Mkiwapima wanafunzi mimba pimeni na bikra mjue walioanza ngono ni kiasi gani

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Kuna mjadala mzito unaoendelea katika jamii—mjadala unaogusa utu, haki, na mustakabali wa watoto wa kike mashuleni. Ingawa kuna wakati watu huingiza siasa ila ni jambo nyeti sana katika jamii.
images - 2026-03-23T222210.296.jpeg

Kwa miaka ya hivi karibuni, imekuwa jambo la kawaida kwa baadhi ya shule kufanya vipimo vya ujauzito kwa wanafunzi wa kike kama sehemu ya udhibiti wa nidhamu na kulinda mustakabali wao wa elimu. Zoezi hili, mara nyingi la kushtukiza, limepongezwa na baadhi ya wadau kwa kusaidia kugundua mimba mapema na hata kufanikisha hatua za kisheria dhidi ya wahusika.
images - 2026-03-23T222218.744.jpeg

Hata hivyo, nyuma ya zoezi hili kuna swali gumu lisilopewa majibu linalostahili: Je, tunashughulikia tatizo au dalili zake? Wakati shule zikijikita kubaini ujauzito, ukweli mchungu unabaki kuwa maisha ya mahusiano kwa wanafunzi haswa wa kike yanaanza mapema zaidi kuliko inavyodhaniwa.
images - 2026-03-23T222230.572.jpeg

Hizi likizo wakiwa majumbani na mitaani kuna mambo ya ajabu sana yanatokea na jamii inachekacheka tu tukisubiria kusikia mtoto wa mzee fulani kapewa mimba. Mtaa mzima unafahamu kuwa mdada Y ana wanaume wanne, wawili ni bodaboda, mwingine fundi gereji na mmoja ni kondakta, jamii inajua kabsa dogo akitoka shule analiwa halafu mnasubiri apate mimba muanze kuwatafuta wadau?
images - 2026-03-23T222307.734.jpeg

Hoja ya kupima bikira imekuwa ikijitokeza mara kwa mara, ikizua hisia kali pande zote. Wapo wanaoona ni njia ya kudhibiti mienendo ya wanafunzi na kuzuia madhara ya mapema, huku wengine wakiona ni uvunjifu mkubwa wa haki za binaadamu na faragha. Kupima mimba sio uvunjifu wa haki za binadamu ila kufahamu kama binti ameanza kushiriki ngono ni uvunjifu wa haki za binadamu? Itabidi nirejee darasani nikasome tena LW 628, DS 111 pamoja na PL 321.
images - 2026-03-23T222317.684.jpeg

Kama jamii tunapaswa kuangazia zaidi mizizi ya tatizo: elimu duni ya afya ya uzazi, ukosefu wa mazungumzo ya wazi kati ya wazazi na watoto, pamoja na ushawishi wa mitandao na mazingira yanayowazunguka vijana. Sio utimamu kumuona Mtoto wa kike wa shule fulani akiwa Bundesliga anakula bata mpaka saa 9 ukatulia kimya mpaka umuone yupo na tumbo kubwa.
images - 2026-03-23T222337.946.jpeg

Ni rahisi kushangaa pale mwanafunzi wa kidato cha kwanza anapobainika kuwa tayari ameshaanza kufanya ngono. Lakini je, tumewahi kujiuliza ni nani aliyemfundisha? Anafanya na nani? Ni nani aliyemlinda au kushindwa kumlinda? Je bikra yake imetolewa na nani? MASWALI MAGUMU YANAHITAJI MAJIBU!
images - 2026-03-23T222218.744.jpeg

Umewahi kujiuliza sisi kama wazazi na walezi ni watoto wangapi wa kike ambao wapo kidato cha pili tatu au hata kidato cha nne ambao tayari ni Mabrigedia, majenerali na Luteni Kanali kwenye ngono na zinaa? tunawatazama na kufurahi tukiwaona wakiwa wanagawa utamu mitaani ila wakibeba ujauzito tunaanza kujadiliana kuwa amekatishwa ndoto zake? Mara uvunjifu wa haki za binadamu!
images - 2026-03-23T222210.296.jpeg

Tukubali au tukatae katika zama hizi, kulinda ndoto za mtoto wa kike kunahitaji zaidi ya akili kubwa sana. Tutaishia kupima mimba za wanafunzi 300 tukapata wenye mimba ni 10 halafu wanafunzi 290 hawana bikra na sehemu za siri zimetumika kuzidi makahaba.
 
Sasa mzazi anafanya kazi gani kama mpaka bikra mnataka zipimwe na Mwal.?.

Kila mzazi achunge binti yake, msitwishe mzigo waalimu
 
hivyo vikatuni vimenikumbusha mbaliiii enzi za Fema🤗,,.nilikua napenda kukimbilia kurasa za katikati nisome story,, sijui saivi bado yapo
 
Hiyo kazi itafanywa na wazazi wao, ww wapime mimba mana inaathiri masomo moja kwa moja
 
Kuna mjadala mzito unaoendelea katika jamii—mjadala unaogusa utu, haki, na mustakabali wa watoto wa kike mashuleni. Ingawa kuna wakati watu huingiza siasa ila ni jambo nyeti sana katika jamii.
View attachment 3561876
Kwa miaka ya hivi karibuni, imekuwa jambo la kawaida kwa baadhi ya shule kufanya vipimo vya ujauzito kwa wanafunzi wa kike kama sehemu ya udhibiti wa nidhamu na kulinda mustakabali wao wa elimu. Zoezi hili, mara nyingi la kushtukiza, limepongezwa na baadhi ya wadau kwa kusaidia kugundua mimba mapema na hata kufanikisha hatua za kisheria dhidi ya wahusika.
View attachment 3561877
Hata hivyo, nyuma ya zoezi hili kuna swali gumu lisilopewa majibu linalostahili: Je, tunashughulikia tatizo au dalili zake? Wakati shule zikijikita kubaini ujauzito, ukweli mchungu unabaki kuwa maisha ya mahusiano kwa wanafunzi haswa wa kike yanaanza mapema zaidi kuliko inavyodhaniwa.
View attachment 3561878
Hizi likizo wakiwa majumbani na mitaani kuna mambo ya ajabu sana yanatokea na jamii inachekacheka tu tukisubiria kusikia mtoto wa mzee fulani kapewa mimba. Mtaa mzima unafahamu kuwa mdada Y ana wanaume wanne, wawili ni bodaboda, mwingine fundi gereji na mmoja ni kondakta, jamii inajua kabsa dogo akitoka shule analiwa halafu mnasubiri apate mimba muanze kuwatafuta wadau?
View attachment 3561879
Hoja ya kupima bikira imekuwa ikijitokeza mara kwa mara, ikizua hisia kali pande zote. Wapo wanaoona ni njia ya kudhibiti mienendo ya wanafunzi na kuzuia madhara ya mapema, huku wengine wakiona ni uvunjifu mkubwa wa haki za binaadamu na faragha. Kupima mimba sio uvunjifu wa haki za binadamu ila kufahamu kama binti ameanza kushiriki ngono ni uvunjifu wa haki za binadamu? Itabidi nirejee darasani nikasome tena LW 628, DS 111 pamoja na PL 321.
View attachment 3561880
Kama jamii tunapaswa kuangazia zaidi mizizi ya tatizo: elimu duni ya afya ya uzazi, ukosefu wa mazungumzo ya wazi kati ya wazazi na watoto, pamoja na ushawishi wa mitandao na mazingira yanayowazunguka vijana. Sio utimamu kumuona Mtoto wa kike wa shule fulani akiwa Bundesliga anakula bata mpaka saa 9 ukatulia kimya mpaka umuone yupo na tumbo kubwa.
View attachment 3561881
Ni rahisi kushangaa pale mwanafunzi wa kidato cha kwanza anapobainika kuwa tayari ameshaanza kufanya ngono. Lakini je, tumewahi kujiuliza ni nani aliyemfundisha? Anafanya na nani? Ni nani aliyemlinda au kushindwa kumlinda? Je bikra yake imetolewa na nani? MASWALI MAGUMU YANAHITAJI MAJIBU!
View attachment 3561877
Umewahi kujiuliza sisi kama wazazi na walezi ni watoto wangapi wa kike ambao wapo kidato cha pili tatu au hata kidato cha nne ambao tayari ni Mabrigedia, majenerali na Luteni Kanali kwenye ngono na zinaa? tunawatazama na kufurahi tukiwaona wakiwa wanagawa utamu mitaani ila wakibeba ujauzito tunaanza kujadiliana kuwa amekatishwa ndoto zake? Mara uvunjifu wa haki za binadamu!
View attachment 3561876
Tukubali au tukatae katika zama hizi, kulinda ndoto za mtoto wa kike kunahitaji zaidi ya akili kubwa sana. Tutaishia kupima mimba za wanafunzi 300 tukapata wenye mimba ni 10 halafu wanafunzi 290 hawana bikra na sehemu za siri zimetumika kuzidi makahaba.
mpaka kupimwa mimba maana yake kuna mgogoro possibly wa kisheria. maana yake uthibitisho ni mimba na si mwaka ambao bikra yake ilitolewa. Ukimpa mimba mwanafunzi uthibitisho ni mimba.
 
ile mvua ya miaka 30 haiwezekani kugawana pasu kwa pasu?
 
Nikupe pongeza kwa bandiko zuri lenye kutoa tahadhari kwa wazazi na kufumbua macho jamii

Hata hivyo, unatakiwa ujipe home work tena ya kuchimba zaidi ili ujue kama siku hizi hata hizo mimba zenyewe zinapimwa? achilia mbali hizo bikra.

Nimeona umeandika eti "siku za hivi karibuni" ukimaanisha shule zinapima mimba wanafunzi wao wa kike kwa kushitukiza. Hili lifanyie home work tena

Kilichopo kwa sasa, kuna haya makundi yenye jina maarufu "watetezi wa haki za binadamu" wako radhi wale sahani moja na wewe mpaka ukome endapo watasikia au kupata tetesi kuwa shule X Mkuu wake wa shule ameamuru watoto wa kike wapimwe mimba kwa kushitukiza bila ridhaa ya wazazi wa wanafunzi husika

Wao wanaita huo ni unyanyasaji kwa watoto wa kike.

Hii imewatia ganzi wakuu wengi wa shule hasa hizi shule za serikali ambazo kwa asilimia kubwa ndizo zinazobeba watoto wengi wenye changamoto za kimalezi kwani ni kama serikali nayo iko upande wa haya makundi

Siku hizi kuna rate kubwa sana ya watoto wa kike wa shule kutoa mimba katika umri mdogo kwasababu hakuna anayejishughulisha nao. Wakishajigundua option yao ya kwanza ni kwenda kuitoa kwasababu hakuna anayejua kuwa ana mimba na itabaki siri yake na wachache waliojua.

Angalau zamani walipokuwa wanapimwa na kugundulika mapema hata utoaji wake ulikuwa mgumu kwasababu tayari wazazi wanajua na walimu wanajua, hivyo ilikuwa vigumu kutoa mimba baada ya kugundulika kwasababu kila mmoja atajua

Ili shule ipime mimba siku hizi (hasa hizi za serikali), kwanza lazima wawe wamemtilia mashaka mtoto, pili lazima waambatane na mzazi wa mtoto na mzazi aridhie vinginevyo akipaza sauti yeye ndio atasikilizwa
 
Back
Top Bottom