Mkoa Gani Una Baridi Kupita Yote Tanzania?

Mbishi 4 real

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2014
Posts
640
Reaction score
657
Heshima kwenu washikadau,

Tanzania ina mikoa mingi yenye hali ya hewa ya ubaridi mfano Mbeya,Arusha,Iringa n.k lakini mpaka leo sijajua ni mkoa upi una baridi kali kuliko yote Tanzania.Mwenye data za uhakika naomba anifute tongotongo juu ya hili

Karibuni
 
Kwa kawaida Mkoa wote hauwezi kuwa na baridi kutokana na Jiografia ilivyo, lakini kuna maeneo ya mikoa kuna kuwa na baridi kali zaidi wakati sehemu nyingine ni kawaida. Makete ambayo kwa sasa ipo Mkoa wa Njombe ni sehemu yenye baridi kali zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote ya Tanzania kwa uzoefu wangu wa kuizunguka Tanzania hii, kwani kule kuna hadi theluji inadondoka na pia meeneo ya Rungwe, Makambako na Mafinga Iringa!
 

Uko sahihi mkuu makete inaongoza ila kyela joto kwa mbeya ni wilaya ya rungwe
 

Njombe na Iringa.
 

!
!
Kyela?? au Tukuyu?! kama ni Kyela nina mashaka na uzoefu wako
 
Nadra sana kumkuta mtu au kwenda bar ukute friji kule makete. Hekaheka ni Kitulo na Kikondo wilaya hiyohiyo huko ni theruji kabisa.
 
Kwa mkoa wa Njombe ni sawa lakini mnasahau kutaja MOSHI na MUFINDI, hizi sehemu ni balaaaaaa, pia na Ifunda.


Mnaosema Makambako, ni kweli hapa panabaridi lakini ni baridi ya upepo na haina barafu.
Na mda huu ni joto tu.

Nb.
Japokuwa huku kunasifika kwa baridi lakini dada zetu wao wanakufa kwa fasion, vipedo/skin tait na vitop kama kawa.
 
Makete ndio mwisho, nakumbuka wakati naenda Shule asubui ilikua kawaida kila mwanafunzi kuingia na jiko la mkaa Darasani.

Maana usipopasha moto mikono huwezi kuandika, vidole vinakosa nguvu kabisa na midomo kutetemeka.

Mwezi wa Sita,Saba hadi wa Nane ukilaza ndoo yenye maji nje asubuhi unakuta jiwe la barafu.!
 
Vijana wa siku hizi ni wavivu sana kujitafutia information.
Ukiwa na juhudi ya kuuliza , uwe na juhudi ya kutafuta jibu.

Sasa nakupa majibu niliyopata hapa hapa kwenye mtandao:

Arusha annual average temperature-17[SUP]0 [/SUP]deg C
lowest annual temp -10[SUP]0[/SUP] deg C (lowest 8[SUP]0[/SUP]-9[SUP]0[/SUP] degC)


Mbeya annual average temperature-17 [SUP]0[/SUP]deg C
lowest annual temp -11[SUP]0[/SUP] deg C(lowest 7[SUP]0[/SUP]-8 [SUP]0[/SUP]deg C)

Iringa annual average temperature -19 [SUP]0[/SUP]deg C
lowest annual temp -13[SUP]0[/SUP] deg C(lowest 11[SUP]0[/SUP] deg C)

Tukuyu annual average temperature-20,5[SUP]0[/SUP] deg C
lowest annual temp - 13.5 d[SUP]0[/SUP]eg C(lowest 8[SUP]0[/SUP]-9[SUP]0[/SUP] deg C)


Full kipupwe.
 
mkoa unaoongoza kwa baridi ni Singida sehemu ya Manyoni waqt wa usiku tunalala na makoti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…