Mkigombana atakae toka ndani ya nyumba ni nani?

Mkigombana atakae toka ndani ya nyumba ni nani?

Hivi vitu ndo sipatani navyo...

Bora nijenge nyumba sehemu nyingine hapo nifuge kuku na kuuza mayai...

Kitu chochote kinachoiba nguvu yako Kama baba/kichwa Cha familia Ni hatari kwa afya ya familia.

wanamke Wana dharau by nature, sasa dharau zinalipukaga from no where kama mwanaume Hana malengo,mvivu kufanya kazi na Hana msimamo,wanaume tucheze kote lakini lazima ujue familia inaelekea wapi sio unakaa kindezindezi tu bila focus...
 
Ila hili swala la wanawake kutuigizia mimi naona tunalitaka sisi wenyewe wanaume kwa sababu kwenye jamii yetu wanawake wanalazimishwa sana kuolewa mapema kuliko wanaume mwanamke akishafika miaka 30 na kuendelea hajaolewa utaona jamii inaanza kumnyooshea vidole kuwa ana mikosi, laana na kila aina ya kashfa lakini mwanaume hata afikishe miaka 50 hajaoa inaonekana ni kawaida na jamii haimshangai

Sasa kumbuka hakuna binadamu anayependa kuonekana ana mikosi au laana kwahiyo hapo ndipo wanawake wenye umri wa kuolewa wanapotafuta ndoa kwa nguvu wanafanyaje wanatusikiliza tu sisi wanaume tunavyojikuta vidume waendesha dunia tunatiririka humu mitandaoni na mitaani kuwa tunataka wanawake wazuri wapole wacha Mungu na wasioomba pesa

Na kumbuka kila binadamu ana mapungufu yake na dhambi zake na hauwezi kumlazimisha mtu abadilike anabadilika pale anapotaka mwenyewe na umri wa wanawake wengi kuolewa unakuwa ni umri wa ujana wanakuwa hawako tayari kubadilika kwa muda huo na hatuwezi kuwalaumu maana wao nao ni binadamu siyo malaika

Kwahiyo kwa sababu wanataka kuolewa na wanaume tumeshataja sifa za wanawake tunaowataka na wao hawana hizo sifa wanaamua kutuigizia mapenzi na maisha ili wapate kuolewa jamii isiwadharau ndo maana siku hizi unasikia wanaume wengi kwenye ndoa wanalalamika eti oh mimi mke wangu kwenye uchumba alikuwa wife material ila baada ya kumuoa tu kajisahau sana siyo kajisahau ni sababu kwenye uchumba aliigiza hakufanya kwa utayari alifanya tu ili aolewe ili jamii isimshangae sasa kashaolewa aendelee kufanya hivyo ili iweje?

Kwahiyo hapa swala siyo kuigiza swala ni kwamba kwanza jamii iache kuwadharau na kuwanyooshea vidole wanawake waliochelewa kuolewa maana ndoa anapanga Mungu hii itawafanya na wao wasiwe na papara ya kuolewa hadi pale watakapokuwa tayari kuwa wake wema pili wanaume tuache kutaja sifa za wanawake tunaotaka kuwaoa kama vile tunataja sifa za malaika wakati sisi wanaume tu wenyewe mara nyingi tunakuwaga hatuna na hatutaki kuwa na hizo sifa tunazotaka wake zetu wawe nazo

Wanaume wengi tunataka wanawake wakamilifu wasio na mapungufu hata kidogo eti kisa hatutaki kuvurugwa sasa mwanamke wa hivyo hayupo hapa duniani labda umuumbe mwenyewe wote kila mtu ana mapungufu yake na dhambi zake sisi tunakuwa na expectations kubwa sana kwamba eti sifa zote ulizoweka wewe asikose hata moja akikosa hata moja basi hafai mwisho wa siku unakuwa malaya wa kutupa jamani tukumbuke kuwa hawa nao ni binadamu na mapenzi yanajengwa kutokana na mapungufu kama ambavyo wao wanatukubali sisi pamoja na mapungufu yetu na sisi pia hivyo hivyo tuwakubali wao pamoja na mapungufu yao mbaya zaidi unakuta hata mwanaume asiye mume wema muhuni naye anataka mke mwema mpole jamani kuwa mkamilifu siyo rahisi kama Mungu tu anatuelewa binadamu wote kwamba siyo wakamilifu ndo maana anatusamehe dhambi zetu sasa sijui kwanini wanaume hatutaki kuwaelewa wanawake kuwa nao siyo wakamilifu halafu mbaya zaidi sisi tunataka wao watuelewe na watukubali hivi hivi tulivyo ni ngumu kwa kweli na ndoa zitaendelea kuwa na majanga na tutaendelea kulalamika kila siku kwa sababu ya kutotaka kubadilisha hii mitazamo yetu hasi juu ya wanawake
Enzi za ukoloni ukifisha miaka 12.kama unavutia na umeshamaliza darasa la nne unaolewa. Ukifisha miaka 16 nyumbani wazazi wanaanza kuwa na wasiwasi
 
Enzi za ukoloni ukifisha miaka 12.kama unavutia na umeshamaliza darasa la nne unaolewa. Ukifisha miaka 16 nyumbani wazazi wanaanza kuwa na wasiwasi


Wewe ulifukuzwa kwenu (kwa wazazi wako) ukiwa na miaka mingapi?
 
Alafu miaka ya sikuhizi sijui nini kimetokea,wanawake wengi wamekuwa wakipata ridhki sana kuliko wanaume.
 
Umekutana na binti mjini Dar, binti huyu wazazi wake ni wanasiasa tangu enzi za chama kushika hatamu. Wana eneo la heka tano na zimezungushiwa uzio.

Mapenzi yenu yameiva mpaka mnaona. Siku ya harusi mbele ya wageni Baba mkwe kwenye hotuba yake anawapa kiwanja ndani ya eneo lake, kwa tambo anasema wajukuu zake wasizaliwe kwenye nyumba ya kupanga.

Baada ya honeymoon mmepewa guest wing muanzie maisha wakati mnajenga. Mmejenga nyumba imekwisha na mmehamia.

Mmekorofishana kidogo na mke, hali halisi ni kuwa wote mna hasira mmoja wenu inabidi aondoke kwa muda. Kati ya wewe na mke wako ataondoka nani?
Mke
 
Umekutana na binti mjini Dar, binti huyu wazazi wake ni wanasiasa tangu enzi za chama kushika hatamu. Wana eneo la heka tano na zimezungushiwa uzio.

Mapenzi yenu yameiva mpaka mnaona. Siku ya harusi mbele ya wageni Baba mkwe kwenye hotuba yake anawapa kiwanja ndani ya eneo lake, kwa tambo anasema wajukuu zake wasizaliwe kwenye nyumba ya kupanga.

Baada ya honeymoon mmepewa guest wing muanzie maisha wakati mnajenga. Mmejenga nyumba imekwisha na mmehamia.

Mmekorofishana kidogo na mke, hali halisi ni kuwa wote mna hasira mmoja wenu inabidi aondoke kwa muda. Kati ya wewe na mke wako ataondoka nani?
Mume ndiye anatakiwa aondoke, mke aondoke nyumbani aende wapi na watoto?
 
Back
Top Bottom