Kuna mmoja alimpata mdada wa 30+ kanisani. Dada amesoma masters Makerere, ofisini ni head wa department, ana nyumba mbili, Ana mabanda manne ya kuku na kila banda Lina uwezo wa kuchukua kuku 500, ana hiaice mbili za kwenda Bagamoyo.
Kaka alijua amepata kitonga. Alimtamkia mimi ninataka kukuoa. Dada alilia kwa furaha. Kabla ya kuvakishwa pete, yule dada alimwambia hivi vyote ni vyangu. Nyumba zote nitapangisha mimi na wewe tukapange tuanze moja. Ukiwa kama mwanaume ninategemea utakua unachangia kodi kila mwezi.