Mkoa upi ulikinukisha kisawa sawa, tupe top 5 yako

Mkoa upi ulikinukisha kisawa sawa, tupe top 5 yako

Swali: katiba yetu inaruhusu maandamano?

Swali: inahitaji kundi liwe na kibali ili waandamane?

Swali: Swali, wiki moja kabla ya maandamano.... inawezekana wananchi ama Watanzania wakajichukulia mahitaji yao ya chakula nyumbani ya kutosha wiki nzima. Halafu siku ya tukio, hakuna mtu anatoka nje hata mifugo haifunguliwi bandani isipokuwa wagonjwa kuelekea hospitali. Wanaobaki wote wanaandamana kwa amani kwa kubaki majumbani. Wanafunzi hawaendi shule, barabara nyeupe hakuna bodaboda wala bajaji wala daladala. Nchi yote hakuna shughuli inayoendelea kwa wiki nzima zaidi ya hospitali. Je, maandamano ya namna hiyo nayo yanahitaji kibali?

Ama watafwatwa majumbani watoke nje ili nchi iendesheke...!!??

Mwenye kufahamu nisaidie majibu tafadhali.
Hiyo ndiyo protest ambayo haiwezi kumwaga damu! Tatizo vaccum ya uongozi kwa ccm na vile vile Vyama vya upinzani.
 
Swali: katiba yetu inaruhusu maandamano?

Swali: inahitaji kundi liwe na kibali ili waandamane?

Swali: Swali, wiki moja kabla ya maandamano.... inawezekana wananchi ama Watanzania wakajichukulia mahitaji yao ya chakula nyumbani ya kutosha wiki nzima. Halafu siku ya tukio, hakuna mtu anatoka nje hata mifugo haifunguliwi bandani isipokuwa wagonjwa kuelekea hospitali. Wanaobaki wote wanaandamana kwa amani kwa kubaki majumbani. Wanafunzi hawaendi shule, barabara nyeupe hakuna bodaboda wala bajaji wala daladala. Nchi yote hakuna shughuli inayoendelea kwa wiki nzima zaidi ya hospitali. Je, maandamano ya namna hiyo nayo yanahitaji kibali?

Ama watafwatwa majumbani watoke nje ili nchi iendesheke...!!??

Mwenye kufahamu nisaidie majibu tafadhali.
Machafuko kidogo yanapaswa kutokea, hii ni ishara ya hasira kwa watawala. Kwa mfano uchaguzi ni total haukufanyika. Watu waliwasusia na wakajitangaza washindi kwa 98%. Na sasa wanaitawala tena hii nchi kwa miaka mi5. Kuwawekea migomo hawa mbwa wanaweza kuendelea kukaza na mahitaji yako yakiisha utatoka nje kwa ajili ya kutafuta mwengine. Nyani hushuka mtini kwa njaa zake.
Sie wenyewe ndio tumewapa nafasi ya kupumua. Tungeendelea ile alhamisi na ijumaa biashara ingeisha. Japo madhara yangejuwa makubwa sana. Ila hii serekali ingeanguka.
 
WaGEITA walichelewa kuanza ila walikinukisha hatar

Nazan ndo sehemu ambacho machafuko yamedumu siku nyingi

Mochwari za Geita zilijaa,ikabid maiti zingine zipelekwe sengerema na mwanza
Hatari mzee siyo ya kusimuliwa niliingia shift ya usiku Daaah kulikuwa na wanywaranda walikuwa wanamimina moto Bara.

Lakini watu wamepinda kama unavyojua ilikuwa afe panya afe paka.

Kuna watu walitoka mgusu asee wale jamaa nina uhakika ni wajeda walioasi walikuwa wanakinukisha sio poa. Niishie hapa
 
Swali: katiba yetu inaruhusu maandamano?
Ndiyo. Ibara 20(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inamtambua “uhuru wa mtu kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, … kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine” — yaani haki ya mikutano na maandamano ya amani. Uhuru huo unaweza kuzuiwa tu kwa “masharti ya sheria za nchi” endapo udhibiti huo unahitajika kulinda usalama, amani, afya, maadili au haki za watu wengine.
 
Swali: inahitaji kundi liwe na kibali ili waandamane?
Kwenye maeneo ya UMMA (barabarani, viwanjani, n.k.) maandamano hufungwa na masharti ya Sheria ya Polisi na Huduma Saidizi (Police Force and Auxiliary Services Act, Cap. 322).

• Kifungu 43(1) cha sheria hiyo kinalazimisha yeyote “anayenusudia kuandaa mkutano au maandamano katika sehemu ya umma” kuwasilisha TAARIFA YA MAANDISHI kwa mkuu wa polisi wa eneo husika si chini ya saa 48 kabla ya tukio, akieleza mahali, muda na madhumuni ya mkutano/maandamano.

• Polisi wanaweza kutoa “stop-order” kama wanao ushahidi kuwa maandamano yatavunja amani, kuhatarisha usalama, n.k. (kifungu 43(3). Ikipuuzwa, mkusanyiko huo hutangazwa “unlawful assembly” (kifungu 45) na washiriki wanaweza kushtakiwa (kifungu 46(1).

Hivyo, kisheria unahitaji kutoa taarifa (de facto kibali) kwa polisi kabla ya maandamano ya wazi.
 
Swali: Swali, wiki moja kabla ya maandamano.... inawezekana wananchi ama Watanzania wakajichukulia mahitaji yao ya chakula nyumbani ya kutosha wiki nzima. Halafu siku ya tukio, hakuna mtu anatoka nje hata mifugo haifunguliwi bandani isipokuwa wagonjwa kuelekea hospitali. Wanaobaki wote wanaandamana kwa amani kwa kubaki majumbani. Wanafunzi hawaendi shule, barabara nyeupe hakuna bodaboda wala bajaji wala daladala. Nchi yote hakuna shughuli inayoendelea kwa wiki nzima zaidi ya hospitali. Je, maandamano ya namna hiyo nayo yanahitaji kibali?

• Kifungu 43 kinahusu “assembly or procession in any public place”. Kukaa nyumbani kwa hiari si mkusanyiko katika sehemu ya umma, kwa hiyo hakifunikwi na kifungu hicho; hakuna wajibu wa kutoa notisi au kuomba kibali ikiwa watu hawakusanyiki barabarani.

• Kitaaluma, kitendo hicho kinajulikana kama civil disobedience/strike/boycott. Kikatiba hakuna kosa mtu kubaki nyumbani, ila:

– Wafanyakazi waajiriwa wanaweza kuchukuliwa hatua za nidhamu za kikazi au kuvunja sheria za ajira endapo hawajafuata taratibu za mgomo zilizowekwa na Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini.

– Watumishi wa “huduma muhimu” (hospitali, umeme, maji n.k.) wako chini ya sheria za kudhibiti migomo katika sekta hizo.

– Serikali inaweza, chini ya Sheria ya Ulinzi wa Jamii au sheria za dharura, kuamuru watu watoke (mf. wakati wa marufuku ya kutotoka nje/lock-down); kutoitii amri halali ya dharura ni kosa.

– Wanafunzi kutohudhuria shule kunaathiri kanuni za elimu lakini si kosa la jinai.
Kwa kifupi: “stay-at-home protest” haina hitaji la kibali cha polisi kwa sababu si mkusanyiko wa hadharani; lakini washiriki wanaweza kuathiriwa na taratibu za kikazi, shule au amri nyingine za kisheria endapo serikali itazitoa.
 
Ama watafwatwa majumbani watoke nje ili nchi iendesheke...!!??
Je, polisi wanaweza “kuwafuata majumbani” wawatoe ili nchi iendelee?

Kisheria hawawezi kumlazimisha mtu kutoka nyumbani bila amri halali:

• Polisi wana mamlaka ya kuingia nyumbani tu kwa kibali cha mahakama, kubaini uhalifu, au kutekeleza amri/ sheria za dharura.
• Iwapo serikali itatoa tamko la dharura (state of emergency) au amri ya kutotoka nje, basi kukaidi amri hiyo ni kosa. Bila tamko hilo, kukaa nyumbani ni haki ya kibinafsi.
 
Mnakinukisha then mnafungiwa ndani, kisha kilo moja ya mchele mnauziana 5,000/=, kilo moja ya nyama mnauziana 15,000/= hadi 17,000/=, mnachoma vituo vya mafuta (sheli), mnapofunguliwa lita moja mnauziwa 5,000/= hadi 6,000/= na vile vituo mlivyoviacha salama.
Wewe si bado unauziwa kilo 2000 sio?
 
Hatari mzee siyo ya kusimuliwa niliingia shift ya usiku Daaah kulikuwa na wanywaranda walikuwa wanamimina moto Bara.

Lakini watu wamepinda kama unavyojua ilikuwa afe panya afe paka.

Kuna watu walitoka mgusu asee wale jamaa nina uhakika ni wajeda walioasi walikuwa wanakinukisha sio poa. Niishie hapa
Hao wa mgusu walikuwa na silaha zozote?
 
Back
Top Bottom