Mkiambiwa wahuni hawafai uongozi, yafaa kuelewa

Mkiambiwa wahuni hawafai uongozi, yafaa kuelewa

Kwanini wale Polepole kawaita wahuni hawafai uongozi nitatoa mfano wa Tanesco chini ya waziri wake kijana Januari.

Kuingia tu akaja na mipango kemkem Tanesco mmojawapo wa mipango ni huu wa kubadili mita za umeme kuweka za kisasa eti ukilipa tu sio tena unapewa token ukaingize mwenyewe kwenye mita. Ukisasa ni kwamba ukilipa tu mita yako moja kwa moja inajibu kwa kupokea na kuongeza units kwenye mita kiasi ulicholipia.

Mambo ya kujiuliza ni kwamba je, kuna ulazima kuleta mpango huo kwa sasa ukizingatia shirika la tanesco lilikua kwenye mkakati wa kujikwamua kutoka kupata hasara? Je, hiyo teknolojia ambayo pengine hata Ulaya bado ni mpya kuna haja ya nchi yetu kuikimbilia?

Halafu la msingi kubadili mita nchi nzima kwa bei ya hizo mita si itakua gharama kubwa sana kwa shirika linalopata hasara? Kwa ufupi wahuni wanakujaga na mipango ya upigaji tu. Hapa tulipo kimaendeleo teknolojia ya mita tuliyonayo inatosheleza kabisa. Hakuna sababu kuingiza shirika gharama kubwa kwa tamaa binafsi ya mtu.

Watakwambia mita zitabadilishwa taratibu lakini sio kweli maana wauzaji hadi ununue ndio upate chako cha juu. Kwa hivyo tutashuhudia ubadhirifu mita nzima zinang'olewa na kubafilishwa.

Huu ni mfano mmoja tu jinsi wahuni hawawezi kuleta maendeleo ya nchi ila kuleta maendeleo yao binafsi ili kujikita kudhibiti dola kwa faida yao.
Halafu kule bungeni yamejaa majitu fulani kazi yao kusifia tu ooh mama ameniletea kwangu bilioni....haijawahi kutokea!
 
Kali ni kubadilisha grid nzima ya Umeme ,yaani nyaya zote zinafumuluwa halafu zinafungwa nyengine mpya kwa trilion kadhaa swali la kujiuliza hizi nyaya za umeme huwa nazo zinachoka ?hapana bali kilichopo zimeungwa vibaya.kuungwa vibaya ndio tufumue grid yote,si palekebishwe palipoungwa vibaya.
Tusichoshane as long nakula na nalala salama .
 
Mnakoseaga sana kumuita Makamba Jr kijana wakati ana miaka 51. Mwigulu Nchemba ana 60 mnamuita kijana. Acheni hizo.

Hata Pascal Mayalla mtamuita kijana?
Makamba ni wa January 1974, Mwigulu pia ni wa 1974-75 hao wote bado vijana wameingia mapema katika mfumo, Wameanza kula kuku wakiwa na umri mdogo.
 
Hii serikali ni ya wapigaji.. sidhani kama hata barabara moja itajengwa kwa mtindo huu
 
Back
Top Bottom