WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 963
- Thread starter
-
- #181
Mtazamo wangu ni kwamba, tumeumbwa tofauti. Ni tofauti hii inayofanya wanawake kupimwa vipimo vya kila aina kuliko wanaume. Na katika kupima huko ndio hayo mengine kama HIV huonekana.
Wanawake kutokana na maumbile yao wanashauriwa kufanyiwa uchunguzi kila mwaka (mambo ya pap smear nk). Wanaume hatuna hayo mambo. Tunapeta tu. Nyinyi kila mara inabidi mjishike shike matiti kuangalia viuvimbe vya kansa. Mna mambo mengi sana ya kiafya yanayosababisha muende kwa waganga kila mara.
Kwa hiyo siyo kwamba wanawake hujitolea tu kwa hiari yao mara mbili kwa mwaka kwa mfano, kwenda kupimwa strictly HIV. Hilo nakataa. Sitaki kabisa. Ni maumbile yenu yanayowafanya muende kupimwa pimwa mara kwa mara.
NB: Itakuwa vyema kama ukileta data zinazoonesha wanawake wasio waja wazito, wasio na matatizo mengine ya kiafya, wanaokwenda zahanati au hospitalini kwa nia na dhumuni moja tu la kupimwa virusi vya ukimwi ili kujua hali zao.
Imebidi nirembe post yako maana ina madoido mengi ( myths zaidi kuliko facts)
1. Red - kweli tuko tofauti na haina ubishi
2. Blue kuna half truths - huenda wanawake hujikuta wakienda kupimwa ujauzito na hata mambo mengine - ukiacha ujauzito ambao hautokei kila mara na kwa kila mwanamke ni kitu gani cha kimaumbile kitamfanya mwanamke apimwe HIV ukizingatia hicho ni kipimo cha hiari? huwezi kwenda for pap smear au mamography/sonography ukaishia kupima VVU!
3. Green - half truth - kwanza kutokana na scientific breakthroughs - vipimo hivi kwa sasa inashauriwa mwanamke afanye akishavuka 45 years ( peri-menopause stage na kuzaa keshaacha mara nyingi) na pia umri huu hata wanaume wanashauriwa wafanyiwe kipimo cha kuchunguza prostrate.Isitoshe ni wanawake wangapi katika population hufanya vipimo hivi kama routine/? ni idadi ndogo mno utashangaa.
4.Orange - mnajidanganya. Rejea 3. hapo juu.
5. Purple - wako wengi sana.. nilitoa mfano mmoja wa kanisani... kuna occassions mbalimbali hutumika kuhamasisha watu wapime eg seminars, mikutano nk - wanaojitokeza kwa wingi ni wanawake na watoto.( utasema watoto nao wana ishu gani? tena wengi ni wa kiume!)
6.Pink - imeshajibiwa kutoka na majibu 1-5. Isitoshe VCT siyo lazima ifanyike zahanati.
the bottomline - hapa hatubishani wala kulaumiana bali tunahamasishana tu... yanayojadiliwa hapa ni maoni . Mwisho wa siku ni mtu na maisha yake, mtu na mwili wake.