Mkoa gani hata ukipewa nyumba na gari hauwezi kuishi?

Mkoa gani hata ukipewa nyumba na gari hauwezi kuishi?

Hivi huyo unaemkaripia umeelewa alichokiandika kweli?au una hangover ya k vant?
Nimemuelewa vyema kuliko unavyofikiria wewe kwanza mimi situmii kinywaji chochote cha kilevi.Sio vyema kutaka kulamisha mawazo yako yafanane na mwingine.Huwezi kandia sehemu ambapo watu wanavuta pumzi na wako ambao ukiwaambia wahame Dodoma hata uwapige bunduki hawakubali
 
Wakuu habari za weekend. Bila shaka ni shwari kabisa,

Kuna kitu nimewaza kuhusiana na harakati za utafutaji maisha na utulivu wa familia.

Niende kwenye maada husika mi nimebahatika kuishi baadhi ya mikoa hapa TZ bara na visiwani Pemba na Unguja nimeishi zaidi ya miaka 6 huko ukija bara Dar, Tanga, Atown, Tabora, Dom, Moro, Pwani, Shinyanga, Mwanza, Kilimanjaro, Sgd, kwa kuna Mkoa ambao hata nikipewa nyumba na gari siwezi kuishi ni Dodoma.

Yaani huo mkoa umekaa tofauti kabisa na sehemu nyingi nilizo ishi kuanzia kiuchumi, kijamii, kwa wale watumishi waliolenga kustaafia na kuishi huko hakika waishia kupauka na kunywa za pombe za kienyeji maana sioni future endelevu kabisa kwenye huo mjini na miongoni mwa miji yenye asili ya njaa uvivu na ukame kuna miji kama Tanga Moro au hata Mwanza unaweza ishi na familia bila tatizo tofauti huo mji wa Dodoma ambao wakazi wake wamekimbilia Dar na shughuli zao kwenye machinjio ya wanyama huko Vingunguti, Pugu na biashara ya Bucha

Ni wazi tunapambana na kwa ajili ya kujiandalia maisha bora ya sasa na baadae kwako na vizazi vyako hakikisha haukosei wewe pamoja na kukiweka kizazi chako jangwani kitateseka chagua sehemu sahihi ambayo itakufanya uishi kwa furaha. Kizazi chako ukikiweka jangwani kitashindwa kukusaidia hata wewe mzazi uzeeni.
Kagera
 
Kwa sisi wapambanaji hakuna penyewe hatuwezi ishi tunaishi popote cha muhimu pesa
 
Popote kusiwe na wanga tu, unalala sumbawanga unaamka masasi🤷‍♂️
 
Kuzuri balaa, fikiria mie nimeishi 1979 to 1984 lkn bado napakumbuka Sana pale regional block, katandala, sumbawanga wenyeji, Regina Mundi, chanji, izia, bangwe, jangwani, mazwi nk. Shule yangu Jangwani Primary school, ndugu zangu walisoma sumbawanga primary school na Mama yetu alifundisha hapo. Nakumbuka kanisa katoliki kila jpili tulikuwa hatukosi enzi za Bab askofu Kalolo Msakila alikuwa jemadari haswa. Nakumbuka ule uwanja wa zamani pale karibu na dimba la Nelson Mandera tulikuwa tunaenda angalia mechi kati ya Ujenzi na RTC, Ujenzi wakipigwa bao. Mdau fika uuone uzuri wa Sumbawanga!
Vp ulijifunza wanga kidogo ?
 
Kagera, lindi, kigoma, simiyu, mpanda na katavi .hayo maeneo napambana sana nisije kuishi huko
Kuna jamaa nimekutana nae kwenye msiba flani ni mhasibu huko Rukwa kaja kula raha jijini anavyopasifia eti Rukwa maisha bure kabisa maharage kilo 700 tu Mahindi debe 5000 maneno meengi nikaona huyu jiji haliwezi.
 
Vp ulijifunza wanga kidogo ?
Hahaha hapana nilichojifunza ni kutega na kula nswa kwenye vichuguu(Kumbikumbi) kula migagi(mabua ya mahindi yakiwa mabichi inakuwa km muwa) uchawi sikuwahi ushuhudia
 
Karibu tena Sumbawanga,usafiri umeimarika sana,waweza kwenda Mbeya na kurudi,fursa nyingi sana sana
Hayo ndo Mambo, mji umekuwa toka enzi za tajiri bhojak na akina Bainz. Nakumbuka Sana Jangwani Inn. Tulikuwa tukikosa maji home Mzee anatupeleka kuchota maji hapo na Mandolini yake, tunapiga na bafu kabisaaa. Hahaha
 
Jau sana lindi
Nilifika Lindi nikielekea Mtwara,pale njiani Ndandahimba sijui Tandahimba niliona vituko 😂😂😂.naona watu wanakimbilia baharini huko kila muda.
Nikauliza hawa wanaenda huko kufanya nini?
Si wakasema wenyeji huko chooni
Jamaa wanaenda kule wanabwaga kimba wanatimua,mawimbi yakija yanaondoka nayo duh nilichoka.
Lindi tukafika hakuna msosi palikua pa hovyo sana.
Fikiria stendi unakosa msosi zunguruka sana mpk tukatafuta taxi atuelekeze ndio kutupeleka nbc club at least tukapata supu kuku.
Mtwara kuna bar nafkiri inaitwa Pentagon ndo tulikua tunashinda hapo,walikua vizuri kwa menyu,huku mahotelini ilikua upuuzi mtupu, vichipsi tomato sauce kibao kipaja unapigwa buku 5.hela nyingi sana miaka hiyo
na ndio msosi wa maana utapata.
At least kwenye ile bar utakuta mbuzi choma , kuku choma, supu na vitu vingi tu.
Expirience yangu huko kusini.
 
Unamdharau bodaboda mkuu?? Kuna jamaa ni bodaboda kwa mwezi anakunja 900k hapo ametoa matumizi yake na kila kitu cha muhimu
We hujaona huu udhi kama una dharau?

So 900k ni pesa kubwa kiivyo?

Nimechukulia boda as general mtu anadharau unamuonesha dharau pia
 
Back
Top Bottom