Shughuli inakua pale wewe uchukue tahadhari ila majirani na wote waliokuzunguka wapo wapo tu hawana habari, kwa mfano kama una watoto, lazima kiaina kwa namna moja au nyingine watacheza na watoto wa majirani na inafahamika watoto ndio "super spreaders".
Kimsingi ni kuhubiriana tahadhari na pia serikali kulazimisha ikihitajika.
Hata kwetu huku kuna majitu yamejitoa ufahamu hayana habari, yaani mpaka akamatwe na polisi kwa kukosa kuvaa barakoa ndio anashtuka, anajitetea kama mtoto. Unakuta jitu linakohoa kohoa tu na halijavaa barakoa......hehehe!! Hiki kirusi kimetuhurumia Afrika maana duh kiukweli ule utabiri wa Waafrika kufa milioni haukua na makosa, ni kwamba kirusi hakina haja na vifo vya Waafrika.