishajiambia hatutaki wa hospitali
We unachagua mume kwa kuangalia picha / au potentialities aliyo nayo huyo mume wako tarajali? Come this way bana mie nimechoka upweke
 
Huh!! Nikajua ni uzi wa kutuchamba tena!!

Mkuu wewe hukuhudhuria kikao? Kikao kilikubaliana kukataa ndoa.
 
Huh!! Nikajua ni uzi wa kutuchamba tena!!

Mkuu wewe hukuhudhuria kikao? Kikao kilikubaliana kukataa ndoa.
Hahahah nilikuwa na udhuru siku hiyo hata hivyo napingana na wajumbe wa kikao🤣🤣
 
Back
Top Bottom