Mkoa Gani Una Baridi Kupita Yote Tanzania?

Mkoa Gani Una Baridi Kupita Yote Tanzania?

Kwa kawaida Mkoa wote hauwezi kuwa na baridi kutokana na Jiografia ilivyo, lakini kuna maeneo ya mikoa kuna kuwa na baridi kali zaidi wakati sehemu nyingine ni kawaida. Makete ambayo kwa sasa ipo Mkoa wa Njombe ni sehemu yenye baridi kali zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote ya Tanzania kwa uzoefu wangu wa kuizunguka Tanzania hii, kwani kule kuna hadi theluji inadondoka na pia meeneo ya Rungwe, Makambako na Mafinga Iringa!
Sure
 
Tanga licha ya Lushoto, milima ya Magoroto na Amani, Muheza ni balaa
 
Kwa kawaida Mkoa wote hauwezi kuwa na baridi kutokana na Jiografia ilivyo, lakini kuna maeneo ya mikoa kuna kuwa na baridi kali zaidi wakati sehemu nyingine ni kawaida. Makete ambayo kwa sasa ipo Mkoa wa Njombe ni sehemu yenye baridi kali zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote ya Tanzania kwa uzoefu wangu wa kuizunguka Tanzania hii, kwani kule kuna hadi theluji inadondoka na pia meeneo ya Rungwe, Makambako na Mafinga Iringa!
Hili ndo jibu sahihi
 
Moshi kibosho kule asubuhi barafu ni jambo la kawaida....... Fridges ni urembo tu.... Maziwa ili yawe mtindi lazima uyaweke kwenye dari na uweke katikati ya nguo nyingi sana ndio yagande..... Kupasuka miguu ni kawaida sana kule...
 
Njombe kitulo huko hadi snow unaipata .kuoga Mara moja kwa wiki
 
Mkoa sijui ingawa nimezunguka karibu miji ya mikoa yote ya Tanzania, Ila kwa sehemu ni kileleni mlima Kilimanjaro tena si kwa Tanzania ni Kwa Africa eti. Ukisema Mbeya naweza kusema hapana maana hata Ruvuma kuna kijiji kinaitwa Njombe ni baridi kuliko hata Njombe mjini
Pamoja na hilo pale marangu na kilema pana barid la kawaida tu
 
Nikiwa likizoni Makete June na July watoto huwa wanaweka maji nje kwenye suguria just for funny. ...asubuhi ni barafu. Chakula kinaweza kaa hata wiki bila kuchacha.....Unaweza pia amuka asubuhi kijiji kizima ni barafu maridhawa.....
 
Back
Top Bottom