Mkoa Gani Una Baridi Kupita Yote Tanzania?

Mkoa Gani Una Baridi Kupita Yote Tanzania?

ni Njombe alafu mikoa ya Mbeya, Arusha, Iringa(wilaya ya Mufindi), Kilimanjaro na Kagera inafuata
 
Iringa wilaya ya Mufindi nadhani inaongoza maana kuna sehemu wanapaita London walikuwa wanakaa wazungu panafanana na sehemu London ya Uingereza kuanzia mazingira yaani kile kijani kibichi pamoja na hali ya hewa ndio maana wazungu walikuwa wanapapenda sana na mimi kote nimefika ndio maana natoa huo ushuhuda
 
Kwa kawaida Mkoa wote hauwezi kuwa na baridi kutokana na Jiografia ilivyo, lakini kuna maeneo ya mikoa kuna kuwa na baridi kali zaidi wakati sehemu nyingine ni kawaida. Makete ambayo kwa sasa ipo Mkoa wa Njombe ni sehemu yenye baridi kali zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote ya Tanzania kwa uzoefu wangu wa kuizunguka Tanzania hii, kwani kule kuna hadi theluji inadondoka na pia meeneo ya Rungwe, Makambako na Mafinga Iringa!
Ata mimi nimezunguka sana mikoa ya tanzania na nilichogundua atojatofautiana na wewe
 
Heshima kwenu washikadau,

Tanzania ina mikoa mingi yenye hali ya hewa ya ubaridi mfano Mbeya,Arusha,Iringa n.k lakini mpaka leo sijajua ni mkoa upi una baridi kali kuliko yote Tanzania.Mwenye data za uhakika naomba anifute tongotongo juu ya hili

Karibuni

Kiltulo shamba la kondoo wa sufi
 
Heshima kwenu washikadau,

Tanzania ina mikoa mingi yenye hali ya hewa ya ubaridi mfano Mbeya,Arusha,Iringa n.k lakini mpaka leo sijajua ni mkoa upi una baridi kali kuliko yote Tanzania.Mwenye data za uhakika naomba anifute tongotongo juu ya hili

Karibuni

Tafuta mkoa wenye "high fertility rate". Huo ndio wenye baridi kali sana kupita yote.
 
Mbeya kuna sehemu inaitwa isyonje na ndaga hayo Maeneo ni wakati wote kuna baridi ya hatari ukungu na barafu ni kitu cha kawaida tu kama mtu amefika maeneo hayo atakubaliana na mimi
 
Kuna sehemu inaitwa Tabata magengeni mtaa wa Amani karibu na kanisa la Anglican hapo ni full snow kama upo Russia
 
Mkoa wenye baridi kali sana na kwa muda mrefu kwa mwaka (miezi 6+) ni Njombe. Mwaka mzima Njombe ni baridi hasa maeneo ya Makete, Njombe mjini na Makambako. Maeneo hayo baridi miezi ya juni hadi September baridi hushuka hadi 0, na barafu hudondoka usiku na asubuhi, mimea kama mboga , nyasi na migomba huungua kabisa na baridi. Miti ulaya yote hustawi sana maeneo haya. Maindi hukaa shambani miezi 8 hadi 9 kufikia kuvunwa. Jua hutoka lote bila wingu lakini halizuii kabisa baridi. Sehemu nyingi ni ukungu zaidi

Iringa
Maeneo ya Mufundi, kilolo na Iringa mjini kidogo.

Mbeya

Maeneo ya Mbeya vijijini yanakopakana na makete kwenye milima ya iporoto na vijiji vya Igoma , iwalanje. Pia Mbeya mjini kidogo, Maeneo ya Rungwe ni baridi ya kawaida hasa asubuhi na jioni na hasa ni kutokana na mlima rungwe. Mchana kuna joto ,na maeneo yenye mvua mwaka mzima.

Tanga
Maeneo machache ya lushoto. Baridi ya kawaida
Kilimanjaro

Maeneo ya chini kidogo ya mlima, kilema, marangu juu, Rombo juu, baridi ya kawaida na inayoambatana na mvua za milimani

Sehemu nyingine nyingi za Tanzania hupata baridi kipindi kifupi sana na nyakati za usiku na asubuhi. Jua likitoka baridi huisha kabisa.
Unaposema rungwe mchana ni joto ninamashaka na ufaham wako wa kuifaham rungwe be specific msimu upi? Yaan unamaana kwamba rungwe sio sehem yenye barid, ila barid ipo kwa bahati mbaya kwasababu ya mlma rungwe wakati kwa mkoa wa mbeya wilaya yenye bard ni rungwe. Na hakuna mkoa ambao through out the yr ni barid tuuu
Na unapo specfy mikoa ya barid huwez ongelea joto kwamba ndo limetawala kwa kpindi kirefu cha mwaka kwa mikoa hiyo as if ni kero mfano joto la njombe, arusha, klm, iringa, huwez sema kuna joto kwamba imekuwa kero kwa wakazi japo kuwa kuna msimu wa joto upo lakini linakuwa ni la kawaida
 
Mkoa wa Njombe wilaya ya makete kuna baridi sana. huwa kuna theluji yaanguka katikati ya mwaka.
Wakinga wanaitwa theluji ing'ala. ukiamka asubuhi unaweza dhania upo antarctica.
HII YA UKWELI KABISA NIMEISHI HUKO MIAKA 18 HASA MAENEO YA KITULO,UJUNI MAKETE MJINI NA KATA YA LUPALILO. ILA SISI TULIKUWA TUNAWEZA KUTEMBEA PEKU PAMOJA NA BARAFU YOTE HIYO.
 
Back
Top Bottom