Mkiwaona CDF, IGP na DGIS, kwenye utoajii wa hiyo ripoti ya Chande, mjue hakuna uwajibikaji

Mkiwaona CDF, IGP na DGIS, kwenye utoajii wa hiyo ripoti ya Chande, mjue hakuna uwajibikaji

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,828
Reaction score
165,667
Binafsi naamini teyari kuna watu wanajua kilichopo kwenye hiyo ripoti ya Jaji Chande wakiwemo watuhumiwa wakuu wa mauaji ya Oktoba 29.

Kwahiyo, kama nilivyoeleza kwenye kichwa cha habari cha huu uzi, mkiwaona hao niliowataja wamehudhuria hilo tukio la utoaji wa hiyo ripoti, mjue tu watu hao watasafishwa na hakuna hata mmoja wao ataewajibika kutokana na nafasi yake.

Kama mtu anaiba kuku anatumikia kifungo, iweje watuhumiwa wa mauji ya mamia ya watanzania wasamehewe huku ushahidi wa kimazingira unaonyesha kuwa kazi yao walifanya kwa namna ambayo sio sahihi?

Watanzania tuipinge kwa nguvu ripoti hii na sasa tuwaombe ICC waanze kazi yao.

Imetosha.
 
Back
Top Bottom