Mkoa Gani Una Baridi Kupita Yote Tanzania?

Mkoa Gani Una Baridi Kupita Yote Tanzania?

naijui mikoa mitatu
1.Tanga - lushoto ni balaa
2.Iringa - mufindi mamaaaaa hatar
3.Njombe makete huko ni lawama

Umenikumbusha lushoto....kuoga ilikuwa ni adhabu kwangu na nikilala sigeuki mana kitanda cha baridi
 
Mkoa sijui ingawa nimezunguka karibu miji ya mikoa yote ya Tanzania, Ila kwa sehemu ni kileleni mlima Kilimanjaro tena si kwa Tanzania ni Kwa Africa eti. Ukisema Mbeya naweza kusema hapana maana hata Ruvuma kuna kijiji kinaitwa Njombe ni baridi kuliko hata Njombe mjini
 
Makete ndio mwisho, nakumbuka wakati naenda Shule asubui ilikua kawaida kila mwanafunzi kuingia na jiko la mkaa Darasani.

Maana usipopasha moto mikono huwezi kuandika, vidole vinakosa nguvu kabisa na midomo kutetemeka.

Mwezi wa Sita,Saba hadi wa Nane ukilaza ndoo yenye maji nje asubuhi unakuta jiwe la barafu.!

Poleni mkuu!
 
Vijana wa siku hizi ni wavivu sana kujitafutia information.
Ukiwa na juhudi ya kuuliza , uwe na juhudi ya kutafuta jibu.

Sasa nakupa majibu niliyopata hapa hapa kwenye mtandao:

Arusha annual average temperature-17[SUP]0 [/SUP]deg C
lowest annual temp -10[SUP]0[/SUP] deg C (lowest 8[SUP]0[/SUP]-9[SUP]0[/SUP] degC)


Mbeya annual average temperature-17 [SUP]0[/SUP]deg C
lowest annual temp -11[SUP]0[/SUP] deg C(lowest 7[SUP]0[/SUP]-8 [SUP]0[/SUP]deg C)

Iringa annual average temperature -19 [SUP]0[/SUP]deg C
lowest annual temp -13[SUP]0[/SUP] deg C(lowest 11[SUP]0[/SUP] deg C)

Tukuyu annual average temperature-20,5[SUP]0[/SUP] deg C
lowest annual temp - 13.5 d[SUP]0[/SUP]eg C(lowest 8[SUP]0[/SUP]-9[SUP]0[/SUP] deg C)


Full kipupwe.

simplistic interpretation
 
Kwa kawaida Mkoa wote hauwezi kuwa na baridi kutokana na Jiografia ilivyo, lakini kuna maeneo ya mikoa kuna kuwa na baridi kali zaidi wakati sehemu nyingine ni kawaida. Makete ambayo kwa sasa ipo Mkoa wa Njombe ni sehemu yenye baridi kali zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote ya Tanzania kwa uzoefu wangu wa kuizunguka Tanzania hii, kwani kule kuna hadi theluji inadondoka na pia meeneo ya Rungwe, Makambako na Mafinga Iringa!

Acha uongo Kibo katika mlima kilimanjaro ndo inaongoza kwa baridi kwani joto lake mara nyingi ni below 0c
 
Kuna sehemu moja hivi kunaitwa kitulo, sijui ni mkoa wa Njombe ule.....!
 
Lakini jambo moja kuhusu baridi kali. Je ni kwa nyakati gani za mwaka? Inamaanisha hayo maeneo ya baridi ni baridi mwaka mzima.

Mtujuze ili tujipange mtu anapotaka kutembelea huko.
 
Kuna sehemu moja hivi kunaitwa kitulo, sijui ni mkoa wa Njombe ule.....!

hiyo iko njombe makete mkuu, njombe inaongocggtza, kunakipindi hadi barafu inaanguka, majani na miti vinaungua kwa baridi kama vile imeunguzwa moto.mambo ya nyamuyuya
 
Back
Top Bottom