Kwahiyo ulitarajia aongee wazi wazi mpango wa kuifanya Chato kuwa mkoa wakati kila mmoja anafahamu haina sifa?! Tafakari: Baada ya kuwa rais tu, akahakikisha uwanja mkubwa wa ndege unajengwa! Ikajengwa hospitali ya rufaa ya kanda ya kanda ya Chato(yaani badala ya kujengwa Geita ikaenda kujengwa Chato)! Akahahakikisha TRA wanajenga jengo kubwa! NHC ikapeleka mradi wa nyumba! Ikajengwa bohari ya madawa! Kama haitoshi, wakaanzisha Mbuga ya Bugiri ambayo hata hivyo wanyama kama simba ikabidi watolewe kwingine na kupelekwa Chato, akaanza hadi mtindo wa kupokea wageni wa kitaifa kutokea Chato!Yote hayo yalifanyika ndani ya miaka 5! Saa bado tu huoni hayo yalikuwa maandalizi ili hata itakapotangazwa rasmi ionekane Chato ina sifa?
Pamoja na hayo, msikilize Samia hapa siku ya maziko ya JPM
View: https://www.youtube.com/watch?v=UmeRoTwBg54
Ili nisikuchoshe, anzia Dakika 1 Sekunde 55