Nafikiri Wabongo ndio mkae mjiulize maswali mengi sana kabla ya kushutumu. Nakuhakikishia ukiishi Kenya, utashangaa sana labda asilimia ndogo ya Wakenya ndio wanafuatilia mambo ya Watanzania. Haswa Wakenya waliowahi kuishi Tanzania, lakini wengine wote huwa hawana haja hata ya kujua nani rais wenu. Yaani hata ukiwa Mtanzania unapiga mishe zako Nairobi, hakuna Mkenya anashughuli na Utanzania wako, kila mtu anarauka alfajili kukimbizana na mishe zake.
Lakini kwa Watanzania, hilo ni tofauti, nyie siku zote mnaona kivuli cha Wakenya, kila mkihojiwa mnamwogopa nani, hamkawii kutaja Mkenya.
Mara nyingi sisi huwa tunaleta taarifa nzuri za kuhusu Kenya humu, lakini kwa jinsi mlivyojaa chuki, badala ya kutoa hongera mnaishia kutukana, na sisi tunajibu matusi yenu kwa dharau. Na tunaendelea hivyo miaka yote maana taratibu naona mnakua, kuna baadhi yenu mliishi kila siku humu JF Kenyan news mkitutusi, lakini siku hizi mumepungua na kuanza kuwa wastaarabu. Ina maana juhudi zetu zinafua dafu.
Ukiona mtu anakudharau, jiulize nini unachokifanya hadi iwe hivyo, hakuna Mkenya anayeweza kukurupuka na kukudharau bila sababu. Kuna Wabongo wengi wazuri wanaojiamini na nimefanya nao shughuli bila matatizo yoyote. Juzi nimekua pale Zanzibar, jamaa wapo wapo sawa sana, kichwa aisei na wana hekima sana na bidii, tumepiga nao shughuli za kikazi tena kwa heshima kubwa sana. Hatukua na Ukenya wala Utanzania, kila mtu anachangia ujuzi wake anavyoweza ili kufanikisha mradi.
Sasa wale niliwaona tofauti sana na kundi la Wabongo wengine nilifanya nao kazi fulani Dar hapo awali. Jamaa hawajiamini full, yaani kwenye vikao hawaongei, kimyaaaa, halafu baadaye wanalalamika ovyo. Hamna tofauti kati yao na nyie mliopo humu JF. Siku zote kuona Wakenya kama ndio vizuizi vyenu vya maendeleo.