Mkesha wa maombi JF kuinusuru Bandari yetu isiuzwe

Ngugu wana JF kama mnavyojua kesho ndio kesho, kama wabunge wataridhia mapendekezo ya Mkataba kati ya TZD na Dubai kuhusu ustawishaji wa bandari, maziwa etc. basi hiyo ndio rasilimali zetu hizo ndio hazitorudi tena mpaka mwisho wa ulimwengu huu.

Yaani miaka elfu moja baadae sisi tutakaojulikana kama mababu na mabibi wa karne ya 21 tutadharaulika na kulaumiwa sana na kizazi hicho kwa kutolinda rasilimali hii muhimu.

Kwa muktadha huo naomba kila mtu kwa imani ya dini yake aangushe maombi hapa mpaka Mungu atunusuru katika tanuru hili la moto lililowashwa na waarabu na kututumbukiza wa TZD.

Eeh Mwenyezi Mungu tunakuomba ikiwezekana kikombe hiki kituepuke. Amen
Mnashindwa kuingia Barabarani mnakomaa na mikesha? Wanawake nyie
 
Uzi wa wala Rushwa akina King Msukuma. Ume futwa
 
[emoji23] Kwakweli tukeshe tu Maana hi ni kama Nyani[emoji205] wanafurahia kifo cha Mkulima kuwa hatowabugudhi wakila Mahindi na wanasahau kesho yataisha na hakuna wa Kulima tena
 
Hahahahaaa!
Tulishindwa kuombea loliondo, serengeti, madini yetu, wanyama wetu, nk nk.
Ijekuwa bandari! Acha nchi iuzwe!
 
Leo ni mkesha amkaa
bila kumjua adui yako ni nani, hata ukikesha wakesha bure. Walivyopitisha Azimio la Zanzibar tuliwachekea. Mie nalala mana yawezekana nakesha bure. Mpaka nipate 10 hivi wanaemjua adui harisi, nitakesha nao.
 
Hahahahaaa!
Tulishindwa kuombea loliondo, serengeti, madini yetu, wanyama wetu, nk nk.
Ijekuwa bandari! Acha nchi iuzwe!
Azimio la Zanzibar! tafakari ndipo tulipojikwaa. Hapa ni mwendo wa DEAL
 
Azimio la Zanzibar! tafakari
Mkuu, hapo mi sina cha kutafakari!
Tuliambiwa kuna siku nchi itapigwa mnada. Tukamuona aliyetuambia ni mbaya akajiuzulu. Tuliambiwa hii nchi imeliwa sana, aliyetuambia akachukiwa kila mahali hata baada ya kifo chake!
Acha nchi ibinafsishwe! Hata kama rais akiwa putin sawa tu! Tuna nini sasa kilichobaki ambacho tunamiliki 100%?
Ilihali Hotel za kifahari, visiwa, viwanda, maduka makubwa nk, ni vya wawekezaji!
 
Ngugu wana JF kama mnavyojua kesho ndio kesho, kama wabunge wataridhia mapendekezo ya Mkataba kati ya TZD na Dubai kuhusu ustawishaji wa bandari, maziwa etc. basi hiyo ndio rasilimali zetu hizo ndio hazitorudi tena mpaka mwisho wa ulimwengu huu.

Yaani miaka elfu moja baadae sisi tutakaojulikana kama mababu na mabibi wa karne ya 21 tutadharaulika na kulaumiwa sana na kizazi hicho kwa kutolinda rasilimali hii muhimu.

Kwa muktadha huo naomba kila mtu kwa imani ya dini yake aangushe maombi hapa mpaka Mungu atunusuru katika tanuru hili la moto lililowashwa na waarabu na kututumbukiza wa TZD.

Eeh Mwenyezi Mungu tunakuomba ikiwezekana kikombe hiki kituepuke. Amen
The Broker! Unataka tukeshe tukiomba tuendelee kuwa mafukara!
 
Uzi wa wala Rushwa akina King Msukuma. Ume futwa
Hata Uzi wa kuwasihi viongozi wa dini kuandaa siku maalum kwa ajili ya kuliombea taifa kwa kuwasomea albadir na kugonga kengele mara3 kuashiria msiba na maombolezo dhidi ya wote waliohusika kwenye mkataba huu wa kuibinafsisha bandari. Uzi huo umefutwa
 
Mungu awajaalie wapate kansa ya utumbo wasile walichotudhulumu.
 
Ngugu wana JF kama mnavyojua kesho ndio kesho, kama wabunge wataridhia mapendekezo ya Mkataba kati ya TZD na Dubai kuhusu ustawishaji wa bandari, maziwa etc. basi hiyo ndio rasilimali zetu hizo ndio hazitorudi tena mpaka mwisho wa ulimwengu huu.

Yaani miaka elfu moja baadae sisi tutakaojulikana kama mababu na mabibi wa karne ya 21 tutadharaulika na kulaumiwa sana na kizazi hicho kwa kutolinda rasilimali hii muhimu.

Kwa muktadha huo naomba kila mtu kwa imani ya dini yake aangushe maombi hapa mpaka Mungu atunusuru katika tanuru hili la moto lililowashwa na waarabu na kututumbukiza wa TZD.

Eeh Mwenyezi Mungu tunakuomba ikiwezekana kikombe hiki kituepuke. Amen
Kichwa cha habari tu kinaonyesha uelewa mdogo wa mwandishi. Hakuna anayeuza bandari ni ukodishaji wenye lengo la kuboresha ufanisi.

Acheni hizi tafsiri potofu za kipuuzi, haziwasaidii chochote.
 
Back
Top Bottom