Mkoa Gani Una Baridi Kupita Yote Tanzania?

Mkoa Gani Una Baridi Kupita Yote Tanzania?

Kwa kawaida Mkoa wote hauwezi kuwa na baridi kutokana na Jiografia ilivyo, lakini kuna maeneo ya mikoa kuna kuwa na baridi kali zaidi wakati sehemu nyingine ni kawaida. Makete ambayo kwa sasa ipo Mkoa wa Njombe ni sehemu yenye baridi kali zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote ya Tanzania kwa uzoefu wangu wa kuizunguka Tanzania hii, kwani kule kuna hadi theluji inadondoka na pia meeneo ya Rungwe, Makambako na Mafinga Iringa!
kwa tanzania hii hakuna sehem yenye baridi kama hiyo.
 
Heshima kwenu washikadau,

Tanzania ina mikoa mingi yenye hali ya hewa ya ubaridi mfano Mbeya,Arusha,Iringa n.k lakini mpaka leo sijajua ni mkoa upi una baridi kali kuliko yote Tanzania.Mwenye data za uhakika naomba anifute tongotongo juu ya hili

Karibuni

mkoa wote hauwezi kuwa na baridi lakini kwa ujumla ni mkoa wa njombe na iringa.
 
arusha hasa maeneo ya ILBORU,SANAWARI,SAKINA NA NGARAMTONI
 
kuna maeneo ya bonde la ufa sehem za mbulu ,karatu na ngorongoro pia kuna kipindi kuna baridi kali sana niliwahi kufika huko
 
kuna maeneo ya bonde la ufa sehem za mbulu ,karatu na ngorongoro pia kuna kipindi kuna baridi kali sana niliwahi kufika huko

uko sahihi ngorongoro panatisha mkuu
 
Kagera lakin mara nyingi ni asubuh sana na jioni, Mbeya katika sehemu za Tukuyu na Ushirika, Moshi maeneo ya Marangu juu, kilema, Iringa sehemu za Mafinga.
 
Lushoto....marangu...na mfindi..hizi sehemu nilitembelea yani hata kushika kikombe sikuweza....na ilikuwa mwezi wa saba...
 
Hata vijana wa mungai nao hawako nyuma,sababu ujinga ndiko ulikoanzia
 
Back
Top Bottom