Mkoa gani hata ukipewa nyumba na gari hauwezi kuishi?

Mkoa gani hata ukipewa nyumba na gari hauwezi kuishi?

Umekaa hapo kwa shemej mguu juu unasubir ule chakula cha mchana alaf undelee kuangalia Tv jion ukazurure huku umevaa soks na malapa meupe jion urud uoge usubir chakula cha jion ala uangalie sultan ya azam tv ndo maana unapata ujasiri wa kuandika huu upuzi
Maisha hajakupiga spana bado
Kweli kabisa Kaka haujapigwa na maisha, kama umepigwa kisawasawa usiombee utatamani kuishi hata pangoni.[emoji16][emoji16]
 
Ila kuna sehemu unaweza kuidharau lakini watu wanafanikiwa hiyo hiyo sehemu..mfano wilaya ya Mwanga Kilimanjaro mi naiona ya hovyo lakini kuna vijana wanakuja na kutajirikia pale pale
 
Wakuu habari za weekend. Bila shaka ni shwari kabisa,

Kuna kitu nimewaza kuhusiana na harakati za utafutaji maisha na utulivu wa familia.

Niende kwenye maada husika mi nimebahatika kuishi baadhi ya mikoa hapa TZ bara na visiwani Pemba na Unguja nimeishi zaidi ya miaka 6 huko ukija bara Dar, Tanga, Atown, Tabora, Dom, Moro, Pwani, Shinyanga, Mwanza, Kilimanjaro, Sgd, kwa kuna Mkoa ambao hata nikipewa nyumba na gari siwezi kuishi ni Dodoma.

Yaani huo mkoa umekaa tofauti kabisa na sehemu nyingi nilizo ishi kuanzia kiuchumi, kijamii, kwa wale watumishi waliolenga kustaafia na kuishi huko hakika waishia kupauka na kunywa za pombe za kienyeji maana sioni future endelevu kabisa kwenye huo mjini na miongoni mwa miji yenye asili ya njaa uvivu na ukame kuna miji kama Tanga Moro au hata Mwanza unaweza ishi na familia bila tatizo tofauti huo mji wa Dodoma ambao wakazi wake wamekimbilia Dar na shughuli zao kwenye machinjio ya wanyama huko Vingunguti, Pugu na biashara ya Bucha

Ni wazi tunapambana na kwa ajili ya kujiandalia maisha bora ya sasa na baadae kwako na vizazi vyako hakikisha haukosei wewe pamoja na kukiweka kizazi chako jangwani kitateseka chagua sehemu sahihi ambayo itakufanya uishi kwa furaha. Kizazi chako ukikiweka jangwani kitashindwa kukusaidia hata wewe mzazi uzeeni.
DAR ES SALAAM DAR ES SALAAM DAR ES SALAAM
 
Naweza kuishi sehemu yoyote as long as ni sehemu ambayo inanifanya nipate mahitaji yangu muhimu.
 
Sumbawanga!
Kuzuri balaa, fikiria mie nimeishi 1979 to 1984 lkn bado napakumbuka Sana pale regional block, katandala, sumbawanga wenyeji, Regina Mundi, chanji, izia, bangwe, jangwani, mazwi nk. Shule yangu Jangwani Primary school, ndugu zangu walisoma sumbawanga primary school na Mama yetu alifundisha hapo. Nakumbuka kanisa katoliki kila jpili tulikuwa hatukosi enzi za Bab askofu Kalolo Msakila alikuwa jemadari haswa. Nakumbuka ule uwanja wa zamani pale karibu na dimba la Nelson Mandera tulikuwa tunaenda angalia mechi kati ya Ujenzi na RTC, Ujenzi wakipigwa bao. Mdau fika uuone uzuri wa Sumbawanga!
 
kweli iasee umeish.huyo msakila alikua yupo huko eenz za Ufipa rukwa
 
Wakinga wa makete nao hawataki hata kusikia habari za kurudi makete[emoji28] ndo maana wanapambana ya hela yote. Kolodeness na vilima vya makete sio poa.
Njombe kuna Hali ya hewa safi sio huko Dar sijui mnapapendea nn.
Mm kwangu nyanda za juu kusini yaani Iringa,Njombe,Mbeya,Songwe na bila kuisahau Swax ni sehemu poa sana kwa kuishi
 
Back
Top Bottom