Mkoa Gani Una Baridi Kupita Yote Tanzania?

Mkoa Gani Una Baridi Kupita Yote Tanzania?

Hivi Makambako iko mkoa wa Iringa au Njombe? Nililala Makambako siku moja kitandani wametandika blanket na nikajifunika blanket na nililala na nguo lakini nilikuwa natetemeka kama kifaranga kanyeshewa mvua.
 
Mkoa sijui ingawa nimezunguka karibu miji ya mikoa yote ya Tanzania, Ila kwa sehemu ni kileleni mlima Kilimanjaro tena si kwa Tanzania ni Kwa Africa eti. Ukisema Mbeya naweza kusema hapana maana hata Ruvuma kuna kijiji kinaitwa Njombe ni baridi kuliko hata Njombe mjini

Tukiwa Germance point(sijui kuiandika,tamka gilmansi point)kuelekea uhuru(kilele cha mlima Kilimanjaro)tulikutana na dada wa Kibelgiji analia ameshindwa kuendelea kupanda mlima sababu ya baridi,kule kamasi zinakutoka huwezi kuzipangusa.
 
Hivi Makambako iko mkoa wa Iringa au Njombe? Nililala Makambako siku moja kitandani wametandika blanket na nikajifunika blanket na nililala na nguo lakini nilikuwa natetemeka kama kifaranga kanyeshewa mvua.

Ni Njombe mkuu,pale napo balaa,ndani ya mwaka ni miezi miwili ya unafuu(sio joto).
 
Mh. Hakuna sehemu ya baridi kama sehemu moja inaitwa nainokanoka ngorongoro. Kwingine kote mnatania tu. Huko hakuna cha mwezi wa sita wala wa saba. Ni full baridi muda wote. Jina lenyewe ni la kimasai lakini linamaanisha ukungu ukungu
 
hatar tupu huko unakutana na wazungu hata sweta hana
 
Kimara kuna baridi kuliko sehemu nyingine. hasa waqt wa usiku wa manane
 
Kwa kawaida Mkoa wote hauwezi kuwa na baridi kutokana na Jiografia ilivyo, lakini kuna maeneo ya mikoa kuna kuwa na baridi kali zaidi wakati sehemu nyingine ni kawaida. Makete ambayo kwa sasa ipo Mkoa wa Njombe ni sehemu yenye baridi kali zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote ya Tanzania kwa uzoefu wangu wa kuizunguka Tanzania hii, kwani kule kuna hadi theluji inadondoka na pia meeneo ya Rungwe, Makambako na Mafinga Iringa!
sahihi
 
Mkoa wa Njombe wilaya ya makete kuna baridi sana. huwa kuna theluji yaanguka katikati ya mwaka.
Wakinga wanaitwa theluji ing'ala. ukiamka asubuhi unaweza dhania upo antarctica.
wanaachaga ndoo ina maji bila kufunika then asubuhi wanakuta barafu.
 
Kilimanjaro, kwenye kilele cha mlima (Kibo). Mzee hyo ni mwaka mzima, masaa yote
 
Back
Top Bottom