Mkeka wa Ma-DC umekaa poa. Muhimu wasisahau Jambo hili

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Nilikuwa napitia majina ya Ndugu zetu waliopewa nafasi za Ukuu WA wilaya. Kwa kweli mkeka upo vizuri Kwa sehemu kubwa

Nawapongeza wote Mliopewa Nafasi hizo. Pia nampongeza Mhe. Rais, Samia Suluhu Kwa kuweza kujitahidi kuwaona hawa.

Ila neno moja Kwa wateuliwa;

Achaneni na Yale mambo ya kujigeuza Miungu watu, ninyi ni. Watu Kama watu wengine. Tumikieni wananchi,

Mikwala na ubabe wa kipuuzi msije mkathubutu kujiingiza.

Maana awamu iliyopita kuna baadhi ya viongozi walijigeuza mabolizozo na kutoa matamko ya hovyo.

Heshima yenu haipo kwenye kutishia watu bali heshima yenu ipo katika kuwatumikia Wananchi.

Mjifunze Kwa Dada Jokate, au Mkuu wa Mkoa WA Dodoma, Anthony Mtaka.
Au mkishindwa huko basi jifunzeni Kwa Rais Samia Suluhu.

Ubolizozo na maneno ya ubabe wa ulimbukeni havitawajengea heshima isipokuwa chuki na vinyongo visivyo na maana yoyote.

Kuna Kaka yangu, Gondwe, nawe ujirekebishe, niliona baadhi ya Clip zako, ambazo ulikuwa ukifoka foka pasipo utulivu na usikivu.
Kiongozi ni pamoja na usikivu.
Showoff na Makamera meng alafu kazi kidunchu muziepuke.

Mhe. Rais nadhani na napendekeza aendelee kuteua watu wasio Wanafiki.

Mtu asiyeweza kukukosoa basi hawezi kukushauri

Ijenge nchi yako.
Kuwa mzalendo.
 
Sawa watakuwa wamesikia watambue nafasi walizopewa ni za muda wasije wakawa Kama Lengai.
 
Mtu anaongea na Mzee Kama mtoto mdogo kisa kacheo kake Ka Ukuu WA wilaya. Nilishangaa Sana

Wakati Rais mwenye na cheo chake hawezi kuthubutu
 
Hapo kwa GG umemuonea sana,wewe alikukaba kwenye dili zako
 
Kikubwa wakafanye kazi kwa weledi na kwa kufuata Sheria na katiba ya nchi.Kuonea watu Kama yule jambazi sabaya hapana wakaache.Pia wawasimamie wakurugenzi katika maeneo yao ipasavyo
 
Wateuliwa baadhi Yao watakuwa na Ari kubwa ya kufanya kazi kutokana na kutokuwa na mizizi mirefu ya ubeberu.
 
Mtoa mada hongera kwa kuwakumbusha wateuliwa!
1.Aliyewateua hapendi mambo ya kutafuta ",kiki"
2.Wateuliwa waache kulaumu watumishi kuwa ndio kikwazo cha matatizo yanayojitokeza katika maeneo yao ya utawala,bali wawe mstari wa mbele kutafuta ufumbuzi wa changamoto zilizopo.Maana Wakuu wengi sio wabunifu.
3.Wateuliwa wafuate sheria,kanuni na taratibu na wajue mipaka ya madaraka yao.
4.Wateuliwa wajifunze kujadiliana kushirikisha kabla ya kutoa maamuzi yenye kuathiri maisha ya mtu au kundi la watu.
 
Hao maDC kazi yao kubwa ni kuhakikisha ccm inasalia madarakani, sioni kama huwa wana jipya lolote.
 
Back
Top Bottom