Mkoa wenye baridi kali sana na kwa muda mrefu kwa mwaka (miezi 6+) ni Njombe. Mwaka mzima Njombe ni baridi hasa maeneo ya Makete, Njombe mjini na Makambako. Maeneo hayo baridi miezi ya juni hadi September baridi hushuka hadi 0, na barafu hudondoka usiku na asubuhi, mimea kama mboga , nyasi na migomba huungua kabisa na baridi. Miti ulaya yote hustawi sana maeneo haya. Maindi hukaa shambani miezi 8 hadi 9 kufikia kuvunwa. Jua hutoka lote bila wingu lakini halizuii kabisa baridi. Sehemu nyingi ni ukungu zaidi
Iringa
Maeneo ya Mufundi, kilolo na Iringa mjini kidogo.
Mbeya
Maeneo ya Mbeya vijijini yanakopakana na makete kwenye milima ya iporoto na vijiji vya Igoma , iwalanje. Pia Mbeya mjini kidogo, Maeneo ya Rungwe ni baridi ya kawaida hasa asubuhi na jioni na hasa ni kutokana na mlima rungwe. Mchana kuna joto ,na maeneo yenye mvua mwaka mzima.
Tanga
Maeneo machache ya lushoto. Baridi ya kawaida
Kilimanjaro
Maeneo ya chini kidogo ya mlima, kilema, marangu juu, Rombo juu, baridi ya kawaida na inayoambatana na mvua za milimani
Sehemu nyingine nyingi za Tanzania hupata baridi kipindi kifupi sana na nyakati za usiku na asubuhi. Jua likitoka baridi huisha kabisa.