Mkeo/mpenzio afanyeje ukubali.....

Mkeo/mpenzio afanyeje ukubali.....

Mtazamo wangu ni kwamba, tumeumbwa tofauti. Ni tofauti hii inayofanya wanawake kupimwa vipimo vya kila aina kuliko wanaume. Na katika kupima huko ndio hayo mengine kama HIV huonekana.

Wanawake kutokana na maumbile yao wanashauriwa kufanyiwa uchunguzi kila mwaka (mambo ya pap smear nk). Wanaume hatuna hayo mambo. Tunapeta tu. Nyinyi kila mara inabidi mjishike shike matiti kuangalia viuvimbe vya kansa. Mna mambo mengi sana ya kiafya yanayosababisha muende kwa waganga kila mara.

Kwa hiyo siyo kwamba wanawake hujitolea tu kwa hiari yao mara mbili kwa mwaka kwa mfano, kwenda kupimwa strictly HIV. Hilo nakataa. Sitaki kabisa. Ni maumbile yenu yanayowafanya muende kupimwa pimwa mara kwa mara.

NB: Itakuwa vyema kama ukileta data zinazoonesha wanawake wasio waja wazito, wasio na matatizo mengine ya kiafya, wanaokwenda zahanati au hospitalini kwa nia na dhumuni moja tu la kupimwa virusi vya ukimwi ili kujua hali zao.

Imebidi nirembe post yako maana ina madoido mengi ( myths zaidi kuliko facts)
1. Red - kweli tuko tofauti na haina ubishi
2. Blue kuna half truths - huenda wanawake hujikuta wakienda kupimwa ujauzito na hata mambo mengine - ukiacha ujauzito ambao hautokei kila mara na kwa kila mwanamke ni kitu gani cha kimaumbile kitamfanya mwanamke apimwe HIV ukizingatia hicho ni kipimo cha hiari? huwezi kwenda for pap smear au mamography/sonography ukaishia kupima VVU!
3. Green - half truth - kwanza kutokana na scientific breakthroughs - vipimo hivi kwa sasa inashauriwa mwanamke afanye akishavuka 45 years ( peri-menopause stage na kuzaa keshaacha mara nyingi) na pia umri huu hata wanaume wanashauriwa wafanyiwe kipimo cha kuchunguza prostrate.Isitoshe ni wanawake wangapi katika population hufanya vipimo hivi kama routine/? ni idadi ndogo mno utashangaa.
4.Orange - mnajidanganya. Rejea 3. hapo juu.
5. Purple - wako wengi sana.. nilitoa mfano mmoja wa kanisani... kuna occassions mbalimbali hutumika kuhamasisha watu wapime eg seminars, mikutano nk - wanaojitokeza kwa wingi ni wanawake na watoto.( utasema watoto nao wana ishu gani? tena wengi ni wa kiume!)
6.Pink - imeshajibiwa kutoka na majibu 1-5. Isitoshe VCT siyo lazima ifanyike zahanati.

the bottomline - hapa hatubishani wala kulaumiana bali tunahamasishana tu... yanayojadiliwa hapa ni maoni . Mwisho wa siku ni mtu na maisha yake, mtu na mwili wake.
 
Imebidi nirembe post yako maana ina madoido mengi ( myths zaidi kuliko facts)

Myths? Haya...kwa mtazamo wako I guess

1. Red - kweli tuko tofauti na haina ubishi
Vizuri umekubali hili maana kuna wengine ving'ang'anizi wa kwamba eti tuko sawa! Amini usiamini wapo.

2. Blue kuna half truths - huenda wanawake hujikuta wakienda kupimwa ujauzito na hata mambo mengine - ukiacha ujauzito ambao hautokei kila mara na kwa kila mwanamke ni kitu gani cha kimaumbile kitamfanya mwanamke apimwe HIV ukizingatia hicho ni kipimo cha hiari?
Sikusema tofauti ya kimaumbile pekee inamfanya mwanamke apimwe HIV unless hili ni swali lako lililotokana na kile nilichokisema. Nilichosema ni kwamba mna (wanawake) mambo mengi ya kiafya yanayopelekea muende kwa waganga mara kwa mara zaidi ya wanaume. Mna irregular periods, vaginal discharge, yeast infection, matatizo ya ovaries yanayosababisha maumivu wakati wa hedhi, nk. Haya hupelekea nyinyi kwenda kwa daktari zaidi ya wanaume. Katika kwenda huko kwa waganga wakati mwingine waganga hushauri mtoe baadhi ya vipimo zaidi (ingawa ndio vingine vinaweza kuwa vya hiari) na wakati mwingine vipimo hivyo huwa ni bloodwork.

huwezi kwenda for pap smear au mamography/sonography ukaishia kupima VVU!
Hilo sikusema. Nilitoa tu mfano wa kiujumla wa mambo yanayopelekea nyinyi kwenda zaidi kwa waganga. Nimeshaishi na wanawake. Nayajua kwa kiasi kikubwa mambo yao. Ni mengi kwa mtazamo wangu.

3. Green - half truth - kwanza kutokana na scientific breakthroughs - vipimo hivi kwa sasa inashauriwa mwanamke afanye akishavuka 45 years ( peri-menopause stage na kuzaa keshaacha mara nyingi)
Okay...I'll give you that but at the same time opinion in the medical field tends to differ a lot. Kwa hiyo wewe unaweza ku cite source inayosema hivyo ulivyodai na mimi nikaja na ya kwangu inayodai nilivyosema.

na pia umri huu hata wanaume wanashauriwa wafanyiwe kipimo cha kuchunguza prostrate.
Hii ni kweli.

Isitoshe ni wanawake wangapi katika population hufanya vipimo hivi kama routine/? ni idadi ndogo mno utashangaa.
Mwaga takwimu kama unazo. Na pia nitashangaa kama idadi ni ndogo kwenye haya yasiyo makubwa halafu kwa wakati huo huo wakawa mstari wa mbele kupimwa Ukimwi kwa hiari yao. What the hell?


4.Orange - mnajidanganya. Rejea 3. hapo juu.
Hatujidanganyi kama unavyodhania. Wanaume hatuna mambo mengi kihivyo. Sikatai umuhimu wa medical check up. Nyinyi mnavyo vingi vya ku check up. Unabisha?


5. Purple - wako wengi sana.. nilitoa mfano mmoja wa kanisani... kuna occassions mbalimbali hutumika kuhamasisha watu wapime eg seminars, mikutano nk - wanaojitokeza kwa wingi ni wanawake na watoto.( utasema watoto nao wana ishu gani? tena wengi ni wa kiume!)
Wengi sana maana yake ndio nini? Mwaga takwimu dada. Broad generalities hazitoshi. Mambo ya "tena wengi ni wa kiume" hayahusiki. Wengi ni kumi? mia moja? mia mbili? elfu moja au laki moja?

6.Pink - imeshajibiwa kutoka na majibu 1-5. Isitoshe VCT siyo lazima ifanyike zahanati.
Sijaona majibu yoyote ya kutosha na kuridhisha zaidi ya broad generalities. Kwa vile tuko hapa kijiweni tu, I'll give you a pass on that one. Otherwise ningekubana kama nilivyokubana kuhusu mshahara wa $20,000. 00/ mwezi bongo. Unakumbuka hiyo? Lol....

the bottomline - hapa hatubishani wala kulaumiana bali tunahamasishana tu... yanayojadiliwa hapa ni maoni.
Kama lengo ni kuhamasishana basi nadhani ku pit kundi moja dhidi ya jingine sio njia nzuri kwa mtazamo wangu. Ukianza kusema wanawake tuko hivi na wanaume mko vile hutahamasisha wengi. Utazua mabishano na finger pointing. Kwa nini usihamasishe kwa kutoa wito kwa akina dada, kaka, mama, na baba na badala yake u single out wanaume tu? Toa hamasa kwa wote.

Mwisho wa siku ni mtu na maisha yake, mtu na mwili wake.
Kula tano. Hilo ndio neno.
 
Sioni sababu hata kidogo kwanini ukaamshe watu waliolala, ni bora waachwe walale mpaka siku watakapoamua kuamka wenyewe, yanini mtu ufe kwa wasiwasi?
mkuu hili swala sidhani kama ni binafsi na hapo ndio tunapokosea.

sawa huoni sababu ya kupima kwa vile unaogopa kufa kwa wasiwasi baada kujua kama unao sio? je unaonaje kwa wale waliokuwa nao na wanaogopa kupima kwahio hawajui na wanaendelea kuambukiza wengine? sasa hapa si tunapoteza watu wengi zaidi mkuu?

mie nadhani mtu ukishajua itasaidia kupunguza kuambukiza wengine kama unao na kama hauna utajikinga zaidi hili usiupate.lakini huu mchezo wakujifanya hatutaki kupima kwa vile tunaogopa tuta kufa kwa wasi wasi ndio linaongeza idadi ya waathirika na waliofariki mpaka leo duniani kote.
 
Halafu wewe mchumba Jumamosi mguu wako mguu wangu tunaenda Angaza kupima status yetu! sio tu kusema unaunga mkono hoja.
Hapo sasa ndipo unapokoseaga!
Mi kupima mpaka nione homa za mara kwa mara haziishi, mkanda wa jeshi unaibuka, harufu ya TB inaibuka........... Dalili zinajulikana kwanini nikapime kabla dalili haijajitokeza?
 
Hapo sasa ndipo unapokoseaga!
Mi kupima mpaka nione homa za mara kwa mara haziishi, mkanda wa jeshi unaibuka, harufu ya TB inaibuka........... Dalili zinajulikana kwanini nikapime kabla dalili haijajitokeza?
Mimi sina mengi ila jambo moja tu;
KAMA KWELI UNANIPENDA UTANILINDA.
 
Back
Top Bottom