Mkeo ana bodaboda wake?

Mkeo ana bodaboda wake?

Ukisikia mama au dada anakwambia ngoja nitamtuma 'bodaboda wangu' basi ujue huyo Bodaboda wake ni bodaboda wake kweli kweli.

Ninamjua mdada ambae anamtuma bodaboda wake kumtolea hela Kwa ATM. Kuna mmoja aliniletea bidhaa nikatakiwa nimrushie zaidi ya 300,000, nikamwambia makato upande wako. Akaniambia basi acha 'namtuma bodaboda wangu'.

Bodaboda anaweza kumsubiri mdada aoge amalize ndo ambebe. Cha kushangaza bodaboda hawa ni wakali mno kama wana deal na vidume. Hawataki kupotezewa muda na mahesabu ya gharama wanakuwa makini but kwa wadada watapigishwa round kibao malipo kiduchu lakini 'watiifu na waaminifu' kupita maelezo.

Achilia mbali wale boda wanaokunywa na wake zetu au kuwafata bar wakiwa hoi ili wawalete nyumbani wakati huo we umesafiri kikazi.

Hii connection ya wamama na wadada na bodaboda si ya mchezo.

Nawauliza Wana JF, mkeo ana bodaboda wake?
Wenyewe tumeshaelewa,
 
Mumeo/boyfriend unampa kadi ya ATM?
Hata password mume Hana, Hawa dada zetu na wake zetu, royalty kwa mwanaume ni kitu kikubwa Sana kwenye mahusiano kuliko hata sex, hawajui kiini kikubwa na mume kutokukujali ni pale anapoona royalty iliyotakiwa kuwa kwake imehamishiwa kwa mwanaume mwingine.
 
Yap hiyo nimeiona sana, unakuta demu kaja kwenye kijiwe cha bodaboda kasimama takriban lisaa lizima anamsubiria bodaboda wake.

Mi nikamuuliza kwani huyo jamaa huwa anakubebaga bure? Kwanini usichukue hizi za hapa uwahi kuliko kuendelea kumsubiria huyo huoni kua unazidi kuchelewa

Akasema "Aah nimemzoea tu naogopa kubadilisha bodaboda mwingine naona anaweza niangusha maana huyu nimemzoea hakimbizi sana"
m mwenye nna jirani yangu analiwa na bodaboda na mme wake ni mwalimu mpaka mwalimu kuja kushtuka ameshaliwa sana,popote atakapoenda lazma amwite bodaboda wake
 
Kuna jamaa kamnunulia mkewe gari mbili
Still mmama gari hatumii
Kazi kumtuma boda Tu..
Na akilewa usiku bar boda ndo anamfata
Jamaa yupo nje ya nchi
Mhhhh!!!, huyo boda atakuwa anamfukunyua huyo mwanamke kwa raha zote.
 
Boda boda wangu ninae nampa ATM kadi anatoa hela kwa uaminifu wote, namtuma sokoni namtuma popote, kwa kifupi bodaboda wangu ni zaidi ya ndugu yangu.
Hata ukimwambia akusubiri uoge kwanza huwa anakusubiri [emoji2957],Tena anakaa Sebuleni huku macho ameelekeza chumbani kwako, nawe unapita mbele yake na kanga moja.Aisee Kweli bodaboda wako ni mtu safi sana [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi bodaboda WANGU[emoji1787] nilipewa namba na baby, sababu yeye alikuwa anaishi maeneo haya kabla yangu ila sasa hivi yeye akipiga simu inaweza isipokewe but mimi lazima apokee na hata kama kashalala anaamka. Huwa inamuuma sana.

All in all ni kijana mwaminifu sana japo sijafika level za kumpa ATM card mtu yeyote yule.
Haya, Mwaminifu eenhh??!!, Ngoja akupenyezee mhogo wake halafu uje urudi hapa ukimsifia kuwa anajua Mapenzi kuliko Baby wako.
 
Sasa ndio wanaume wajue wanawake wanapenda mtu anayewajali ,wanyenyekea na kuwaonyesha upendo kidogo tu.Utakuta mwanaume uliyenae hicho kitu hakipo wanafikiri akikupa hela au gari ndio mapenzi .Waume zetu wajitafakari sana
Unatema big G kwa karanga za kuonjeshwa, ukipata fahamu unajikuta tayari ushapotea.
 
Mkuu umeshawahi kukaa na madogo?
Nilikuwa na bodaboda kadhaa, kwahiyo walikuwa wakinizingua hesabu nawafuata kijiweni, nisipowakuta nakaa kuwasubiri, watu wangu walikuwa wanapaki vijiwe vitatu tofauti, Kwahiyo boda boda walikuwa wananiona kama mwana.
Anyway sijui wewe utaanzia wapi kupata stori?
Ila walikuwa wakijua nawasubiria na hesabu hawana hawatokei, ukipiga simu anakuambia nina abiria.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kwahiyo haya maelezo yako yanahusiana na boda boda kupendwa na mashoga? Khaaaaaah.
Mbna unajibu usicho ulizwa, uwiiiiih

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom